Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda wakipokea haeshima za marais muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Rwanda leo asubuhi.
 Rais dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda wakikagua gwaride la  heshima katika uwanja wa ndege wa Kigali.
 Rais Paul Kagame wa Rwanda akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete katika uwanja wa michezo wa Amahoro mjini Kigali Rwanda kwaajili ya sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Rwanda.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiteta jambo wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Rwanda zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Amahoro jijini Kigali leo asubuhi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2012

    Mr.Paul ana kazi ya ziada na tuhuma za kuwasaidia Waasi Mashariki ya Kongo.

    Ni wazi hili suala limekaa vibaya pande zote, ukiweli ni kuwa pana makundi mawili ya Waasi kama hivi:

    1.Kiundi la FDLR:
    Linaundwa na Wahutu wengi wao ndio walioshiriki mauaji ya Kimbari 1994 wao azma yao ni kuiangusha Serikali Kigali na Kuwaangamiza Watutsi wote, huku wakitetea maslahi yao dhidi ya Wababe wa Jamii zingine wateka ardhi ktk Mashariki ya Kongo.

    2.M-23 /Zamani CNDL
    Kundi hili linaundwa na Watutsi waliopo Mashariki ya Kongo, wanayahami maeneo na maslahi ya Watutsi waliopo huko Mashariki a Kongo, linakabiliana na Makundi mengine ya Wababe pamoja na hilo hapo juu dhidi yao FDLR,
    Hivyo wao Rwanda kwa Maslahi inabidi wawaache hao M-23 kwa vile wanakabiliana na Maadui zao wakubwa na kupelekea kuonekana kuwa kama wanawasaidia.

    Jambo la kushangaza ni kuwa UN repoti yao inashutumu upande mmoja tu wa Serikali ya Rwanda na M-23 bila kuongelea juu ya hao FDLR ambao pia ni Waasi wanao hatarisha mustakabali wa Rwanda wakitokea Mashariki ya Kongo.

    Pia inasemekana kuwa kama M-23 wanasaidiwa na Rwanda pia FDLR wanasaidiwa na DRC lakini UN hawalioni hili.

    Bajeti kubwa ya US$ 1.2 Bilioni(Nusu ya Bajeti ya Serikali ya Rwanda kwa maka mmoja) imeelekezwa kwa Majeshi ya UN ya MONUSCO yanayolinda Amani Mashariki ya Kongo, sasa kwa nini haya Majeshi ya UN kwa Bajeti hiyo yasiwadhibiti Waasi wa Makundi haya mawili M-23 na FDLR na badala yake ishutumiwe Serikali ya Rwanda?

    Kwa kweli Mr.Paul vita imemkalia vibaya 'ukubwa ni jiwe' na hakuna jinsi inabidi azibebe tuhuma na lawama hizi.

    Mungu amsaidie!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...