Ndugu zangu, 
 

Ahsanteni kwa mitazamo yenu. Katika hili yawezekana tukawa na mitazamo tofauti, ni hali ya kibinadamu. Kwangu mimi, kwa wanahabari huu si wakati wa kutangaza mgomo wa kuripoti habari za kipolisi, kinyume chake, ni wakati wa kushambulia kwa pamoja kwa kuwakabili polisi na wahusika wengine kwa maswali yenye kuhitaji majibu.

Huu ni wakati wa jeshi la  wanahabari  kuishambualia polisi kama taasisi muhimu ya dola ili ipate majibu ya maswali ambayo jamii inataka majibu yake. Mbali ya  tukio la mauaji ya mwandishi mwenzetu Daud Mwangosi, hatuwezi kuacha kufanya kazi na polisi kupata majibu ya matukio mengine ya kihalifu yanayotokea katika jamii kwa vile tu tuna mgogoro na polisi. 


Naamini, tofauti na kugoma, kuna njia nyingine za kuishinikiza Serikali na hata taasisi ya polisi kuchukua hatua katika yanayotokea. Na moja ya njia hiyo ni kila linapotokea tukio, kwa  wanahabari kwa uwingi wetu,  ' kuvamia' ofisi za wenye kuhusika na kutoa majibu ya maswali ambayo jamii inataka majibu yake.
 

Msimamo wangu huu unaeleweka hata na baadhi ya viongozi wa juu wa Iringa Press Club ambao nina ushirikiano nao mzuri.  Na jema katika hili  ni kuwa,  ushauri wangu wa namna ya kwenda mbele umepokelewa vema na Makamu Mwenyekiti ( Francis Godwin) na Katibu  Mkuu wa IPC ( Frank Leonard) ambao kimsingi nimefanya mazungumzo nao  na  wanaufanyia kazi ushauri wangu.
 

Vinginevyo, naelewa hasira na jazba tuliyo nayo  wanahabari wengi kutokana na  kilichotokea. Hata hivyo, hata katika hali kama hii, tuwe na ujasiri wa kumeza vipande vya barafu. Tutangulize hekima na busara. Ndio, tutulie na kupanga mikakati ya pamoja itakayohakikisha jamii tunayoitumikia hainyimwi haki yake ya kimsingi ya kupata habari ikiwamo habari za kipolisi. Na hata katika hili, jamii ina mengi inayoyahoji kupitia wanahabari. Wenye kuhitajika kuhojiwa ndio hao tunaofikiria kuwagomea. Naam, tuna lazima ya kuwahoji wahusika. Ni kazi yetu.
 

Ndio, mikakati hiyo ituhakikishie wenye kuhusika na  kutoa majibu ya unyama uliomtokea mwanahabari mwenzetu hawapati muda wa kupumua. Hii ni pamoja na sisi tulio mstari wa mbele kuhakikisha kila kukicha wahusika wanatukuta nje ya  milango ya ofisi zao tukisubiri majibu ya maswali ambayo jamii inayauliza. 



Kwamba matukio kama ya mauaji ya Daud Mwangosi kamwe yasiwe ni ' Upepo tu unaopita'- Kwa wanahabari kugomea kuwakabili polisi  kwa maswali ni  namna moja au nyingine ya kutengeneza mazingira ya kuruhusu ' Upepo upite'.
 

Kufanya hivyo ni kulisaliti jukumu letu la msingi- Kuitumikia Jamii ya Watanzania.


Na Mpiganaji Maggid Mjengwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hivi polisi ikiitisha press conf kuwataadhirisha na tukio la ughaidi mtasusia? Please! Ndiyo wanafanya makosa mengi lakini kuna mazuri pia. Kama polisi wamefanya makosa wapelekeni mahakamani kwani ugumu uko wapi? Naungana na mjengwa.

    ReplyDelete
  2. Ni rahisi kusema tugome au tusigome, very easy.. na kusema ukweli wa mazingira ya TZ inawezekana hiyo siraha waliyonayo pekee.

    Ukweli ni kwamba tatizo hili ni zito na gumu kuliko tunavyoliona, Mjengwa umekaa magharibi na unaelewa maana ya uhandishi wa habari ni nini?

    Kitendo cha kumuua, sio kumuumiza ila kumuua mwandishi wa habari makusudi mchana mwelee hakiwezi kuishia polisi bwana.

    Na mpaka leo nashangaa saana kuona vyombo vingi vya habari na watanzania walio wengi wameona ni sawa tu, ni "mtu mmoja amepoteza maisha tuendelee kama kawaida" guess what? nxt time watapigwa kumi, lets wake up this serious man

    ReplyDelete
  3. Poleni jamii ya waandishi.
    Pamoja na yaliyotokea waandishi sometimes mmejirahisisha mno na mnakwepaga hata kujitambulisha - kwanini msivaage vijambakoti vimiandikwa PRESS mjulikane - yawezekana hao afandez walitembeza kipondo bila kumjua vema. Tuamke tuwajibike.

    ReplyDelete
  4. Hata kama si mwandishi wa habari, police kazi yake ni kulinda raia. Si kupiga raia! Haijalishi wewe ni nani? Inakua rahisi kuongea kwa vile aliyeuawa si jamaa wala ndugu yako. Hebu imagine kama angekua ni baba yako, kaka ama mwanao. WaTanzania mmezoea kuburuzwa!!!

    ReplyDelete
  5. Sawa naungana na mjengwa kugoma si suluhisho la matatizo hayo.iburuzeni polisi mahakamani haki ikapatikane.
    Sasa huyo hapo anaye sapoti mgomo eti ambao hatu sapoti hatuna uchungu,mm naona yeye ndiyo hana uchungu maana adhari za migomo hazijui.

    ReplyDelete
  6. ...Watanzania ni kweli tumezoea kuburuzwa..fact..na mimi nadiriki kusema kuwa ni hawa hawa waandishi wa habari wanachanguia katika kuburuzwa kwetu. Naipa pole sana familia ya woote waliouwawa na polisi au kupata madhara kwa fujo za polisi.
    Waandishi wa habari hawaji katika press conference mpaka walipwe na mwitaji..

    mmatokeo yake hatupati habari za uchambuzi bali za kupaka mafuta hata penye ukurutu.
    waandishi mjue mnajishushia hadhi ninyi wenyewe.

    ReplyDelete
  7. Nianze kwa kusema MSINGI WA HAKI NI UADILIFU na uadilifu kwa ufupi maana yake ni kumpa kila anayestahiki haki yake apewe bila kujali ni nani kwako alimuradi hiyo ni haki yake basi apewe!!
    wanahabari poleni sana kwa msiba wa kusikitisha uliowapata na watanzania wote poleni kwa msiba huo wa kuhuzunisha ndani ya nchi inayosifiwa kila kukicha kwamba inautawala bora na unaofuata sheria!........wanahabari nadhani mumesahau msemo wa kiswahili usemao "YALIOMPATA KIBEKU NA UNGO YATAMFIKA" wanahabari mumekuwa munaripoti habari nyingi sana lakini mumekosa uadilifu katika fani yenu, mumekuwa mukiripoti habari kwa utashi zaidi aidha kwa utashi na maslahi ya wakuu wenu wa kazi au makundi ya jamii zenu husika kuliko maaadili ya kazi zenu ya uwazi,kuelimasha, haki,kufundisha,kuadabisha na kuburudisha bila kusahau kuonya mfano;walipouwawa waislamu pale mwembechaikwa kosa la polisi kuingia msikitini na kumkamata kiongozi wao nyie hamkuripoti kiusahihi bali kwa kejeli kwamba hao ni wahuni na hawakufuata sheria katika kudai madai yao ya kukamatwa kwa kiongozi wao "upepo ukapita" wakauwawa wananchi Pemba baada ya uchaguzi wa 1995 kwa kugomea matokeo ya uchaguzi kiongozi mmoja akasema hao ni wahuni kwa hiyo ilikuwa sawa kuuwawa,wanahabari hamkuliona hilo mkakaa kimya kwa kuwa hakukuwa na mwanahabari aliye jeruhiwa na wala hamkushurutisha kuanzishwa kwa tume ya uchunguzi kama ilivyokuwa mwembechai damu za watu zikatiwa mchanga yakapita tena haraka zaidi ya upepo,Aliuwawa Jenerali Amrani Kombe kwa risasi za kifuani ikasemwa alikuwa akikimbia!!!! hamkuhoja kivipi akimbile halafu apigwe risasi za kifuani muliona Dogo hamkutumia kalamu zenu kuhakikisha haki juu ya unyama ule unapatikana kwa kuwa hakuwa mwandishi mwenzenu!! nayo yakapita kama upepo!!wamepigwa na wengine kusadikika wapepoteza maisha katika vurugu zilizotokea Newala baada ya wakulima wa korosho kuamua kwenda KUDAI CHAO kilichotokana na jasho lao la ukulima wa korosho hamkuwasapoti badala yake walilaaniwa kwa madai hawakufuata taratibu!!? hakuna asiye jua kwamba nchi hii ina uhuru wa kuabudu kila mahali mpaka vyuoni na mashuleni waandishi mlikaaa kimya vijana wa kiislamu walipotimuliwa pale ndanda sekondari kwa kuomba tu shule iwapatie mahala pa kusalia na hawakufanya mtihani wa kidato cha sita na kuwafanya warudie mwaka!!!sasa katika hali kama hii nyie kama waandishi mumejiweka wapi katika kusimamia na kuona haki inatendeka kila kona? au haki ni kwa watu ambao mnamaslahi nao tu mwengine yeyote akidhurika alimuradi hakusu haikupasini kuisimamia haki yake? hivi karibuni kunahabari kuwa baadhi ya viongozi wao wamekamatwa kwa madai ya kukataa kuandikishwa sensa hali inajulikana kwamba si kosa mtu kukataa kuandikishwa kwa kauli za hao hao viongozi wa usalama wa raia sasa mbona waandishi hawa viongozi wanakamatwa kwa lipi hali ya kuwa imeshasemwa kuataa sensa si kosa alimuradi tu usimfanyie vurugu mwandishi wa sensa hiyo mbona hili hamlisemi au ndio halina maslahi na nyie........nini maana ya haki na uhuru wa kujieleza basi ikiwa mtu akisema no iwe kosa mpaka yes tu ndio awe kafanya vyema!!? mwengine kafungwa huko tanga miaka miwili kwa kosa la kukataa kuandikishwa sensa hali yakuwa shiria ina sema ukimzuia mwandishi wa sensa kwa vurugu adhabu haizidi miaezi sit!!!??? hapa hamjapaona???
    ndio maana waswahili wakasemaa " yaliompata kibeku(ungo mchakavu) na ungo yatamfika" usipomzuia mtu kudhulumu ipo siku atakudhulumu wewe na utakosa msaada wa jamii ya watu wanaokuzunguka.. wananchi kwa uwingi na mshikamano wao na waandishi kwa kutumia kalamu zao na vinywa vyao jambo kama hilo linakoma na haki inapatikana na watu wanawajibika lakini ilivyo sasa ni kama waandishi na wananchi wengine kuna mwanya unaoondosha mshikamano wa viungo hivi muhimu kwa mabadiliko ya hali za watu na ndio maana jambo hili la kuwaw kwa mwanahabari huyu ni kama msiba wa waandishi peke yao!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...