Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani,Afande Mohamed Mpinga akipokea msaada wa fulana 1000 za kuhamasisha wiki ya nenda kwa usalama barabarani na vipeperushi 500 kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Mampuni ya Bia ya Serengeti (SBL),Teddy Mpunda katika makabidhiano yaliyofanyika leo kwenye makao makuu ya Trafic jijini Dar es salaam.Kushoto ni Meneja wa Mipango Endelevu na Uwajibikaji wa Kampuni ya Serengeti,Nandi Mwiyombela.Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 17.5 na kampuni hiyo imesema inaangalia uwezekano wa kuchapisha vipeperushi vingine kwa ajili ya mkoa wa Dar es salaam ambapo hivi vya awali vitapelekwa mikoani.
. 
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani,Afande Mohamed Mpinga akizungumza katika makabidhiano hayo wakati alipokuwa akitoa shukurani zake kwa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL).wanaofuatia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL),Teddy Mpunda na Meneja wa Mipango Endelevu na Uwajibikaji kampuni ya Serengeti,Nandi Mwiyombela.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL),Teddy Mpunda akizungumza katika makabidhiano hayo.kushoto ni Meneja wa Mipango Endelevu na Uwajibikaji Kampuni ya Serengeti,Nandi Mwiyombela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...