Brother Michuzi,
   Kwanza nikushukuru kwa kazi ya kutuunganisha, niseme kwamba nimekuwa addicted na blog yako make hakuna siku inapita bila kuicheki.  Naomba kwa ruhusa yako niulize wadau haya yafuatayo...
  
    Mimi ningependa kuuliza kwa wale ambao wamekaa nchi za Magharibi(Ulaya na Marekani). Je mnafikiri ndoa ni ngumu Marekani na Ulaya kuliko nyumbani (Tanzania)? Nimeoa dada wa kitanzania na kusema ukweli kile nilichokuwa naona kwenye ndoa za Tanzania kama heshima, kusaidiana, na kusikilizana sivioni kabisa huku. Dada zangu  wa kiafrika nawapenda saana ila nashangaa kila nikiongea na kina kaka wanalalamika kwamba kina dada wakifika huku wanaota mapembe. Juzijuzi kuna mtu aliniambia kwamba dada zetu walivyofika Ulaya na Marekani waka­-demand haki zaidi ya zile za wenyeji;  kwamba ni bora kuoa mwenyeji wa huku kwani unajua tayari nini unachodeal nacho. Siku hizi dada zetu saa nyingine hata kama hafanyi kazi bado ukitoka kazini anakwambia "nilikuwa naangalia program zangu kwenye TV kanunue chakula ule."
  
  Sasa nauliza hivi ni kweli mambo yamebadilika dunia nzima kwa swala la ndoa au ni dada zetu walivyofika huko wamebadilika?
 
Naomba nisaidiwe make naona mimi na mama watoto wangu saa nyingine hatuelewani kabisa kwenye hii swala.

Mdau Majuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2012

    Women are empty boxes when are married. If you don't fill in the box with what you want to be filled in, others will do it for you but with what they want to fill. So, if you brought a woman all the way from Africa and when she was there you didn't fill her with what you wanted, then she has been filled in by others with what they wanted.
    Sisi Waafrika tunaponzwa na kuiga maisha ya watu weupe. Mwanaume anaoa mke afu ananza kumdekeza, oooh honey, darling, sweetheart...na kumbebea mikoba mnapotoka na kila aina ya midekezo. Sasa wanawake huwa wana tabia ya kupitiliza. Ukianza hivyo, naye anafanya zaidi. Matokeo yake ndo hayo. Kama hukumzoesha mwenyewe tangu mwanzo, kamwe hawezi kuanza tu ghafla. Mkija kuoa huku mnazidisha mbwembwe za uzungu.

    Pole sana, umebugi step mkuu. Ukimchekea nyani shambani, utavuna mabua.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2012

    Hawa dada zetu siyo suala la majuu.Ni wasumbufu hata huku Tanania.Jitahidi umvumilie huyo.Wakiwa wanatafuta kuolewa wana-act wapole sana.Wakishaingia 'mjengoni' wanakuwa 'mnyama tofauti'.Bottom line ni kwamba ndoa yoyote inahitaji uvumilivu uwe Ulaya,Amerika,Asia au Afrika.Mbaya sana ukitaka kujikomboa kwa kuanzisha 'chama cha Upinzani'(Sikushauri uanzishe chama cha Upinzani) wanalalamika sana,ingawa chama cha upinzani kinasaidia kuwanyoosha hao akina mama jeuri.

    David V

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2012

    you are not alone..........
    It is sad, all but true. Masikini akipata..........................
    Sometimes however, in some cases we are to blame in so many ways.....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2012

    umeona eeh! halafu watu wakikimbilia watasha mnasema......oooh wanababaika ...mara hivi. Mimi ni M-bara, tena wa asili, na visiwani sijafika kabisaaa na wala sina link nako, lakini kwa utafiti wangu wengi wa dada zetu wenye asili ya visiwani hawana matatizo kama haya kabisaaaa! nakupa uhakika hasa kwa hapa UK. Wao huwaenzi waume ama wenza wao kama vile huko kwetu. Lakini hawa wetu wa Bara..duh! utamalizia mwenyewe

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2012

    Mkuu, huyo dada umekutana naye marekani au umemfuata Tanzania? Kama wote mmekutana marekani basi makosa ni yako, kwa sababu ulitakiwa umjue naye pia akujue kabla hamjaoana.
    Na kama umemfuata Tanzania basi hilo ni kosa kubwa sana umefanya. Wana dada wa Tanzania hawaoi mume wa marekani, bali wanaioa nchi, kama ni marekani au ulaya. Hata kama hakupendi atakubali tuu kuolewa na wewe na hayo ndiyo matokeo yake.
    Kitu kingine, baadhi yetu sisi wanaume kuna mabwege kama alivyosema mdau mmoja huko juu. Hayo mambo yenya "wow!!! darling zis iz so swiiit" hayo ndiyo matokeo yake.
    Na kuna wajinga wengine wakishafika Ulaya na marekani, wanajitengenea maisha na yakishaanza kukaa sawa wanarudi Bongo kutafuta wanawake ambao walikuwa hawawezi kuwapata wakati wako Bongo. Kama alikuwa hakutaki wakati umechoka kimaisha kamwe usiwe naye wakati mambo yako yanaanza kukaa mswano.

    Na ukichukua Mnugu, (mmarekani mweusi) basi ujue kila ukienda kazi tuu, huku nyuma Tyrone au Clarence anakuja kukusaidia.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2012

    why you people mnaegemea upande mmoja,kwasababu ni mwanaume mwenzenu si ndiyo,not all cases wanawake wanakuwa hivyo bila sababu,mara nyingine wanaume wanafanya vitu vya ajabu at that moment mwanamke anachange,wanawake wengine wako so inocent lakini unakuta mwanaume mlevi,kurudi nyumbani asubuhi,anaspend all time na friends zake,just because yeye ni mwanaume so anataka wewe mwanamke ubaki kuwa chombo no my dear the world is changing mwanamke is not an empty box thats why can lead a parliament which is 80% of your gender.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2012

    Mambo matatu katika ndoa yanachangia: 1)maelewano ktk majukumu ya kila siku;uwiano wa kazi na kipato kati yenu,lazima kuwepo amani suala hili
    2)kuheshimiana;ndani na nje ya nyumba
    3)Kuridhishana,mwanaume please mkeo na vice versa(u know wat i mean). La majukumu,kaka zetu mnatuangusha kwani ulaya hakuna housegirl,so kupika mara mojamoja sio mbaya.Hivyo hali ya maisha afrika iko tofauti kabisa na ulaya sote tuwe flexible tusilaumiane,yote maelewano.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2012

    anayewatetea wanawake hapa atakuwa mwanamke tu, kwn hoja ya ulevi au kuchelewa kurudi nyumbani, huo ni uzushi mtupu, ndoa zoote zina misingi yake, kwenye hii misingi ikisahaulika basi na ndoa haipo, kweli mwanaume atatoka koote huko akachukue mke amlete ulaya au marekani halafu akamtelekeze ukiuliza ulevi, hapa tusidanganyane, wanawake wakwetu ni malimbukeni hawajui nini wanataka, matokeo yake sasa hv na wao baada ya kuachwa na waume, wengine kujiingiza kwenye usagaji, hatimaye wanakwenda nje na wao kuwaowa wanaume ili wawalete ulaya waanzishe maisha, hapo sasa ndy unamkuta mmke anakuwa makini na mtiifu kwenye ndoa, kwani koote kishamaliza na kajionea mwenyewe! lkn huwezi kumkuta mmke wa kighana akawest time yake kwa upuuzi huo!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 23, 2012

    Najisikia vibaya mnasema wana wake wezangu tatizo Kubwa mazingira kwawale tulio letwa tunajisahau wakati mwingine na ukiambiwa unaona kama unasimangwa lakini niukweli mimi binafsi nilikuwa kutwa nachinda kwenye nety kutazama umbea wa udakuni najisahau mpaka kukogo ata kula sikumbuki mwenzangu akiludi akinambia twende madukani tukiwa njiani nalalamika njaa mpaka inafika wakati tunagombana kwanini sili wakati najiandaa kipindi nikijua anakalibia kuja sasa naaza kukulupuka kufanya kila kitu lakini sasa nimezoea naona kawaida ushamba umenisha sasa tunakwenda sawa Nazani ao piya wanajisahau lakini ipo siku watajuwa nini kimewaleta kazi au Mume

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 23, 2012

    Tatizo hilo huwa kwa upande wa wanawake na wanaume, halibagui. Ishu ni kwamba, watu hawaelewi maana ya ndoa, matokeo yake wanaingia kwenye ndoa kama fasheni ("rafiki yangu kaolewa basi na mimi nataka niolewe"). Kumbe kwa bahati mbaya ndoa haitaki mambo ya namna hiyo. Ndio maana migigiro hutokea baina ya wanandoa.

    Mimi bianfsi najitambua kuwa nipo tayari kuwa kwenye ndoa, lakini hadi leo nasita kuoa maana mwenzangu haishi mambo. Yaani ni bora niishi single tu (nazaa tu nje) kuliko kuishi maisha yangu yote kwa huzuni na majuto. Bahati mbaya mtu mwenyewe hata kugombana kwa maneno sijui, akirefusha mdomo tu anakula konde. Kisha najuta sana kwa kumpiga, ila kila nikimkumbusha awe ananiambia dukuduku lake kirafiki tu naye haelewi, ni kupayuka payuka tu.Hii ishu ya 'kuvumiliana' kwa kweli haiingii katika kila jambo eti ili mradi tu mpo katika uhusiano.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 23, 2012

    Si unaona wanawake wenyewe ndiyo wa "no my dear". Sasa huyo mwanaume ambaye ni mlei na anaspend muda wote na rafiki zake, kwanini wewe umekubali kuolewa na chapombe? au ameanza kuwa mlevi baada ya ndoa yenu?

    Ulikuwa unajua kama huyu mtu ni mlevi lakini kwa ajili ya "u-desperado" ukaamua kuolewa na chapombe.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 23, 2012

    E bwana mdau mimi nimeishi ulaya muda mrefu sana ,pia nimeishi USA ,hawa dada zetu hasa wa huko kwetu bara wana usumbufu sana wakiwa huku majuu ,hivyo nashauri kwa wale wote wanaokutana na mademu huku majuu ambao ni wa nyumbani wakae na mademu hao muda mrefu ,hii tabia ya kuoana haraka haraka na kutojuana huwa nin maafa makubwa.Mara nyingi hawa dada zetu huku kutokana na sababu mbali mbali huwa wameshapitia maisha mbali mbali ,pamoja na kulazimika kuuza miili yao inagawa siyo wote ila wengi wao (prostutition) kutkana na life la huku na wanawake huingia ktk biashara hii ili kuongeza kipato chao kwani maisha ya huku ni gharama kibao ,hivyo ndoa na mademu hawa hazikai muda mrefu ni matatizo matupu na nina washikaji kibao ambao wanaishi maerkani na kwa sasa wanalia kwa sababu ya kuoa wabongo,hivyo wanaume kuweni macho ,haya mapenzi ya kujuana huku na mademu wa kibongo siyo wale ambao mmewazoea walioko kule na hata ukiwatoa kule baadhi yao ni matatizo matupu.Mdau ughaibuni

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 23, 2012

    Kila mtu anaongea ukweli, mimi nina miaka zaidi ya 7 huku ugh.. na nilianza maisha ya ndoa huko tz ukweli hali ni mbaya na sijui ninakoelekea maana mamaa hasikii wala haoni na kuniwakia kila ninachomueleza ukweli mguu ndani mguu nje hakuna mapenzi kabisa wala sijui kwa nini nimeoa maana napika mwenyewe, nafua, sipewi penzi na naambiwa kama nataka kwa nini sianzi yaani kwa ufupi hakuna sababu ya kuoa mtz kama unajua maisha yako yatakua nje ya nchi. Wanawake ni watu wanaohitaji kusimamiwa na ndugu wa mwanaume yaani kila wanapowatembelea basi atakua anajaribu kuonyesha umuhimu wa yeye kua mke kwa kifupi najuta sana kuishi nje.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 23, 2012

    Hao ndio WABEIJING bwana!Ukosefu wa maadili na mafunzo ya dini ndio chanzo cha matatizo yote.M/Mungu katuumba tofauti kwa sababu zake hivyo majukumu yetu na uwezo wetu wakiutendaji pia ni tofauti lkn wanapotokea wanaojifanya wanamjua zaidi mwanaadamu kuliko Mwenyezi alietuumba ndipo hapo anapopewa mtu haki na majukumu asiyostahili wala asiyoyaweza.Haya ndio matokeo ya yakujifanya tunadai usawa,tunataka kila kitu sawa mwisho ni familia na jamii kwa ujumla kuparaganyika.Ushauri,wanaume msioe kwakutizama umbile na uzuri wa sura tu bali toeni umuhimu mkubwa zaidi kny tabia na dini ya unaetaka kumuoa hapo ndipo utakaponusurika mkono wako usiambulie mchanga badala ya dhahabu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 23, 2012

    Hupendwi wewe inapendwa pesa. Mdau hapo juu kaeleza vizuri ni kwamba tafuta mke ambaye hata kama huko ughaibuni basi atakupenda tu. Mdau anayesema Wazanzibari wanatulia hiyo sio kwa wote. Tunarudi kule kule hao Wazanzibari waliotulia wote wake zao wametafutiwa na wazee tena ni wale ambao hata kama hawakufika ughaibuni basi bado wataoana. Mfano hapa Zanzibar tunajua kuwa Mpemba au Mmakunduchi akioana na mtu ambaye hatoki sehemu moja basi huwa sio waaminifu. Kuhusu wanawake wakiughaibuni hawa wanaangalia leo tu pia wanapenda kutumia uhuru wao na wengi wao hawafati misingi ya kidini. Sasa kwa wale Wabongo walio ughaibuni wanaofikiri kwa sababu uko ughaibuni unavipesa kuliko mwanamme aliye Bongo basi hiyo ni dhana potofu maana ukishamleta mwanamke wa kibongo halafu ukemuweka kwenye nyumba ya council au project halafu akaona kumbe kazi yako ni security guard au warehouse operative na kigari chako cha toyota avensis cha kukopa basi anajuta kuolewa na wewe bora angebaki bongo akawa na kina Masanja wahasibu wa vodacom wanaoendesha BMW X5 series na holiday dubai kila mwaka!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 23, 2012

    mdau wanaume wa bongo wakiingia ulaya hali ya hewa ulaya inaathiri heshima ya bomba kushuka na kupotea kabisa jogoo anagoma kuwika hata upepee na feni,uliza wote tatizo ndio hilo

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 23, 2012

    wanaume wa ki tz asilimia kubwa hawajui kupika.

    Mie nimeolewa na m west africa tunashindana nani anapika chakula vizuri.

    wa tz wanataka walale wale, hawajalelewa ikiwa wataishi wenyewe watafanyaje

    mnatia aibu kuwa ulaya na kutegemea mke afanye 100% jikoni, maisha ulaya ni kusaidiana 50/50

    ukitaka ubosi rudi tz.

    mjifunze kupika, na kusaidia wanawake zenu ndani ya nyumba usafi pia, i guess ni wachache sana watakuwa hivyo labda asilimia 0.1

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 23, 2012

    Mdau pole sana kwa hali uliyokuwa nayo ila tu ujuwe kwamba hupo peke yako, wako wengi tuu wenye hali kama hiyo. Ikiwa nyooote mnafanya kazi na mnachangia gharama za maisha yenu yote basi ni vyema kusaidiana na hata kazi za nyumbani mnapopata nafasi. Ila ikiwa mke hana kazi, yuko nyumbani tuu, mume akafanye kazi alete pesa ya matumizi ya chakula na kodi ya nyumba na matumizi mengineyo kisha mke huyo hapiki wala hasafishi nyumba (wako wengi tu kama hao) basi huyo mke hafai kabisaaa, ni mzigo asipotaka kujirekebisha.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 23, 2012

    Bro, tena hii mada hii ,ngoja kwanza nikakoroge kahawa. Braza ?? hayo yaliyokukuta !! ni mvua za manyunyu,mbona mambo badoooo!!! siuko majuu,na hapo bado una miaka 40 bado mbichii, subiri sasa ugote 60 na una watoto 3 na wote wamedrop shule na wako kwenye makundi, heleni puani na chini,kurudi nyumbani ni saa 9 za usiku au zaidi,lugha yao siyo Kiswahili ni ile slang iliyojaa F words kila sentence. Huyu Mke atakuacha maana tayari yeye kishajenga kwao Moshi, wewe huna nyuma wala mbele na hao watoto sahau kukupa msaada wowote,sababu hata wao future yao ni matatani na washukuru ,kuna kitu kinaitwa Food stamps,chakula cha dezo. Yaani wewe hapo ulipo,ulisha lose ile mbaya,kama uko na umri wa miaka 40 hadi 45 au chini ya hapo, basi muda bado uko upande wako. USHAURI MADHUBUTI ni huu VUNJA ndoa mara moja, baki single for 5 or 7 years,PIGA box hata sehemu 2 au 3 utachoka lakini vumilia ,utakapogota miaka 50, tayari utakuwa na shamba Mwanalumango au RUVU na tayari utakuwa na nyumba ambayo iko kwenye renta. kumbuka kwamba dola 100 ni sawa na laki moja na nusu shillingi, hiyo ni mifuko 10 ya simenti ambayo ni sawa na tofari 400 safi za simenti, Yaani ,utajikuta umejenga nyumba kilaini mpaka utashangaa.Hiyo dola mia kama utampeleka out huyo limbukeni ,basi mkirudi nyumbani huna kitu zaidi ya cheji chenji tu, siku zinakwenda,stress na pressure zinazidi kukupanda, huko majuu huna raha ,nyumbani hukuwekeza chochote ,kurudi unaona aibu,una watoto ambao huwezi hata kuwatuma maji,ukimpandishia sauti basi ya kwake itakuwa juu zaidi,ukimuachia kibao basi Polisi watatinga mlangoni, huna haki wala faraja , wakati walipokuwa wadogo ,ulinunua nepi na matoi mpaka basi,leo utabaki unajiuliza ,what did i get into ??? .Chukua ushauri wangu leo leo go solo,miaka mitano kaa peke yako ( piga kunyeto inapobidi) you dont need them anyways,they simply cost us time and money. Nijulishe how your life will change in 5 years.After dumping that do nothing,shit disturber. Mimi Zebedayo, daima msema kweli.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 23, 2012

    Sasawewe mwanamkeunakutananaye,ulaya,marecan yeyemwenyewekahangaikakuondoka bongoweweunakutananaye ugaibuni,unategemeahatakuheshimu?yeyeanaondoka hasubui kwamataila,wewekwenye box unategemeaheshima?

    ReplyDelete
  21. MWANAMKE WA KITANZANIAJuly 23, 2012

    KWASABABU MMEZOWEA KUNYENYEKEWA NA WANAWAKE HUKO BONGO NDO MAANA UNALALAMIKA. A WOMAN IS WRONG KUKAA MBELE YA TV SIKU NZIMA HALAFU AKWAMBIE UKANUNUE JUNK FOOD LAKINI WENGI WENU NAONA MMEANDIKA KWA GHADHABU. JIULIZENI NA NYIE KWANINI WANAWAKE WENU WA KIAFRICA WAKIFIKA HUKU WANABADILIKA? KWANINI WENGI SIKUHIZI BORA WAOLEWE NA MZUNGU ATA KAMA HANA KITU LAKINI WANAJUA WATADHAMINIWA NA KUESHIMIWA NA HAO WANAUME WAO NI MORE ROMANTIC? UNAKUTA MWANAUME WA KIAFRICA ANAMAMBO YA KIZAMANIIII.. MWANAMKE AMPIKIE, AMFULIE NA BADO ANAFANYA KAZI LAKINI AT THE END OF THE DAY ATA M TREAT KAMA SI KITU, KISA KAMUOA. BADILIKENI OTHERWISE MTAACHWA, USILAUMI INSTEAD ONGEA NA HUYO MKEO( NA NYIE WENGINE WOTE WENYE GHADHABU) WAULIZENI NININI SHIDA? COMMUNICATION IS THE KEY NA UBABE WA KUWA KICHWA CHA NYUMBA MMEUACHA KULE AFRICA!!!HAYA YOTE NI KWASABABU HAMTAKI CHALLENGES, MNATAKA TU WANAWAKE WATAKAO SEMA NDIYO MUME WANGU!! OTHERWISE KATAFUTENI WANAWAKE WA KULE KIJIJINI NA MUKAE NAO HUKO HUKO MAANA ATAWAO WAKIPATA MWANGA WATAJUA EXACTLY HOW A WOMAN IS SUPPORTED TO BE TREATED.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 23, 2012

    Waaume wa kibongo msilete za kuleta! et wadada wa kitanzania!!!!!!! "do not blame your enemy because you are the one who created her". Yaani lugha ndio tatizo la wanaume. Hawajui kuapreciate hata ungefanya nini. Hata akitoka kazini unampa poe kwa tabasamu anaitikia huku mbio anaelekea kwenye TV au PC. Sasa nitakuheshimu na kutimizia je. You better improve your communication. Wanawaake ni binadamu pia wanahitaji hayo mnayoyahitai pia! Mr Mchuzi usitupe hii plz.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 23, 2012

    We anon wa Sun Jul 22, 11:57:00 PM 2012 umeniacha hoi kinoma, lol.. nimecheka mpaka machozi..

    Sasa tufanye nini? make nikirudi Bongo kumchukua aliyekuwa hanitaki hayo sio mapenzi, nikienda Bush kuchukua Chakubanga yeye anaolewa na Marekani au Ulaya sio mimi. Na hawa kina Shanikwa wana wavuta Bangi pembeni.. Its crazy man..

    Ila the bottom line, nakubalina na mwenye swali ukweli dada zetu wakifika huku wanabadilika saana. Wakiona Kardashians kwenye tv wanataka the same life. Wanasahau hiyo ni show, its not real life

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 23, 2012

    Mithupu mimi napenda saana hizi mada make nachekaaaa mpaka majirani wanauliza kama kuna usalama. We "ZEBEDATO msema kweli" sijui unakaa wapi ila ungekuwa karibu ningeomba tukapate lunch au dinner make comments zako zimenivunja mbavu.

    Man naipenda Bongo, Michuzi mungu akupe nguvu make unatupa raha ya maisha kupitia blog ya jamii..

    ReplyDelete
  25. Tanzanian WomanJuly 23, 2012

    Yaani wanaume wa kibongo nuksi sana..wanapendenda kuendesha wanawake wa kibongo kama gari, kufanyiwa kila kitu kama mtoto mdogo halafu hata shukrani haina..
    Kwanza haipo romantic, kazi kuamrisha tu kama jeshini na vilevile kuona wanawake kama wahudumu wao..
    I begoo, not in my house! Mwanaume atachakarika..nikipika, kaosha vyombo nk. eti itokee nipike na kutenga chakula tumalize kula halafu aache chombo mezani, thubutuuuu!
    Tatizo mkikutana na wanawake wanaowanyoosha mnaona ukosefu wa heshima...kalaghabao!!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 23, 2012

    Na kwa akina dada zetu ambao mmekuja na hoja ya kusema kwamba eti mwanaume anataka apikiwe na afuliwe. Mimi niweishi Uingereza na Marekani na sijawahi kuona nyumba hata moja isiyokuwa na "washing machine" kwa hiyo ilo la kufuliwa nguo ni uongo mtupu.

    Kuhusu kupikiwa ni kweli, wanaume wa ki-bongo wengi wetu hatukulelewa kupika huko nyumbani. Mimi binafsi sijaoa lakini naishi na mwanamke wa kizungu miaka tisa sasa. Kila siku anapika yeye na ana nidhamu nzuri tuu, namuheshimu na ananiheshimu. Tena hili la kupika, kila nikitaka kupika mimi nimsaidie anakataa kwa hoja zake mbili.
    1. Anasema kwamba mimi sijui kupika vizuri

    2. Anasema, "naturally, female species are nurturer", I don't have any issues with cooking for you an my boys.

    Na anafanya kazi, yeye ni mwalimu.

    Tatizo ni kwamba, dada zetu mmeuvamia uzungu, halafu dhana yenu ya uzungu mmekosea. Wengi wenu hamuogopi kuwa single mothers kwa sababu kuna "welfare". Akili fupi zinawatuma kwamba, mtoto akipata chakula akashiba, baba wa kazi gani?
    Wazungu hakuna kitu wanachokiogopa kama dysfunctional family. Dada zetu wanafanya kila linalowezekana kuishi katika dysfunctional family. Matokeo yake wanaolewa na vibabu vizee vya kizungu. Lets face it, wengi wenu mlioolewa na wazungu, waume wenu wamewapita zaidi ya miaka 15. Na wale mlioolewa na wazungu vijana, mumeo anaogopa kukutambulisha kwa familia yake au rafiki zake. Wangapi kati yenu ambao mmeshawahi kufunga safari kwenda kwa wazazi wa mumeo wa kizungu bila ya yeye kuwepo na ukakaa nao angalau wikiendi moja tuu? Jibu unalo mwenyewe. Hamfanyi hivyo kwa sababu mnajua kwamba hamtakiwi na wakwe zenu, na mnaishia kuishi kama chawa kwenye koti.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 23, 2012

    No wonder wanaigeria a.k.a wapopo wanawafukuza mbaya mijianamume ya kiafrika...mmezoea mfumo dume hata mkienda western countries mnataka m behave kama maporini mlikotoka

    Ona comments zenu hamna hata mmoja anayetumia akili kuwa sasa ni karne ya 21 na hakuna cha hii kazi ya mwanamke na hii ya mwanaume. Mtajibeba....

    Wanaigeria wako juu...mchezo wanaujua plus care. I LOVE WAPOPO

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 23, 2012

    Dada uliyesema kwamba wanaijeria mchezo wanaujua, bila shaka utakuwa umejaribu mataifa mengi sana mpaka kufukia conclusion yako.

    Wanaijeria? Caring? kukuachia credit card yake ndiyo caring? Nimewahi kuishi Scotland na nilikuwa na demu wa kinyarwanda. Mnyarwanda huyo huyo alikuwa na bwana wa ki-nigeria at the same time. Alikuwa akiwasifia sana kwamba wanajua caring, na alikwa anaachiwa credit card akae nayo. Wakati huo huo ananipa mambo mimi m-bongo na tukienda Nandos kula kuku wa kuchoma ilikuwa inachanjwa credit card ya m-nigeria.

    Swala la kuujua mchezo ni swala binafsi na halitegemei utaifa.

    ReplyDelete
  29. Tanzanian WomanJuly 23, 2012

    Yaani annon 12:00 umeniacha hoi wape vidonge vyao..
    nakwambia wanaume wa kibongo hawako romantic kabisa, hata wakaishi wapi..hapo ulikute limeoa mtasha mpaka mbwa atawapeleka for a walk, sasa aoe mtanzania mwenzio anajiona kidumee..my foot!!
    Wanawake wanabadilika na maisha ndiyo yanatubadilisha..

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 23, 2012

    oeni wa zanzibari,mtafaidi,hakuna hayo kabisa.wengi wao ni heshima kwa waume zao

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 23, 2012

    lazima tuwe kichwa ngumu, uzuri huku majuu sheria inamlinda mwanamke sanaaa. kwa hiyo ule ubabe wenu wa kibongo huku lazima mfyate! tena mie hubby wangu tuna zamu hadi ya kuosha choo na bafu chezea majuu? na anajua kumenya hadi ndizi na kitanda tunatandika kwa zamu. yani nyumba yetu ni safiiiiii. kama mkate wa mezani kila mtu analeta so hakuna ubabe alaaa. mlizoea sana eeh ? na anajua hadi kubadili mtoto diaper na kumpa maziwa. he he hee kwani siye tumekuwa robot zenu? binadamu wote ni sawa, mtajibeba majuu huku wallah, na ukileta chama cha upinzani kama david v anavyodai, hata mie na uwezo wa kuleta vyama vya upinzani chezea kidumu weye? na kweli tangu nije majuu nimekuwa na kibri si mchezo hii si bongo bwana huku haki sawa kwa wote!

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 23, 2012

    Pole wewe apo juu unaependa wapopo waulize majilani walivyo alibiwa naao mapopo sasa wamebaki kujitongozesha kwa vibabu vya kizungu ili wasiludishwe nyumbani kwakukosa kibali wakikuona umetulia na mumeo wana muiliza mkeo mgeni akiwajibu apana utawasikia basi usikubali atoke pekeyake kuja mjini kwanii kuna mapopo wahalibifu awashindwi kukutongoza ata wakuijua unamume unafikili ao ndio watulia wanazichanga kisha wanahalibu wanatimua jiazali ipo siku utawajua vizuri

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 23, 2012

    Hahahaha,

    Bossi umeshauvaa mkenge!

    Suluhisho la tatizo lako rudi Tanzania hadi Kijijini kwako ukaoe!

    Huyo aliyeko Majuu si ndio kageuka Mume kwako?

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 23, 2012

    No Woman no Cry!!!

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 23, 2012

    ha ha ha !!! mkubwa uliyependa sana coments zangu na mpaka unanialika tukapate Lunch au dinner, Nakushukuru sana, ila tu niko mbali kidogo ila nitafute. Lakini umeziona comments nyingi za hao wanawake wa Kibongo ???? yaani inatisha !!! hawafai hata kidogo na sasa ndo wamejianika kabisaaa wazi peupe-wewe rudia kusoma maneno yao ndipo utakapofahamu zaidi kwamba huyo aliyoleta hii mada yaani mengi kaficha . Hawa dada wa kibongo ni kufuru,bora uoe nyani mutaelewana, kingine , eti wanajigamba wako majuu !!!! sinilitaja lakini kwamba hawa ni malimbukeni wa kutupwa ?? sasa umeamini !! Achaneni nao, save your money and time. KUNYETO NI BURE. Hela yako yooote unayoitupa na kunyanyaswa na huyo malaya, iweke kwenye miradi yako bongo, kesho keshokutwa ,itakufaa-halafu wengine wanajidai kuandika kingereza humu hao kina dada ,ovyoooo !! darasa la 7 kaona mwezi , eti yuko majuu. mmoja nilikutana naye uwanja wa ndege Holland, kaniuliza unatokea wapi nikamwambia Mwanza, basi kaleta zake za kuleta, me im from Boston, kizungu cha lasha lasha, nilipomuangushia !!! mwenyewe alirudi kwenye Kiswahili, Kisa aliniona nimevaa jeans imepauka kaniona kama mimi ni storoway vile. hawa wadudu( demu) wa kibongo-waacheni waolewe na mapopo maana wajinga wale nao wanataka wanawake wenye laiti cola. Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 23, 2012

    Ahaaa walahi tena, napenda hii mada. Sasa wacha nitoe ushuhuda. E bwana tatiz kubwa hapa ni kuiga utamaduni. Mi niliona familia ya kibongo hapa ughaibuni basi kila kitu ni kama wazungu baba anafua anapika anabadili mtoto nepi nk. Lakini nilipoongea na mama anasema mume wake ni "PEPO" nilipoouliza anasema kazi yake ni kulalamika tuu kwa yale ananyoyafanya japo hajalazimishwa. Kingine alichonieleza ni kwamba mume ana dharau. Mama alikuwa anakusanya vijisent pengine zaidi ya baba. Sasa ni kosa hapo. Mke alikuwa machachari kwa mambo ya academia lakini jamaa ni mvivu fulani mwenye misimamo ya uswaaz ambayo hawezi hata kumaintain.
    Yaani suala zima ni mawasiliano na mipango katika ndoa. Kama watu hawapangi namna wanavyotaka maisha yao yawe na kuendelea kukumbushana ahadi zao za maisha basi. Ndio majuto yasiyoisha.

    Safari ni ndefu ila sasa mabadiliko si kama zamani mwanamke akiwa chombo. Sasa chombo kimekuwa binadamu. Wanaume amlijue hilo. Heshimuni wake zenu ongeeni na wake zenu kwa upendo yale manayoyataka. Acheni hasira na dharau. Mnaweza kufdanya hivi kama mtarudi vijijni na kuanza maisha huko ila katita mazingira ya usasa msitegemee.
    Tatizo kubwa wanaume wengi wamekulia vijijini na wameona baba zao walivyoishi na mama zao na wanategemea hayo kutoka kwa wake zao na hii haitawekana maana hiki ni kizazi kipya.
    Kuweni macho ndugu zangu. Epukeni lawama, zaidi mtafakari kwa utulivu amani na upendo juu ya maisha ya ndoa zenu.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 23, 2012

    Unapotaka kuoa inabidi uwe makini. sasa hivi 50% ya wasichana wa kibongo wanajiuza. So labda uliangukia mmoja ya wanaojiuza. Sorry for that.

    ReplyDelete
  38. AnonymousJuly 23, 2012

    Kuna mtu yoyote ambaye anamjua msichana angalau mmoja tuu wa kibongo aliyeolewa na mzungu au mpopo na akawa aendelei kutoka na m-bongo?
    Nawajua wasichana wengi tuu ambao waume zao ni wazungu, wapopo na wazaire. Na kila mmoja wao ana bwana wa kibongo nje.

    ReplyDelete
  39. AnonymousJuly 23, 2012

    Zebedayo msema kweli nimekusikia tena, seriously nimependa saaana comments zako. Kwa ufupi nilicheka mpaka nikaamua kuzima computer.

    Kwanini? kwasababu unaongea ukweli mtupu nimeona exactly unachosema hapa states watu wanaoa dada zetu wakifikiri mambo yatakuwa poa wataelewana. Ohh huyu mchaga mwenzangu, niambie kasheshe yake baada ya siku mbili tatu??

    Ohh mbona sisi hatununui Hammer kama Hamis, ohh mbona sisi tunakaa apartment na kina George wanakaa nyumba kubwa. Ukimwambia hujui majirani zako wanafanya nini, anasema fanya wanachofanya wao.. je kama wanajiuza usiku??

    Ulimbukeni, tamaa, na kutojua kumaharibu mabinti etu wazuri

    ReplyDelete
  40. AnonymousJuly 23, 2012

    WANAUME WABONGO MNATAKA KUNYENYEKEWA ULAYA? POLE SANA. AMESEMA DADA MMOJA HAPO JUU HUKU NI 50 PASENTI, TUPIKE PAMOJA, TUSAIDIANE. MIMI MWENZANGU MZUNGU ANAPIKA, ANALEA MTOTO, NA MIMI NAPATA DAY OFF YA KUPUMZIKA NIENDE KURELAX.INGEKUWA NI MWANAUME WA KIBONGO MTOTO ANGEKUWA MIKONONI MWA MAMA 24/7. WABONGO SIWATAKI NG'O KWA RAHA ZANGU.

    ReplyDelete
  41. AnonymousJuly 23, 2012

    Wewe dada wa 50 pasenti; anony wa Mon Jul 23, 08:19:00 PM 2012.

    Huyo mzungu wako mwezini pia mwaingia kwa zamu 50 pasenti; mwezi huu wewe mwezi ujao yeye; na mimba pia mwashika kwa zamu? mtoto wa kwanza yeye mtoto wa pili wewe?

    Hayo mambo mawili tuu yanatosha kuwafahamisheni kwamba hiyo 50 pasenti yenu itaendelea kubakia kuwa fantasy tuu.
    Kamwe hatutavuja wala kushika mimba.

    ReplyDelete
  42. AnonymousJuly 23, 2012

    Mtakuwa mnapiga wake za wadhungu nyie...mna uwezo wa kupiga wake za wapopo...stimu zenu zenyewe mpaka mvuuuute kwa kula pweza. Na Mungu kama alijua mgekuwa rijali kama wapopo tusingekunywa maji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...