Michoro ya majengo ya Ukumbi,Ofisi za Makao makuu na Hotel ya nyota tano vya CCM yalioanzwa kujengwa mjini Dodoma.
 Muonekano kwa mbali
 Mchoro wa jengo la hoteli ya nyota tano
 .Rais wa Zanzibar akiwasili eneo la Makulu mjini Dodoma kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za makao makuu ya CCM, Ukumbi wa Mikutano na Hotel ya Hadhi ya nyota tano leo.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Chama,Ukumbi wa Mikutano na Hotel za Hadhi ya Nyota Tano katika eneo la Makulu Dodoma leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

 1. Nimekubali...Dom itapendeza

  ReplyDelete
 2. Chama kina miradi gani ya kufadhili ujenzi huo, maelezo tafadhali.

  ReplyDelete
 3. Chinese wanatununua sasa..

  ReplyDelete
 4. ufisadi tu. raia hawa afford matibabu, hamna madawa mahospitalini. miradi gani isiyoinufaisha taifa.

  ReplyDelete
 5. Mwanzo mlijenga Chamwino kwa kodi za wananchi!
  Mkajenga tena Chimwaga kwa kodi za wananchi!
  Sasa tena mnajenga ukumbi mwingine kwa kupata pesa toka wapi?
  Viwanja vya mpira vyote mmejimilikisha! Wakati mlikuwa mkipita nyumba hadi nyumba kuchangia kwa lazima wakati wa ujenzi wa viwanja vile! Nakumbuka nilikuwa na duka langu la jumla wakati ule nililazimishwa kutoa pesa nyingi sana ili kuchangia ujenzi wa viwanja hivyo!
  Virudisheni kwa wananchi vyote ili pato la taifa liingie sio kuota viwanja vya ccm.
  Naomba wabunge muulize ccm ina miradi gani mikubwa ya kuweza kujenga ukumbi mkubwa wa mikutana na hotel ya nyota tano, kama sio ufisadi na mahesabu ya pesa za wananchi wanachukua bila wananchi kujua?
  Najua Michuzi, hii huwezi kuitoa kwa sababu na we unaingia polepole kwenye kundi hilo!

  ReplyDelete
 6. Kwa nini CCM iswe na majengo mapya? Si majengo tu. CCM ime uza mji wa Dar ime wazulumu wananchi majumba kwa kuzia wageni.Hakuna kipya, Baada ya mkutano na sharehe yale yale ya zamani ndiyo yata rundi. Uchawai ume kwisha sasa.Tanzania itasonga mbele.

  ReplyDelete
 7. kwa mtaji huu chadema kuingia ikulu ni ndoto mbaya sana

  ReplyDelete
 8. Acha wajenge wakati wa Watanzania kuchukua mali zao ukifika haya yote yatakuwa mali ya umma tu. Kumbuka chama cha KANU kule Kenya walijimilikisha ukumbi wa Kenyatta International Conference Centre (KICC), lakini baada ya NARC kuingia madarakani walitaifisha kituo hicho mara moja. Suala sio CHADEMA, CUF wala TLP kuingia madarakani suala ni mali za umma kuwa mikononi mwa umma, na si kuwaachia majambazi wa CCM. Na muda huo unakaribia kwa kasi sana. Wazalendo iweni na matumaini ya Tanzania njema na yenye neema bila mzimu na ajenti wa ibilisi CCM.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...