Gari aina ya Mitsubishi Fuso lenye nambari za usajili T 612 BHY limepiga mwereka mchana wa leo maeneo ya Tabata Matumbi kama unaelekea Ubungo kwenye Barabara ya Mandela.Chanzo cha kutokea kwa ajali hiyo bado hakijafahamika na hakuna mtu yeyote aliejeruhiwa wala kupoteza maisha.
Gari hiyo ikiwa imelala ubavu baada ya kupiga mweleka mchana huu.
Yaani ni taabu tupu kila kukicha maisha ya watu yanateketea na mali zao pia, ebu fikiria kwa taarifa ambazo zimefanikiwa kuripotiwa dhidi ya kupinduka kwa magari ni mbili kwa siku ya leo yaani hii na ile ya dakawa morogoro iliyochukua maisha ya abiria wanne, bahati taarifa zote zimeambatanishwa na picha za hayo magari yaani ni mabovu sijui nani anayaruhusu aidha kutembea au kubeba watu? jamani wahusika tuwe makini ktk usajiri na hata ukaguzi.
ReplyDeleteKupitia taarifa hii namkumbusha pia mdau mmoja siku za nyuma aliwahi kuchangia kwamba precision air wanunue ndege zilizotumika asome au aone hizi taarifa.