Wananchi mbalimbali wakishuhudia Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akiwahishwa katika Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akitolewa katika Chumba cha Huduma ya Mwanzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.
Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akipandishwa kwenye Gari ya Wagonjwa kwa lengo la kuwahishwa katika Hospitali ya Muhimbili Dare es Salaam baada ya kurushiwa Tindi kali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazowezi huko katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Dah kweli Zanzibar ubinadamu umeisha ! siashangai ilianza kuuliwa kwa askari polisi na sasa naibu mufti.Unyama gani huu ? tutakwenda kujibu nn kwa Mungu kesho. Tunasahau huyo mzee mwenye familia yake na inamtegemea.Endeleni tu na uchafu wenu mnaoufanya na Serikali endeleeni kukaa kimya.Si ndio mnayoyaona mazuri hayo kuchoma maskani,maduka ya biashara,kuuwa,na sasa kutumia acid.Lakini ipo siku patachimbika hapo Zanzibar,subiri siku hazigandi.

    ReplyDelete
  2. Matunda ya Uamsho hayooooo!

    Je SMZ itaweza kutoa huduma ya Masks yaani 'viziba uso' kama vile Israel ilivyokuwa ikipigwa vita vya Iraq na Saddam mwaka 1991?

    ReplyDelete
  3. jamani hapo nikwamba hao uamsho hawawataki waislam wenzao wanataka wao ndio wasikilizwe na mihadhara yao na misikitini sasa wameshindwa wanaona bora wawaue au kuwaharibia wenzao wafungwe.kwa mtu ambae hajui kuhusu hili anaweza akasema wakrito ndio walio fanya hili,wakristo wenyewe ni wakuhesabu hapo zanzibar.Na pia wakristo wote wana akili ya kufikiria familia zao hawafanyi vitu kwa kukurupuka.

    ReplyDelete
  4. Mdau wa kwanza, mauaji mbona hata bara yapo? Tumuombe Mungu tu atuepushie vita kwani huko tuendako hali si shwari kama hawatatafuta suluhisho la matatizo ya watanzania.

    ReplyDelete
  5. DUH! POLE SANA, TUNAKUOMBEA DUA UPONE HARAKA.

    HIVI JAMANI TUMELONGWA? TUMEINGIWA NA NINI, INA MAANA IMESHAKUWA UNYAMA, UNYAMA.

    HAKHI YA NANI! NAONA NI SAWA YA YALE ALIYOSEMA BABA WA TAIFA, KUHUSU KULA NYAMA YA MTU. UKISHAANZA KULA HUWEZI KUACHAAA...........

    ReplyDelete
  6. Wauza ACID wote sasa lazima wapate kibali cha polisi. Pia, mnunuzi wa ACID lazima apate kibali cha polisi kabla ya kuuziwa. Kumbukumbu ziwekwe kwa aliyenunua na aliyeuza, tarehe, saa, kitambulisho, namba ya simu iliyosajiliwa, anwani yenye uthibitisho, wingi wa acid usiozidi battery ya gari. Pia iwe marufuku kuingiza battery za gari zenye kujazwa ACID. Kusiwe na sababu ya raia wa kawaida kutumia ACID.

    ReplyDelete
  7. Kina jambo hapa c bure, wanatafuta la kuwasingizia UAMSHO ili yao yatimie huwezi zuia mabadiliko kwa vsababu vdogo vyakisikizia watu tu.. tusipotoshane hapa UAMSHO hawausiki kwa lolote hapo.. ni siasa chafu tu za wapuuzi wachache kutaka kuharibu umoja wawazanzibari

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...