THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

kamanda wa FFU Ughaibuni Ras Makonja asakwa na jimama pesa


Katika hali ya utatanishi kiongozi wa Ngoma Africa band kamanda Ras Makunja wa FFU amejikuta akipewa mashaka ya maisha na mwanamama moja kisa wimbo "Mama Kimwaga"  ambao takribani mwezi mzima wimbo huo na nyingine za bendi zimekuwa zikipigwa mara kwa mara na kituo cha Radio Funk haus,inayorusha matangazo mjini Bremen,Ujerumani. 

Mwanamama moja ambaye aliguswa sana na ujumbe wa nyimbo hiyo aliamua kutinga katika ukumbi wa mazoezi wa bendi hiyo mjini Oldenburg,mkononi akiwa na bakora ! mdomoni yakiwa yanamtoka maneno ya hasira,alisikika akidai kuonana na mkuu wa kikosi kazi cha Ngoma Africa aka FFU kamanda Ras Makunja,kwa bahati mbaya alijibiwa na wanamuziki waliokua pale kuwa Kamanda hayupo. 

Alipoulizwa kulikoni ?Jimama Pesa huyo alisikika akidai kuwa alikuja kumtia adabu Kamanda Ras makunja wa FFU,jimama pesa lilikoroma na kutema kibesi kuwa wimbo ule wa "Mama Kimwaga" ujumbe wake unamnyima raha jimama huyo mwenye kuongea kiswahili kinachoonyesha kuwa anatoka nchi jirani kwa watani wa jadi. 

Jimama pesa hilo limedai kuwa hakutegemea kabisa kama wimbo ule wa "Mama Kimwaga" ungepelekwa tena kwa maDJ wa redio Bremen na kurushwa hewani Ujerumani kote kwa kupitia sauti ya Funk Haus Europa, wanamuziki aka "maafande" wa Ngoma Africa band wakimtetea Boss wao Kamanda Ras Makunja,wamedai kuwa hawezi kuingilia uhuru wa ma Dj wa redio kwa CD hiyo ilikuwapo pale redio siku nyingi,na katika CD hiyo aliyeimbwa ni "Mama Kimwaga"  sasa inakuaje ? kamanda asakwe
na bakora ka kushtumiwa kuwa anaziwia ridhiki ya mahitaji ya starehe ya jimama pesa .wanamuziki wa ngoma africa
wanamuhoji mwanamama anayemsaka kwa bakora kamanda wao Ras Makunja,ambaye mara nyingi anadaiwa kuwa ni mtunzi na mwimbaji mwenye darubini kali. wimbo huo pia unasikika at www.myspace.com/thengomaafrica pia
 at


Kuna Maoni 5 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Polisi Ujerumani nadhani itakuwa makini sana kuhakikisha inamdhibiti Jimama Pesa huku Kamanda Ras Makunja anakuwa salama na amani!

 2. Anonymous Anasema:

  Sidhani kwa mkasa huu Kamanda kama atanusurika kuchapwa bakora za matakoni kwa ukosefu wa adabu,Jimama pesa zidisha mwendo Kamanda lazima achapwe bakora

 3. Anonymous Anasema:

  Jimama mipesa anataka kuwafunga midomo ffu bin watoto wa mbwa kwa bakora,te!te!te! Kikamnda ketu cha ffu kinaonja choto ya jiwe

 4. Anonymous Anasema:

  jimama pesa ,pole sana lakini wewe inasemekana ndie uliowapa ffu jina la "WATOTO WA MBWA" unachokivuna ni halali yako,lakini si unawajua ffu tabia zao? wasije kuanza kukusaka wewe

 5. Anonymous Anasema:

  ole wako mama kama wakikugeuza kibao ndio utawajua kuwa hao si vijana wema kabisa