Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika mazungumzo na Gavana Jenerali wa Canada Mhe. David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson na viongozi wa serikali ya nchi hiyo katika jumba la Rideau jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni huku akiangaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Mhe. John Baird baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Macdonald Cartier jijini Ottawa, Canada, kwa ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada Mhe. John Baird baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Macdonald Cartier jijini Ottawa, Canada, kwa ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi katika viwanja vya jumba la Rideau Hall jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012. Jumba hilo ndilo makazi na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangia mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi humo pia hapo ndipo hutumika kwa kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema, pa kupokelea wageni mashuhuri wa nchi za nje na pia ndipo anapofanyia shughuli zote za kitaifa akiwa kama mwakilishi wa Malkia wa Uingereza. 

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Jaman watu wa protokali mbona mnamfanyia hv raisi wetu?.kweli mnaanda ziara ya yeye kupokelewa na waziri wa mambo ya nje?hv mnajua uzito wa cheo cha rais wa nchi?hv kweli kiongozi mkuu wa canada akija tz anaweza kupokelewa na waziri Membe kweli?.watu wa protokali kuweni na heshima na rais wetu maana ninyi ndio mnaopanga hizi safari..Mh rais wangu JK siku nyingine usikubal kwenda kwenye hizi ziara ambazo haupokelew na watu wa level yako.

    Mdau Toronto

    ReplyDelete
  2. We mdau wa Toronto hapo juu,usitutie aibu. Mhe, amepokewa rasmi na gavana wa canada ambaye anamuwakilisha malkia katika nchi hiyo unayoishi wewe.muulize michuzi akupe habari zaidi mimi nimeona kwenye luninga mapokezi rasmi.

    ReplyDelete
  3. Cha ajabu kuhusu Canada: Prime Minister (mtendaji mkuu wa serikali kitaifa) anateuliwa na wananchi kupitia sanduku la kura. Kisha yeye anapendekeza kwa Malkia wa Uingereza jina la atakayekuwa Governor General na Malkia anampitisha. Governor General anakuwa na nguvu kubwa hata kumshinda Prime Minister kwa vile anamuwakilisha Malkia moja kwa moja, ambaye ndiye mwenye dola ya Canada. Ajabu la tisa na nusu la dunia.

    ReplyDelete
  4. Big up Anony wa misho Fri Oct 05, 07:59:00 AM 2012.
    Hii ni ajabu kweli..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...