Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa sera ya Kilimo na Chakula toka kwa Bw. Ajay VAshee, Makamu Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali inayohusika na sera za kilimo na chakula na Maliasili n ijulikanayo kama Food, Agriculture and Natural Resources Policy (FANRPAN) katika hoteli ya White Sands jana Septemba 5, 2012. Anayeshuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa FANRPAN) Dkt Lindiwe Sibanda. Tuzo hiyo, ambayo hutolewa kwa kiongozi aliyefanya juhudi kuhakikisha kuwepo kwa sera bora za kilimo na chakula nchini kwake, ilichukuliwa na Malkia Ntombi Indlovukazi wa Swaziland mwaka jana, wakati Rais Hifikepunye Pohamba alitunukiwa mwaka 2010, Rais Armando Emilio Gwebuza mwaka 2009 na Rais wa Malawi, Hayati Bingu Wa Mutharika, aliipokea mwaka 2008.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia baadhi ya ng'ombe anaowafuga kwa kufuata njia za kisasa kwenye shamba lake kijijini kwake Msoga, Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, leo Septemba 6, 2012.PICHA NA IKULU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa 1. WTF,,,Hongera Mhe Raisi kwa kupewa tuzo kweli unazo nyingi.... kama nakuona vile,,,

  hahahah @ J.Kikwete mpaka umalize uongozi utakua nazo kama tuzo 10 kila mwaka unapewa moja ila ni wakati sasa wa watanzania kumtunikia raisi wenu tuzo pia

  ReplyDelete
 2. Safi sana rais wetu ila sasa watanzania tumtunukie rais wetu tuzo kwa vitendo kwa kulima kilimo cha kisasa zaidi kwani kwa kufanya hivyo tutapiga hatua kubwa ktk historia ya nchi yetu

  ReplyDelete
 3. anaonesha mfano na anajitayarisha kustaafu. Ila Kijiji cha Msoga kina maendeleo ya aina, nyie waandishi wa habari ndio mnatakiwa nfuatilie kama analingana na wenzake pale kiijijini.

  ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...