Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Charles Singili akizungumza na wateja wa benki hiyo wakati hafla ya kufuturisha wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa msimu wa Ramadan unaoendelea
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Charles Singili (kulia) akifurahia jambo na mmoja wateja wa benk hiyo wakati wa hafla ya kufuturisha wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha na mpicha wetu
Akina mama wakifuturu katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Azania na kuwakutanisha wateja wa benki hiyo.
 Badhi ya wafanyakazi wa Benki ya Azania wakifuturu katika hafla hiyo.
Badhi ya wateja na Benk ya Azania wakipakua chakula wakati wa hafla ya kufuturisha wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa msimu wa Ramadan unaoendelea
========  =======  ======
BENKI YA AZANIA YAFUTURISHA WATEJA WAKE

Benki ya Azania ilianda futari kwa ajili ya wateja wake kwa lengo la kuwakutanisha katika msimu huu wa Ramadan.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Charles Singili alisema benki yake inathamini mchango wa wateja katika ukuaji wa benki hiyo.
Singili alisema benki yake ipo katika mkakati ya kutanua huduma zake katika ukanda wa ziwa kwa kufungua tawi jipya mkoani Geita kabla ya mwisho wa mweshi ujao na tawi jingine Mtwara kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Awali Bw. Twalib Ahmed Lubangula akizungumza kwa niaba ya wateja wa benki ya Azania alielezea imani waliyonayo na benki hiyo hasa katika upatikanaji wa huduma bila usumbufu na kuongeza kuwa wataendelea kuipa ushirikiano katika shughuli zake mbalimbali.

 “Tunafurahia huduma nzuri za kibenki zinazotolewa na benki ya Azania. Ukweli ni kwamba huduma zinapatikana kirahisi ukilinganisha na benki nyingine. Benki hii tulianza nayo ikiwa na tawi moja tu lakini imeweza kufungua matawi mengine mapya ndani ya kipindi kifupi. Tunajivunia kuwa injini ya maendeleo ya benki hii,” aliongeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongereni sana uongozi wa bank kwa kuandaa kitu kama hiki kama shukrani kwa wateja wa bank

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...