THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

ujenzi wa njia mbili barabara ya bagamoyo road unaendelea kwa kasi

 Hapa karibu na njia panda ya Kunduchi. Baada ya muda wadau waliondoka Dar muda mrefu uliopita  wakija nyumbani watakuta mabadiliko makubwa kwenye barabara hii na nyingine kibao ambazo foleni zake ni za kufa mtu kutokana na ufinyu wa barabara
 Maeneo ya Kunduchi karibu na pale wanapochimbaga kokoto za kujengea
 Maeneo ya Tegeta njia panda ya Wazo Hill
Daraja karibu na kufika Tegeta kituoni


Kuna Maoni 7 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Barabara ya Bagamoyo Road!! Duh

 2. Anonymous Anasema:

  Anachonifurahisha mkandalasi huyu ni kutambua na kutunza miti. Ameweza kuacha miti mingi barabarani iendelee na maisha yake hasa eneo la Africana hadi Mbuyuni.
  Hongera sana kwa jambo hilo

 3. HK Anasema:

  Bagamoyo Road (in English) au Barabara ya Bagamoyo (kwa lugha yetu ya Taifa), vyovyote vile ni fasaha kabisa na inajitosheleza. Haya mazowea ya kusema au kuandika "Barabara ya Bagamoyo ROAD" ndio hizo lugha gongana na hatimae zinakuwa mazowea yetu. Kila la kheri katika shughuli nzima za ujenzi wa barabara hiyo.

 4. Anonymous Anasema:

  Michu,good job.Please zidi kutuletea taswira za barabara,hii inakoga mioyo ya watu sana hasa hasa waliolowea nchi za mbali na kwa miaka mingi hawajarudi bongo . pia nachukua nafasi hii kukuomba unitangazie kwa wanablog kwamba ,nina mashine za kuprinti picha kwenye vikombe na (mag) zake (vikombe) vyake kama elfu moja hivi,naomba mjasiliamali aje tuonane nimuuzie. email yangu ni jacobmayillah@hotmail.ca.

 5. Anonymous Anasema:

  michuzi nakuomba sana kaka yangu utuwekee kituo cha mabasi cha hiyo barabara alafu utuwekee na kituo cha moroko kwa pamoja halafu uangalie vina fanana?mimi sijapenda wameweka kituo vibaya sasa magari yata simama vipi kipaa chenyewe kifupi basi litakwangua kianguke,nafasi ndogo halafu hakuna mchepuko hiyo ni hiway.unaweza simama unapakia abiria unagongwa kwa nyuma sababu haijulikani umesimama au unakwenda ni mbaya sana.nenda kaone mwenyewe utaelewa ninachokueleza.utatusaidia sana labda kwa namna yeyote mdau wa kunduchi.

 6. Anonymous Anasema:

  Barabara ya bagamoyo road! badilisha hiyo statement please!

 7. Anonymous Anasema:

  Ni vizuri sana kuongeza road, Je usalama wa wananchi utaendana na barabara mpya, hivi sasa hatuna barabara lakini tunachinjana kwa ajari ,je zikamilika itakuaje?naomba serikali ilitazame hilipia