Mwanaharakati Novatus Mutoka kutoka Mkoani Dodoma akiongea na waandishi wa habari (hawapo picha) leo mkoani Dodoma wakati akitambulisha kitabu chake kinachoitwa "HARAKATI ZA DKT JAKAYA KIKWETE KATIKA KUMUENZI MWL JK NYERERE" ambapo pia alielezea lengo la yeye kuandika kitabu hiko mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani)
Mwanaharakati Novatus Mutoka akionyesha kitabu alichoandika yeye kinachoitwa "HARAKATI ZA DKT JAKAYA KIKWETE KATIKA KUMUENZI MWL JK NYERERE" mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo ofisini kwake mkoani Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kwanza nampongeza mwandishi kwa kuandika kitabu. Nategemea amefanya utafiti na tafakari nzito hadi akafikia kutoa msimamo wake kuhusu JK.

    Nitakitafuta kitabu hiki hima ili nikisome. Mimi ni mmoja wa wale ambao tunasema kuwa CCM imekuwa mhujumu wa fikra na mwelekeo wa Mwalimu Nyerere, kwamba CCM ni mhujumu wa mapinduzi aliyoyataka Mwalimu Nyerere. Tunasema kuwa CCM imehujumu "Azimio la Arusha," "Mwongozo," na mengine mengi aliyoyasema Mwalimu Nyerere, akifafanua dhana ya mapinduzi.

    Kwa hali hiyo, kauli kwamba JK, mwenyekiti wa hii CCM, ni mwanaharakati wa kumwenzi Mwalimu Nyerere imenitoa msituni. Mimi kama mwanataaluma nawajibika kukitafuta kitabu hiki na kukisoma, maana huenda kitanipanua upeo wa fikra.

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli tunaomba maelekezo ya jinsi ya kupata kitabu hiki. Nahisi huenda kikawa kitabu kizuri sana ambacho sijapata kukisoma maishani mwangu!

    ReplyDelete
  3. Mbele we ni mkereketwa wa chadema...hatutegemei ukatoa juu ya ccm...mafisadi wachache wenye pia na maslahi ktk hivyo vyama vyama upinzani ndio wamekiharibu chama.

    ReplyDelete
  4. Ndugu anonymous uliyeandika Oct 08, 08:21:00, napenda kusema kuwa ifike wakati wa-Tanzania watambue kuwa sisi raia ambao hatuna chama tuna haki sawa na wengine ya kuongelea masuala ya nchi yetu, bila kubambikizwa uchama.

    Msingi wa upinzani wangu kwa CCM ni kwamba hiki ni chama kinachojuhumu mapinduzi. Dhana ya mapinduzi ilifafanuliwa vizuri katika Azimio la Arusha, Mwongozo na maandishi mengine ya Mwalimu Nyerere.

    Ukiyasoma hayo, na kuyatafakari kwa kina, utaona kuwa CCM si chama cha mapinduzi, bali kinahujumu mapinduzi, na nashangaa kwa nini msajili wa vyama bado hajatambua hilo na kukifuta usajili chama hiki. Namshangaa sana msajili.

    Kwa mtazamo wangu wa sasa, kungekuwa na chama cha mapinduzi ningejiunga. Lakini CHADEMA sidhani kama ni chama cha mapinduzi. Isipokuwa nakiunga mkono kwa mambo yake mawili matatu, hasa msisitizo wake juu ya elimu, na pia harakati zake dhidi ya ufisadi.

    Ila mimi si mwana-CHADEMA, na sijawahi hata kuingia kwenye ofisi yoyote ya CHADEMA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...