TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE,INAELEZA KUWA MSANII WA MAIGIZO NA MUIMBAJI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA (BONGO FLEVA),HUSSEIN MKIETY ' ALMAARUFU KAMA Sharo Milionea' (PICHANI) AMEPATA AJALI MBAYA NA KUFARIKI DUNIA  MAENEO  YA  KIJIJI CHA LUSANGA  WILAYANI MUHEZA, MKOA WA TANGA, AMBAPO NDIO NYUMBANI KWAO.

KWA MUJIBU WA WASANII WENZAKE, MWANADADA SHILOLE NA STEVE NYERERE (KWA WAKATI TOFAUTI),WAMETHIBIBISHA KUTOKEA KWA AJALI HIYO NA KUSEMA KUWA MSANII MWENZAO HUYO AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUPATA AJALI HIYO JIONI YA LEO. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA, AFANDE  CONSTANTINE  MASAWE PIA AMETHIBITISHA KUTOKEA KWA AJALI HIYO PAMOJA NA KIFO CHA MSANII HUYO ALIYEKUWA ANAKUJA JUU KWA KASI YA AJABU KWA UMAHIRI WAKE WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA PAMOJA NA MATANGAZO YA BIASHARA ALIYOKUWA AKIFANYA NA MSANII MKONGWE MZEE MAJUTO KATIKA KUTANGAZA AIRTEL MONEY.

CHANZO CHA  AJALI HIYO BADO HAKIJAFAHAMIKA.

GLOBU YA JAMII IMEPOKEA TAARIFA HIZI KWA MSHTUKO NA MASIKITIKO MAKUBWA, IKIZINGATIWA KWAMBA NYOTA YA SHARO MILIONEA NDIO KWANZA ILIKUWA INAANZA KUNG'ARA HASA BAADA YA MAREHEMU NA MZEE MAJUTO KUPUMULIA PUMZI MPYA KATIKA MATANGAZO YA BIASHARA KWA WELEDI WA HALI YA JUU KIASI CHA KUPENDWA NA KILA MTU.

TUTAENDELEA KUTOA  TAARIFA  ZAIDI KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.


MOLA AIWEKE MAHALI PEMA

 PEPONI ROHO YA MAREHEMU
AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. innalilah wainna ilahi rajiun! mungu amuweke mahala pema huko aendako

    ReplyDelete
  2. Inna lillahi wa inna ilayhi rajiuun dah tutakumis men.....RIP

    ReplyDelete
  3. Dah! Kweli vizuri havidumu. The boy was a genius.

    ReplyDelete
  4. mungu na aiweke mahali pema roho ya marehemu aminaaa........

    ReplyDelete
  5. Poleni wahusika wote! Shaloo alikua mkali si mchezo, we will miss you!

    ReplyDelete
  6. mungu amlaze pema peponi,japo kila mtu ana siku yake lakini haya maajari ya barabarani naona kama yanatuchukua kwa haraka sana.
    Inaniuma mno ni kijana mdogo sana ameondoka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...