Wakazi wa Kijiji cha Mkata Mkoani Tanga wakiwa na madumu yao ya maji kwenye Baiskeli zao wakati wakitoka kuchota maji katika vijiji vya jirani.kwa mujibu wa mmoja wa wakazi wa kijiji hicho (jina kapuni),amemueleza Ripota wa Globu ya Jamii (aliesimama kwa muda katika kijiji hicho akiwa safarini kuelekea jijini Arusha) kuwa katika eneo lao hili kumekuwa na shinda ya upatikanaji wa maji safi  kirefu sasa,hivyo inawabidi kwenda umbali mrefu kwa kutumia baiskeli kuteka maji hayo.
 Baadhi ya Vijana wa eneo hilo la Mkata wakijadiliana jambo na mwenzao ambaye alionekana akiulizia hali ya sehemu yanakopatikana maji hayo.
 Ukiwa ni mkazi wa eneo hili basi ni lazima ujue maji yanakopatikana ili uweze kwenda kuchota,maana bila hivyo hakuna kula wala kunywa.
Baadhi ya Watoto wakiwa kwenye moja ya Bomba lililokatika wakiteka maji kwa ajili ya Matumizi ya Majumbani kwao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hivi ndivyo ndugu zetu wanavyosherehekea miaka 51 ya uhuru karne ya sayansi na teknolojia. Wakati wenzetu wanapeleka chombo kwe sayari ya mars kufanya uchunguzi ikiwa ni pamaja na maji, sisi tunatafuta maji hapa hapa duniani.

    ReplyDelete
  2. Anonymous una sema ukweli je changamoto kwa vijana wa diaspora mna fanya nini kusaidia nchi yenu?

    ReplyDelete
  3. Sii hatuwezi kusaidia taifa wala kuwekeza kama uraia wa nchi mbili mnatubania, tukiwekeza mtataifisha mali zetu

    ReplyDelete
  4. Wadau juhudi za makusudi zinahitajika kutoka kwa wenyeji au niseme wanaotokea maeneo haya ambao wana uwezo kusaidia kutatua tatizo hili bila ya kutegemea serikali kwani tumeshaona mwendo wake. Huduma ya maji ni muhimu sana kwa maisha ya binaadam. Kuona wazee, wanawake, na watoto wakiteseka kutafuta maji kama hivi ni aibu sana. Mimi sitokei maeneo hayo lakini hii tasriwa imeniuma kibinaadam. Kaka Michuzi kama kuna mpango wa mchango wowote utapitisha basi niko tayari kusaidia chochote ili wapatiwe alau kisima cha karibu. Naweza kupatikana kwenye email yangu hii jingothegreat@hotmail.com lakini iminyie. Mdau Haji Jingo...Los-Angeles, CA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...