Meneja Masoko wa kampuni ya Selcom Pay Point Bw.Juma Mgori akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na uboreshaji wa kukata tiketi za mabasi yaendayo mikoani kwa njia rahisi za mtandao(Mobile Ticketing) Katikati ni Mkurugenzi wa Biashara na Maendeleo wa Kampuni ya Mobile Ticketing Timited, Constantine (Costa) Kumalija
Afisa Maendeleo ya Biashara Mobile Ticketing Limited Bw.Albert Muchuruza akiwaonesha waandishi wa habari njia muhimu za kukata tiketi za mabasi kwa njia ya Mobile Ticketing kwa wasafiri wanaotumia mabasi yaendayo mikoani,anaeshuhudia kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo Juma Mgori.

KAMPUNI ya Mobile Ticketing Tanzania Limited imezidi kuboresha huduma zake kufuatia kurahisisha zaidi upatikanaji wa tiketi za kusafiria kwenye Selcom Pay Point kama zinavyopatikana huduma nyingine muhimu nchini.

Uboreshaji huo umekuja kutokana na kampuni hiyo kutambua umuhimu mkubwa wa huduma hiyo katika jamii ili kuzidi kuwarahisishia hata wale wasiokuwa na simu za mikononi waweze kupata huduma hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini,Afisa Maendeleo ya Biashara wa kampuni hiyo, Albert Muchuruza, alisema kuwa amefikia uamuzi wa kuwa na huduma hiyo huku ikiendelea kushirikiana na Vodacom kwaajili ya kuhakikisha huduma hiyo ya tiketi popote inamfikia kila mwananchi hapa nchini.

"Tuko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha vitu vichache japo huduma hii ya upatikanaji wa tiketi za Usafiri wa Mabasi wa Mabasi kupitia wakala wa Selcom Pay Point kama zinavyopatikana huduma nyingine za kulipia ANKARA za maji, umeme, ving'amuzi nk, imeshaanza kutumika hapa nchini lengo likiwa ni kuhakikisha huduma hii inapatikana kwa urahisi zaidi na kumfikia kila mtu.

Aidha, Muchuruza alisisitiza kwamba huduma hiyo ya upatikanaji wa tiketi kwenye selcom pay point imekwishaanza kufanya kazi siku chache zilizopita na kuiomba jamii itambue mchango wa kampuni yake ambao ni kurahisisha na kuweka huduma kama hiyo karibu na jamii kitu ambacho ni uzalendo.

Mbali na hayo, pia Muchuruza alisifu muitikio chanya wa wananchi juu ya utumiaji wa huduma hiyo ya tiketi popote na kusema kuwa tathmini iliyofanywa na kampuni yake inaonyesha kuwa jamii imeanza kutambua na kuelewa umuhimu na matumizi sahihi, hadi sasa muitikio ni mkubwa na wenye kuridhisha kwa kipindi kifupi cha mwezi mmoja tangu huduma hiyo kuzinduliwa mapema mwezi uliopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2012

    nawapongeza kwa kuleta huduma hii, itakupunguza usumbufu hasa wa wale wapiga bede pale ubungo

    ReplyDelete
  2. Huyo wa katikati sio Albert Muchuruza, wa Kulia ndio Albert Mwenyewe, halafu ndio Managing Director

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2012

    nawapongeza sana. ila nana hawajatueleza kuwa tunawapataje au tunafanyaje kuwapata

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 04, 2012

    hongera, tutaepukana na wale wenye mabasi ya mijampora wakati wa mwisho wa mwaka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...