THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

BREAKING NYUZZZZZZ... MSANII SHARO MILIONEA AFA AJALINI TANGA

TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE,INAELEZA KUWA MSANII WA MAIGIZO NA MUIMBAJI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA (BONGO FLEVA),HUSSEIN MKIETY ' ALMAARUFU KAMA Sharo Milionea' (PICHANI) AMEPATA AJALI MBAYA NA KUFARIKI DUNIA  MAENEO  YA  KIJIJI CHA LUSANGA  WILAYANI MUHEZA, MKOA WA TANGA, AMBAPO NDIO NYUMBANI KWAO.

KWA MUJIBU WA WASANII WENZAKE, MWANADADA SHILOLE NA STEVE NYERERE (KWA WAKATI TOFAUTI),WAMETHIBIBISHA KUTOKEA KWA AJALI HIYO NA KUSEMA KUWA MSANII MWENZAO HUYO AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUPATA AJALI HIYO JIONI YA LEO. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA, AFANDE  CONSTANTINE  MASAWE PIA AMETHIBITISHA KUTOKEA KWA AJALI HIYO PAMOJA NA KIFO CHA MSANII HUYO ALIYEKUWA ANAKUJA JUU KWA KASI YA AJABU KWA UMAHIRI WAKE WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA PAMOJA NA MATANGAZO YA BIASHARA ALIYOKUWA AKIFANYA NA MSANII MKONGWE MZEE MAJUTO KATIKA KUTANGAZA AIRTEL MONEY.

CHANZO CHA  AJALI HIYO BADO HAKIJAFAHAMIKA.

GLOBU YA JAMII IMEPOKEA TAARIFA HIZI KWA MSHTUKO NA MASIKITIKO MAKUBWA, IKIZINGATIWA KWAMBA NYOTA YA SHARO MILIONEA NDIO KWANZA ILIKUWA INAANZA KUNG'ARA HASA BAADA YA MAREHEMU NA MZEE MAJUTO KUPUMULIA PUMZI MPYA KATIKA MATANGAZO YA BIASHARA KWA WELEDI WA HALI YA JUU KIASI CHA KUPENDWA NA KILA MTU.

TUTAENDELEA KUTOA  TAARIFA  ZAIDI KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.


MOLA AIWEKE MAHALI PEMA

 PEPONI ROHO YA MAREHEMU
AMINA


Kuna Maoni 7 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  innalilah wainna ilahi rajiun! mungu amuweke mahala pema huko aendako

 2. Anonymous Anasema:

  Inna lillahi wa inna ilayhi rajiuun dah tutakumis men.....RIP

 3. Anonymous Anasema:

  Dah! Kweli vizuri havidumu. The boy was a genius.

 4. mungu na aiweke mahali pema roho ya marehemu aminaaa........

 5. Anonymous Anasema:

  Poleni wahusika wote! Shaloo alikua mkali si mchezo, we will miss you!

 6. Anonymous Anasema:

  mungu amlaze pema peponi,japo kila mtu ana siku yake lakini haya maajari ya barabarani naona kama yanatuchukua kwa haraka sana.
  Inaniuma mno ni kijana mdogo sana ameondoka.

 7. Sogole Anasema:

  RIP Sharo Milionea