THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Mkataba wa mradi wa umeme wa Stiegler’s wasainiwa jijini Dar

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA), Bw. Aloyce Masanja (kulia) akibadilishana nyaraka za makubaliano ya awali ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa umeme wa Stiegler’s pamoja na Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya Odebrecht ya Brazil, Bw. Fernando Soares leo jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni mwanasheria wa kampuni hiyo, Bw. Tiago Matos (kushoto); Mwenyekiti wa Bodi ya RUBADA, Prof. Raphael Mwalyosi (mwenye miwani katikati) na Mkurugenzi wa Mipango wa RUBADA, Bi. Tatu Ndataro (kulia).


Kuna Maoni 4 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Wa-Tanzania achaneni na ushamba huo wa "leboozi" kwenye mikono ya suti!

  Ni aibu jamani!

  Mwmabieni huyo Masanja kuwa "fashinita" kasema!

 2. Anonymous Anasema:

  Hii mikataba imepitiwa kweli?? isije kuwa Richmond!!

 3. Anonymous Anasema:

  Jamani tufahamisheni tujue, je ?? hawa stieglers ,tutanunua umeme moja kwa moja kutoka kwao ????? au ndo yale yale ?? wao wawauzie Tannesco halafu Tannesco watutapeli siye. Tumechoka na Tannesco. Kwa nini isiwe kama simu au mabenki,unaona jinsi ushindani ulivyoturahisishia maisha ?? zamani ilikuwa benki moja tu ya NBC-yaani unapanga foleni hapo mpaka magoti yanafika kwenye utumbo,simu nazo ilikuwa TTCL peke yake-yaani unatukanwa na operator lakini una vumilia tu la sivyo ukifanya mdomo basi hakuunganishi n'go, yaani ilikuwa kero bin shida na hii ilichangia sana watu kuikimbia nchi yetu Tanzania. Mungu umetutoa mbali. Sasa tuko semi fainali, tukimuondoa Tannesco na kuweza kupata umeme wa uhakika na wa gharama nafuu !!!! Peponi tutakuwa tumefika. Mungu ,hatupi viumbe vyake. Babu yangu Zebedayo akifufuka leo anikute nina simu ya mkono wachilia mbali TV ambayo atataka akawashike wale wanaoongea ndani ya TV, lazima atasema ,Tanzania sasa ni mbinguni. ( tumetoka mbali ) Zebedayo msema kweli.

 4. Anonymous Anasema:

  KAMA SERIKALI YETU NI YA UWAZI, NI VYEMA MIKATABA HII INGEWEKWA KWENYE GLOB KWANZA ILI WANANCHI (NDIO WENYE NCHI AMBAO MWISHO WA SIKU TUNAUMIA NA UPANDISHWA WA GHARAMA ZA UMEME HOVYO HOVYO) TUIPITIE.

  HII ITASAIDIA MACHO YA WANANCHI WENGI KUIPITIA NA KUGUNDUA KASORO NA MAPUNGUFU YANAWEZA KUJITOKEZA.

  JICHO LA 3 NI SIE WANANCHI, TUPEWE FURSA YA KULIKOMBOA TAIFA LETU KUTOKA KWENYE MIKATABA MIBOVU.

  KAMA KWELI TUPO KWENYE ZAMA ZA UWAZI NA UKWELI, BASI NI VYEMA HII MIKATABA NAYO IWEKWE WAZI ILI WANANCHI TUIPITIE KWANZA.