Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi WILLIAM MHANDO (pichani)  ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa dhidi ya Menejimenti ya TANESCO.
Taarifa hiyo imetolewa na mwenyekiti wa bodi hiyo Jenerali Mstaafu ROBERT MBOMA ambapo katika taarifa yake amesema maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha dharura kilichofanyika jana kujadili masuala mbalimbali ikiwemo tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.
Taarifa zinasema katika kikao hicho, Bodi iliona tuhuma hizo ni nzito hivyo ni vyema zikafanyiwa uchunguzi huru na wa kina mara moja.
Jenerali MBOMA katika taarifa hiyo amesema uchunguzi huo utaanza mara moja kwa kutumia mchunguzi huru.
Aidha Bodi hiyo, leo imefanya kikao kingine cha dharura ambapo imeamua kuwasimamisha kazi mara moja wafanyakazi wengine wakiwemo naibu mkurugenzi mtendaji, huduma za Shirika Ndugu ROBERT SHEMHILU, afisa mkuu wa fedha Ndugu LUSEKELO KASANGA na meneja mwandamizi, manunuzi Ndugu HARUN MATAMBO.
Jenerali MBOMA amesema kufuatia hatua hizo zilizochukuliwa, Bodi imechukua hatua stahiki ili kuhakikisha shughuli za kiutendaji na uendeshaj wa TANESCO zinaendelea kama kawaida.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2012

    Duh Shuhuli pevu. Pole Br.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2012

    Why it took so long? This guy should have been out of that position long time ago.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2012

    mmmmmmmhhhh!!!!!!!!!! haya we, vyeo vya kupewa ndo taabu yake. bora angekuwa desk officer.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 14, 2012

    Nasikitika kwa yaliomkuta CEO, lakini pia natoa pongezi kwa bodi kwani inaonyesha inafanya kazi kwa mujibu wa sheria. Natusubiri kuona haki inatendeka kwa Bw Mhando kwa mujibu wa sheria za nchi. Bodi nyingine zifanye kazi kama hii ya TANESCO kwa umakini. Bodi ya DAWASCO mpo?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2012

    Jamaa lazima atakuwa alikuwa Threats tu kwa wanasiasa, Serikali yetu haiko serious kiasi hiko

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2012

    SIKU ZOTE MASHIRIKA UMMA YAMEKUWA YANAFANYIWA UBADHIRIFU MKUBWA WA MALI NA MADARAKA KWA FAIDA ZA WATU WACHACHE NA SI TAIFA,JE BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA NANYI MNASUBIRI NINI? AU NDIYO NANYI MNAPINGA KAULI YA MH J.KIKWETE YA UWAJIBIKAJI KWA KUMLINDA POSTAMASTA MKUU? NI SISI WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA POSTA WENYE UCHUNGU

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2012

    DEO KHAMIS MNDEME POSTAMASTA MKUU NA DR YAMUNGU KAYANDABILA M/KITI WA BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA MPOOOO!!! MWENZENU AKINYOLEWA NYINYI TIENI MAJI HAYA HAYANA MMOJA! YOU JUST GET PREPARED! WADAU WA GPO.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2012

    mmmmmh umeme utapungua bei? wizi mtupu!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2012

    Bajeti ya Nishati na madini bado. Huenda mambo yameshakuwa mabaya na taarifa zimevuja, hivyo wanahofia hoja isije ikatolewa na wapinzani ikaleta noma.

    Unakumbuka hoja ya uteuzi wa majaji na wakuu wa wilaya kilichotokea kule mjengoni?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 14, 2012

    BLOG YA JAMII naomba mpost na hizi kero.
    1>TRA nayo imulikwe.Jana tarehe 13 July nilikutana na kizaazaa cha aina yake Uwanja wa ndege Dar(JNIA) wakati nasafiri kwenda majuu saa 11 alfajiri.Kuna viwango vipya vya kodi uwanja wa ndege.Wale tuliokuwa tumekata tiketi zetu kabla ya viwango hivi havijapanda tulikuwa tunalipishwa dola Kumi na wale wahudumu wa pale kwenye dawati la tiketi(eti amri imetoka juu-juu kwa nani??),hakuna risti,hakuna ofisa hata mmoja wa TRA.Sina uhakika kama fedha hizi zilifika huko kunakotakiwa.

    2>:Mamlaka ya Uwanja wa ndege Dar, JNIA:Maneno yanayoonyesha jina la uwanja wakati wa giza hayasomeki..zinaonekana herufi 2 au 3 tu J......N.....bulb zingine zote zimeungua.Zile hela za parking ya magari zinafanya nini??

    David V

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 14, 2012

    This shows progress in terms of accountability! Hakuna cha pole hapa! Yaani ukisema pole ni kama unamwonea huruma mwenzako. Sasa kama mwizi anaweza kuwa mwenzako sijui tena hapa.
    Ikiwa hivi katika idara zote tanzania itaendelea. Kujuana ndio tatizo. It will take time, but we will be there Inshallah!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 14, 2012

    Safi sana!
    Jamani mimi ningeomba pia shirika la Posta lifanyiwe uchunguzi, coz limejaa mno madudu. Tatizo watu wamezidi mno kulindana!
    Mizigo ya watu inaibiwa kila siku. Mzigo unau-track online unaonyesha kabisa umekuwa delivered Tanzania lakini ukienda kufwatilia Posta wanakwambia bado.
    Nina package mbili zimtumwa tangu mwezi wa tano, nimejaribu kufwatilia bila mafanikio. Kila nikienda napigwa danadana. Hata ukifungua claim hamna kinachofanyika. Wananchi wamechoka na huduma mbovu.
    Naomba Postmaster general afanyie uchunguzi swala hili.
    Kwa kweli inauma sana kuona upotevu wa mizigo Kilauea siku!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 15, 2012

    Ningeomba pia na Swissport ichunguzwe. Kuna uwizi mkubwa sana wa mizigo pale airport.
    Naona Posta wanashirikiana na wafanyakazi wa swissport kuiba vifurushi vinavyotumwa kutoka nje ya nchi.
    Ukiuliza unajibiwa kwa hauna "insurance" yani bima.
    Kwa hiyo mali iliyokatiwa bima ni haki kuibiwa au kupotea??
    Naomba uchunguzi ufanyike haraka sana. Wananchi tumechoka kuumizwa!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 15, 2012

    Ningeomba pia na Swissport ichunguzwe. Kuna uwizi mkubwa sana wa mizigo pale airport.
    Naona Posta wanashirikiana na wafanyakazi wa swissport kuiba vifurushi vinavyotumwa kutoka nje ya nchi.
    Ukiuliza unajibiwa kwa hauna "insurance" yani bima.
    Kwa hiyo mali iliyokatiwa bima ni haki kuibiwa au kupotea??
    Naomba uchunguzi ufanyike haraka sana. Wananchi tumechoka kuumizwa!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 15, 2012

    Huu uwajibikaji unatakiwa kuwa endelevu na si visasi visivyo na msingi.Nahisi kuna moto bado unakuja kwani JK wakati anabadilisha mawaziri aliapa kuwa watendaji waliochini ya mawaziri walowajibika watakipata.Ila sasa tunasahau kuwa hili swala la uwajibikaji inabidi liwe utamaduni ili tusogee.kwani siku zote hizo bodi hazikuwepo?nimesoma comment moja ya mzungu nikahurumia TZ.yeye alisema baada ya wakoloni kuondoka viongozi wa afrika waliwekeza kwenye Rushwa,ufisadi nk so akimaanisha kuwa kuwepo ukoloni na kutokuwepo hakujaleta unafuu kwa mwafrika wa kawaida.Nikifikiria nchi yangu TZ nashindwa kuamua ukweli ni upi.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 15, 2012

    CHANGA LA JICHO LINGINE HILOOOOOOOOOOOOOO.......MIJIZI INAPOZIDIANA...TATIZO NI KWAMBA KWA KUENDELEA KUFANYA VILE TUFANYAVYO KILA SIKU...NAAM TUTAENDELEA KUPATA MATOKEO YALE YALE...ETHICS,ETHICS...+ CORRUPTION

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 15, 2012

    Swaala tu la ajira kama lilivyo linanitia kichefuchefu, kasababu kama hizi, sasa mheshimiwa mzima anavuliwa nguo hadharani namna hii ndo nini? Tatizo tu hatuna mtaji namna nyingine ofisi zao tungewaachia tuone wangemfukuza nani au kumnyanyasa kazini.
    Yaani mtu kila kukicha una wasiwasi sijui leo kazi ipo au ndo nimeshafukuzwa, huna amani moyo, kwanini mambo haya yamekaa hivi?

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 15, 2012

    Nami nilituma kitabu toka mwaka juzi hakijafika.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 15, 2012

    Heheheh hii bodi kweli kichekesho!!! Jamaa week iliyopita tuu walikuwa wanafanya msako kwa wafanyabiashara wakubwa wanaohujumu nchi kwa kuiba umeme sasa naona huyu jamaa mhando kawaingilia washikaji anga zao!!! Kweli changalamacho!!! Siku zote hawajatoa maamuzi leo tuu ghafla duuh!!!

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 15, 2012

    NIMESOMA MCHANGIAJI MMOJA AKISHUTUMU SHIRIKA LA POSTA,IMENIGUSA KIDOGO KWA KUWA KATIKA MASHIRIKA YALIYOPO TANZANIA YA UMMA BASI POSTA UTENDAJI WAKE UPO WA KIZAMANI SANA YAANI UKISIKIA WAO WAPO BADO NYUMA SANA KIZAMANI KWELI KWELI,WAO NI ANALOG KABISA KABISA,WANABODI YA TENDA NI RUSHWA TUPU,HAIFUATI SHERIA ZA PPRA
    KABISA

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 15, 2012

    Mimi nimetumiwa laptop na iPad tangu mwezi May, zinaonyesha zimefika Dar es salaam, lakini jamaa wanipiga calendar.
    Inasikitisha sana!

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 15, 2012

    Hapa hatuwezi kutoa hukumu, tusubiri tuone. Hivi uchunguzi wa Jairo uliotumia shiling milioni 260 umeishia wapi? taarifa ya uchunguzi huo imepelekwa wapi? Kesi ya Mataka wa ATCL imeishia wapi? Mashirika yetu yamulikwe hasa kwenye mifuko ya hifadhi ya Jamii na Regulatory Bodies kuna wizi mkubwa sana.

    Kwa hili la Mhandisi Mhando kidogo nachelea kusema. Juzi ameanzisha operation ya kukamata WEZI WAKUBWA wa umeme ambao wengi ni wenye viwanda, mahoteli na nyumba za wageni. Inawezekana hili nalo limegusa UNTACHABLEZ.

    TANESCO watamkumbuka sana DR. Rashid na Mkurugenzi wa Fedha Bw. Ngilime (sikumbuki jina vizuri) hawa ndio watu wangelifikisha hili shirika mahali lilipo takiwa kuwa. Kwakuwa TANESCO ni biashara ya Watu:-
    1. Wazalishaji umeme wa zarura
    2. Wauzaji wa mafuta ya kufulia umeme
    3. wanasheria wanaosimamia kesi za Tanesco kama Mhe. Mhand
    4. Waingizaji wa majenerator
    5. Na wazabuni mbalimbali
    Hawa wamefanya TANESCO ishindwe kujiendesha professionaly ikichangiwa na kuingiliwa sana na wanasisa.

    Ofcoz uongozi wa TANESCO unaudhaifu mkubwa hasa japokuwa wamebadilisha muundo na kuongeza ukubwa wa uongozi kitu ambacho kimeongeza gharama za uendeshaji wa SHirika. WaTANESCO wenyewe wanasema ukabila nao upo juu kwani Shemuhilu nae ananguvu sana kwani amekuwa analindwa na kaka yake Mhando.


    Ila kwa hili la TANESCO la sasa nadhani ni safisha njia ili bajeti iweze kupita! Katibu Mkuu wa Nishati na Waziri wake ni people of "Actions" naamini hivyo ila waangalie wasijetake actions kwenye maneno ya kusikia bila kujiridhisha maana kwa nafasi yao wanaweza kuumiza mtu, familia yake na wategemezi wao bila kuwa na hatia kwasababu ya kusikiliza maneno na kufanya maamuzi ya haraka. ni witu wangu kuwa pamoja na yote baada ya uchunguzi wa mchunguzi Huru basi HAKI ITENDEKE. Pia vyombo husika kama Mkaguzi Mkuu, Polisi na TAKUKURU nao wafanye kazi yao ili haki itendeke.


    Kwenye mijadala (Klabuni) nimesikia kuna mgongano wa kimaslahi kati ya watu wa Wizara na TANESCO. Tafadhali kila mmoja apate nafasi ya kujieleza.

    TANESCO imekuwa mchwa wa kutafuna keki ya TAIFA IPTL, DOWANS, AGREKKO etc. Uchunnguzi huo unaokusudiwa kufanyika uangalie kwa kipindi chote cha miaka mitano hasa sehemu ya mikataba ya kukodisha mitambo, wakandarasi wa ujenzio wa mitambo mbalimbali na wazabuni wa mita, nguzo, matairi ya magari n.k huko nako sio kwema.

    Tatizo kubwa nalo ona kwa mashirika kama haya ni kuwa viongozi wa haya mashirika wananguvu kuliko viongozi wa wizara zinazowasimami. Mf. Mshahara wa Mhando sio chini ya shilingi milioni kumi lakini Katibu Mkuu wa Nishati Mshahara wake ni Milioni moja na nusu. Haya ni mambo ya kuangalia. kuna watendaji wa mashirika wanalipwa hadi shlingi milioni 20.

    Wito kwa Bodi za Mashirika yetu huko nyumbani! Management iwajibishwe pale inapokosea. Hongera kwa Bodi ya TANESCO na nyingine zifuate mfano.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 15, 2012

    Go Mboma go. Nadhani bodi zote zingeongozwa na Wajeshi... wana nidhamu na ni waadilifu sana wanajeshi compared na hao wanasiasa ambao wanaongoza bodi kinjaa njaa. Wakioewa sitting allowance na allowance ambazo ni kubwa kuliko sheria inavyosema basi wanafunga midomo. Big up General!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 15, 2012

    naomba pia bodi ya mamlaka ya maji arusha nayo iwajibike ama imwajibishe mkurugenzi, kwanza upotevu wa maji umekisiri na upatikanaji wa maji ni afifu, walijitokeza wasema kweli juu ya upotevu wa maji lakini akawekwa pembeni eti ameidanganya bodi sasa ukweli unaonekana wazi je aibu ya nani, pili meneja wa fedha amechaguliwa pasipo kufuata taratibu na sheria za tangazo lenyewe kwanza inakuwaje meneja fedha anaajiriwa pasipokuwa na cpa na bodi mkampitisha, angalieni pia utendaji wa mkurugenzi mwenyewe ni afifu na wenye maamuzi yasiyofuata taratibu tunaomba pccb arusha mchunguzi hili, mfanyaazi auwsa

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 16, 2012

    Michuzi ndo umeamua kubana comment yangu ya swissport JNIA kuhusu Martha, sawa. nitatafuta blog isiyokuwa na watu waoga kama wewe nitatoa kilio changu huko. Kama ni dada yako useme. Kumbuka hii ndo sehemu ya kuelimishana hasa ukizingatia watu wengi wanaibiwa pale Airport kiubabeubabe wakati wanataka kusafiri.

    Hata hivyo nilishamripoti vyombo vya usalama na kuna siku zake hamsini zitatimia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...