Jizi hilo lisilo na aibu lilileta sms hii saa saba na dakika 27, 
 Ankal alipomjibu alipo akatuma sms ya pili hiyo na Ankal (Me) akamjibu
Jizi hilo baada ya kupiga mzinga likatoa namba ya huyo 'Shangazi' yake. Baadaye likaulizia kama Ankal kaingia geji. Ankal alipomuuliza kikao kiko wapi akasema Kunduchi Beach Resort, akiwa hajui kwamba mtandao wa Ankal umetapakaa kila sehemu. Huko Kunduchi hakuna kikao kinachoenedelea huko, na huyo Mkumbwa Ally aliyesingiziwa na hilo jizi jinga  kwanza hatumii namba hiyo. Ankal amempigia kwa namba yake halisi naye kasema  hakuandika yeye hiyo sms na hiyo si namba yake. Wadau nimeanika haya ili kuwatahadharisha dhidi ya wizi huu ambao umeingia nchini. Namba ya hilo jizi ni 0714530869 naomba vyombo husika viishughulikie haraka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

 1. SHUKRAN UNCLE KWA KUTUFAHAMISHA, HALI KWA SASA IMEKUA MBAYA SANA UTAPELI KILA KONA HUJUI HATA NANI WA KUMUAMINI,

  ReplyDelete
 2. hiyo namba ni ya polisi mmoja hapa kituoni sasa hii kali sijui itakuwaje kwani kila tukimpigia sasa imekuwa hapatikani na tunaye ofisini tatizo ni mkubwa kidogo kicheo hauliziki kwa sisi kuruti aisee noma.
  mdau.
  manzese polisi posti.

  ReplyDelete
 3. KAKA MICHUZI NIMEFURAHI UMEFUNGUKA KWA HILI JAMBO. TATIZO LIPO WAPI?

  1. TUME YA MAWASILIANO NI NGUVU YA SODA KATIKA KUHAKIKISHA KILA SIMU INASAJILIWA NA ISIYO SAJILIWA KUFUNGIWA.

  2. MAKAMPUNI YA SIMU YAMEAJIRI VIJANA HUKO MTAANI WANAOSAJILI SIMU WENGI TUNAWAONA WAKITOA VITAMBULISHO VYA WATEJA NA KUBADILI MAJINA ID NAMBA ILE ILE LAKINI WANABANDIKA VIKARATASI THEN WANATOKA NAKALA ILI WAFIKE IDADI WAPATE COMMISSION. TUMETOA TAARIFA LAKINI SI TIGO, VODA, ZANTEL WA AIRTEL WANAFATILIA USAJILI WA BARABARANI.

  3. OMBI SERIKALI IWE MAKINI KUANZIA SASA USAJILI WA SIMU UFANYIKE MAKAO MAKUU YA OFISI WA WAKALA WAKUBWA NA SI MITAANI.

  UNABAHATI HAO WEZI WA MPESA WANATUPA SIMU WAKISHAKUIBIA

  ReplyDelete
 4. Hilo ni jizi kwa njia ya TigoPesa. Hata namba inaonesha. Mpesa hawanaga matatizo hayo kabisa, na kama yapo basi sio sana. Mimi waliniliza laki saba kwa Tigopesa sina hamu nao. Halafu Tigo hawakunipa msaada wowote pamoja na kuripoti wizi huo Polisi pamoja na huko Tigo kwenyewe.

  Mungu atanilipia Inshaallah.

  ReplyDelete


 5. vizuri sana tena nahamu wangekuliza hela ili iwe vizuri kwako

  Hahaha Kwani hamkujua hilo mapema?? ni mara ngapi uncle nimekutumia email za kuanika wizi huu ukawa unabania?? nakumbuka nilikutumia email kabiaa hukuwka labla sababu unawalinda coz wanatangaza kwenye blog yako, mpaka yamekukuta ndo unaweka kwenda zako huko naoenda sana blog yako tatizo na wewe ni mnafiki sana sana kwa hapo tu ndo unanikera hata kama ukibania hii commet lakini message sent


  Ukweli ni kwamba kwa TANZANIA yetu no maendeleo mpaka mwisho wa dunia kama unabisha waulize waliopo ughaibuni hakuna unafiki na ubinafsi kabisaa kati yao ila upo kati ya mtanzania na mtanzania yote haya ni sababu ya poverty back ground

  ReplyDelete
 6. Mjomba Muchuzi pole sana kwa kukoswa koswa na wezi!

  Ama kweli Ankali na wewe ni Polisi kiasi, ingekuwa umeliwa mazima.

  Jambo lingine jamaa inanawezekana ni mmoja ktk Wadau wako akaona ni mbali kukufikia ili apate chochote baada ya kukwama kimaisha 'Mjomba zingatia tupo wengi humu Jamvini na hali zetu zinatofautiana' isipokuwa Jamaa ametumia njia isiyo sahihi.

  Bora kama alikuwa na mahitaji ya uchache angetoa taarifa zirushwe hewani hapa Jamvini kama yule dada yetu ktk Baa moja kule Sinza aliyeandika meseji ktk karatasi akipiga mizinga Wateja.

  Kwani kuna ubaya akitoa shida akatoa na namba ya M-Pesa, si atatumiwa michango kwa hiyari za wanandugu humu, badala ya mipango michafu ya wizi na utapeli?

  ReplyDelete
 7. Hakika TCRA ni kivuli tu maana wao ndio wanatakiwa watoe msaada wa haraka kubaini upuuzi huu unaofanywa. Binafsi nilipeleka taarifa ya matapeli Polisi kituo cha Kati hapa DSM lakini sioni hatua za dhati za kuwakamata. Namba zipo inakuwaje asikamatwe nae amejisajili? Kunahaja ya sisi wananchi kufikiria hatua zaidi au Wabunge wetu walivalie njuga.Ikera

  ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...