Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (katikati) akifafanua kwa  Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu hoja zilizotolewa na Serikali ya Malawi za kujitoa katika mazungumzo kuhusu mgogoro uliopo kati  ya Tanzania na Malawi kuhusu Ziwa Nyasa. Wengine katika picha kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule  na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju.
Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka Vyombo na Mashirika mbalimbali ya Habari hapa nchini wakimsiliza kwa makini Mhe. Waziri Membe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa, Bw. John M. Haule (aliyesimama) wakati akimkaribisha Mhe. Waziri Membe kuzungumza na  Waandishi wa Habari (hawapo pichani).
Mmoja wa Wanahabari  Bw. Florian Kaijage akiuliza swali wakati wa mkutano wao na Mhe. Waziri Membe.
Mhe. Waziri Membe (waliokaa kushoto) akionesha kwa Waandishi wa Habari Ramani mpya ya Tanzania. Wengine katika picha (aliyekaa kulia) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule akifuatiwa na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Selasie Mayunga na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria hapa Wizarani Balozi Irene Kasyanju.
Mhe. Waziri Membe akifafanua kwa Waandishi wa Habari kuwa mpaka katika ramani ya Tanzania umepita katikati ya Ziwa Nyasa na si ufukweni kama inavyodaiwa na Malawi.
Wageni waalikwa na baadhi ya waandishi wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe.

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. MMH HAWA JAMAA NI WABISHI SANA, DAWA YAO NI KUWAPIGA TU NOTHING ELSE, NAPENDA AMANI LAKINI KAMA MTU ANAKULETEA ZA KULETA LETS JUST DO IT JWTZ PLZ

    ReplyDelete
  2. ANONY WA KWANZA, VITA SI SULUHISHO. UNAWAPIGA UNAONEKANA WEWE NDIO MGOMVI UNAHUKUMIWA KULIPA FIDIA NA ZIWA UNANYANG'NYWA.

    ReplyDelete
  3. SASA KAMA MH MEMBE ANATUHAKIKISHIA USHINDI NI KWA NINI TUNAOGOPA KUPELKWA ICJ? NAJUA KUNA GHARAMA NYINGI LAKINI KAMA HUKO NDO HAKI ILIPO HATUNA SABABU YA KUZIKWEPA HIZO GHARAMA. KUTAFUTA MSULUHISHI ZAIDI YA ICJ NI KAZI BURE KWA SABABU MALAWI HAWAKUBALIANI NA MSULUHISHI MWINGINE ZAIDI YA ICJ - MTAKUWA MNATWANGA MAJI KWENYE KINU.

    ReplyDelete
  4. KAZI KWELIKWELI MATATIZO HAYO YAPO JAPAN NA KOREA KUHUSU MLIMA ULIOPO BAHARINI ILA PANDE ZOTE MBILI LIMEUPA MAJINA KILA MTU LAKE KISA UTALII

    ReplyDelete
  5. Mimi ni Mtanzania ila kihistoria malawi wako sahihi kabisa...tulia soma historia vizuri kuhusu mipaka na ziwa nyasa kwa malawi..

    Sema hii issue itaonekana Malawi wanatatizo kwa sababu tayari kuna mzimu wa Mafuta hapo.

    ReplyDelete
  6. Wewe Anony unayesema Malawi wako sahihi unaumwa ugonjwa usioujua. Tangu niko mdogo ramani zote za Afrika na ile ya Tanzania zilikuwa zinaonesha mpaka upo katikati ya ziwa. Wewe ndo hujui historia. Nahisi wewe si mtanganyika, bali ni mamluki.

    ReplyDelete
  7. Anony wa pili juu hakuna kitu kama tukiwapiga tutanyang'anywa ziwa. Uingereza walipambana na Argentina na kukitwaa kisiwa cha Falklands(Malvinas) na mpaka sasa wanakimiliki, hakuna aliyewanyang'anya haki yao. Tanzania ina wajibu wa kulinda mipaka yake kwa hali yoyote, walichofanya Malawi ni uvamizi na uchokozi.

    ReplyDelete
  8. Miaka yote nchi zikae kimya. kumeanza Asia china na japan, sudan, zanziabar kutaka kujitoa muungano sasa tanzania na malawi. Mmmh nahisi kuna program za kimataifa zinapikwa. Kwa taifa kama yenye utajiri wahali yajuu ila watu wake masikini na mali ghafi nyingi tutakuwa tunaishi na madeni mpaka kiyama. Hizi case zinahitaji pesa na naamini akitokea mfadhili tukumbuke tusishangae akapewa contract ya mika 50.DUNIA YA KIMAFYA HII...TUTAZIDI KUTAWALIWA TUKITAKA TUSITAKE.

    ReplyDelete
  9. Anony wa Sun Oct 07, 08:17:00 AM 2012 akili yako ni matope..umetumwa kuja kutoa comment humu. Tangu nianze shule ya msingi enzi hizo sikuwahi kuchora ramani halafu tukaambiwa na mwalimu mpaka umepita ufukweni. Kawaida tulikuwa tunachora katikati. Sasa kwa nini wao Malawi toka zamani walikubali mpaka wao uonekane katikati? Au kwa kuwa nao wamegundua mafuta ndo wanaona mpaka uko ufukweni?

    ReplyDelete
  10. Hawa dawa yao ni bakora tu....na haituchukui muda ni wiki moja tu rais wao anakuwa secretary wa Kikwete...!! tunawaingiza katika Muungano bila kupenda...!!

    ReplyDelete
  11. nini maana ya ZIWA NYASA? na historia yake ipo vipi,Hili ziwa ni la Mawali na linatokana na nyassa land au nyasa au niasa kama sikosei,na maana ya nyasa ni lake lakini sintofahamu ya mtafiti wa kiengereza kama sikosei alipouliza akajibiwa nyasa akafikiri ndio jina tafsiri sahihi ni ziwa ziwa, sasa lakini hata hivo haiwezekani malawi wapate lote tugawane nusu kwa nusu tu hapa.

    ReplyDelete
  12. Nashangaa na kusikitika kwamba eti inaitwa ramani mpya. Ramani tulizosomea miaka ya 1960s na 1970s (na hata siku za waliotutangulia shule)siku zote zilionyesha mpaka uko katikati. Nashangaa magazeti ya waKenya kama Mwananchi na The Citizen wanasema eti "Tanzania has unveiled a new map". Si kweli this is utter rubish, it is not a new map.
    Hata mchangiaji mmoja kati blogu hii kama wiki 7 au 9 zilizopita akaja akatuonyesha stempu ya Malawi ya mwaka 1945 ikionyesha Ziwa Nyasa na mpaka wake kati ya Nyasaland na Tanganyika ukiwa katikati. Nitashukuru kama Michuzi ataweza kututafutia tena ule mchango wa yule jamaa ukionyesha ile stempu ya Nyasaland. Please Michuzi tutafutie uianike tena kwenye Globu ya Jamii.

    ReplyDelete
  13. Mheshimiwa Anonymous wa Sun Oct 07, 08:17:00 AM 2012. Kama wewe kweli ni Mtanzania basi ni Mtanzania muuza nchi. Eti soma historia Malawi wako sahihi..... Kuna stempu za kihistoria za Nyasaland zinaoliita ziwa ziwa Nyasa alafu zinaonyesha mpaka uko katikati. Ni stempu ya 1945 na ni stempu ya Nyasaland ya kipindi hicho wala si stempu ya Tanganyika.
    Alafu international law ya mipaka kwenye maji kati ya nchi mbili inasema mpaka unawekwa katikati ya maji hayo. Kwa kuzingatia hilo mpaka kati ya Malawi na Tanzania kwenye mto Songwe umewekwa hivyo. Mpaka wa Malawi na Mozambique kwenye ziwa Nyasa umewekwa hivyo vile vile.
    Hawa Wanyasa wezi tu lakini kinachosikitisha kuna Watanzania wanataka kuwasaidia.

    ReplyDelete
  14. Jamani vita si lelemama tujitahidi kadri iwezekanavyo kuikwepa. Nchi yenyewe hii ni maskini wa kutupwa (japo ni wa kujitakia)halafu tuingie kwenye vita! Tukishamaliza kupigana na Malawi tusubiri Kenya maana na wao wanakuja kuudai mlima Kilimanjaro eti ni wao. Baada ya hapo huwezi jua kuna Kongo (ziwa Tanganyika), ziwa Victoria na ziwa Nyasa upande wa Msumbiji!!

    ReplyDelete
  15. KESI TUTASHINDA:

    ISIPOKUWA WAPELEKWE WATU WENYE KUJUA MBINU ZA MEDANI NA SIO WAENDE WATU KUISIMAMIA TANZANIA KWA MSINGI WA MAFAO YA SAFARI PEKEE, HAPANA WAWE PIA NI WATU WENYE KUIJUA SHERIA NA USANII WAKE KTK KUSIMAMIA MAMBO NYETI KAMA HILI

    Kwa hoja hizi tano (5) nafikiri tutashinda:

    1.Malawi kama inadai ziwa lote ni lake basi itaje huko MAHAKAMA YA DUNIA-ICJ nchi yeyote dunaiani ambayo ina miliki ziwa loote peke yake huku nchi nyingine jirani Mpaka wake ukiwa ufukweni.

    2.Inafahamika ya kuwa maji yana kupwa na kujaa ktk Bahari na Maziwa, huku MIPAKA YOTE IKIWA SEHEMU MAALUMU ISIYOSOGEA (FIXED LINE OF BOUNDARY-NI SHERIA YA KIMATAIFA MPAKA HUTAKIWA UWE IN FIXED POSITION (grid reference positioning,Latitute and Longitude HATA KWA SATELITE UNASOMEKA) je ktk Dunia pana nchi yenye mpaka una hama hama kwa maji kupwa na kujaa kwa maji?,,,wataje nchi yeyote ambayo mpaka wake UNA HAMA HAMA KAMA UTAKAVYOKUWA HUO WA KWENYE MAJI YA ZIWA NYASA KAMA WANAVYOTAKA WAO.

    3.INAJULIKANA KTK DUNIA YA KUWA RASILIMALI ZOTE ZA DUNIA ZINAGAWANYWA KWA WAKAZI WOTE WA DUNIA, PIA HATA WENGINE WA MBALI WANA HAKI NA RASILIMALI HASA ZILE ZILIZO ADIMU ZILIZOPO SEHEMU ZINGINE (UNESCO WORLD HERITAGE) HIVYO MPANGO WA HELIGOLAND TREATY KWA MUJIBU WA MWAKA 1890 MAKUBALIANO KATI YA WAKOLONI MJERUMAJI NA MWINGEREZA HAUZINGATII MWONGOZO HUU MPYA WA KIMATAIFA KUHUSU RASILIMALI ZA DUNIA NA MGAWANYO WAKE KWA WAKAZI WA DUNIA (walikubaliana kipindi Azimio hili halijaanzishwa, HIVYO MPAKA HUO (KUPITA UFUKWENI) NI BATILI,,,KAMA ALIVYOSEMA MHE. RAISI JAKAYA M. KIKWETE.

    4.KAMA WAO MALAWI WAKIDAI ZIWA LOTE NYASA NI LA KWAO JE NA SISI TANZANIA AMBAO ZIWA TANGANYIKA LINA JINA LETU LA ZAMANI LOTE NI LA KWETU?,,,PIA KWA NINI MALAWI WASIDAI UPANDE WA ZIWA NYASA WANOPAKANA NA MSUMBIJI?

    5.INAFAHAMIKA YA KUWA JAMII ZETU ZINA MAUNGANIKO YA KINASABA MFANO MAKABILA KAMA WAMASAI WAPO KENYA NA TANZANIA,WAJALUO WAPO KENYA,TANZANIA, UGANDA NA SUDAN PIA WAMAKONDE WAPO TANZANIA NA MSUMBIJI, PIA NI WAZI KUWA WANYASA WAPO MALAWI NA TANZANIA!

    VIVYO HIVYO KUHUSU MGAWO WA RASILIMALI ZA DUNIA KWA WAKAZI WOTE WA DUNIA, WANYASA WALIOPO TANZANIA (Ukingoni mwa Ziwa) KITAIFA NI WATANZANIA LAKINI PIA ASILI YA MALAWI WANAYO HIVYO NAO WANASTAHILI MGAWO WA ZIWA NYASA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...