THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MSIBA NEW YORK, Marekani, na Shirati, Tanzania


Marehemu Jesca Emmanuel

Mhe. Tuvako Manongi, Balozi  wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  kwa majonzi makubwa, anasikitika  kutangaza kifo cha  Jesca Emmanuel  (12), Mtoto wa  Afisa mwenzetu  Bw.  Emmanuel Swere Alfred  na Bi Doto, kilichotokea ghafla siku ya Jumapili 18/11/2012 katika Hospitali ya Mt. Sinai, Queens, New York. Taratibu na mipango ya  kuusafirisha Mwili wa Marehemu Mtoto Jesca kwenda kijijini  Bumbombi- Shirati Tanzania kwa mazishi  zinaendelea kwa usimamizi wa Ubalozi na Familia ya Marehemu.

Taarifa zaidi  zitatolewa na Ubalozi  kuhusu  siku, tarehe na  mahali tutakapomuaga   mpendwa wetu  Jesca Emmanuel.

Raha ya Milele Umpe Eee Bwana, na Mwanga wa Milele Umuangazie apumzike kwa amani. Amina
  
UBALOZI WA TANZANIA  UMOJA WA MATAIFA
 NEW YORK


Kuna Maoni 8 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Jamani it is just so sad to see the little ones going so soon! Mtoto mzuri... looking so sweet but she's no more! It is heartbreaking to the parents, family and friends. Mungu awatie nguvu na awaondolee majonzi yatokanayo na msiba huu mzito. May God grant this beautiful angel everlasting peace. Pumzika kwa amani mtoto mzuri!

 2. Anonymous Anasema:

  Dah! Poleni wazazi ndugu na marafiki, inasikitisha sana, juzi tu mtoto Daniela tuomeona ameenda, but dont worry, she is at Peace in ALLAh's beautiful heaven, he was looking for a beautiful flower to place somewhere in his heaven and he chose this little angel... inauma sana but ALLAh atawajaalia Subira InshaALLAh, sote ni wa ALLAh na kwake ndio marejeo yetu, RIP beautiful Angel ..Amin

 3. Anonymous Anasema:

  Poleni wafiwa. So sad. Siwajui wazazi wala marehemu mwenyewe lakini this untimely death imenigusa sana. It is a loss to the family and the nation maisha yapokatika mapema hivi. My heart and prayers go to the bereaved family. Kama mzazi, I can feel your pain.

 4. Mulashani RC Anasema:

  R.I.P sweet daughter, May Our Almighty God shines all your way! Wazazi, ndugu jamaa na marafiki jipe moyo mkuu maana tumaini letu ni ktk Bwana aliye hai! Mapenzi yake yatimizwe.... ni mshumaa umezimika ghafla ktk umri huu wa matumaini! Inauma sana.

 5. Anonymous Anasema:

  Sifahamiani na hii familia wala ya Daniella lakini misiba hii imeniumiza sana, imeniuma mno, Poleni sana wazazi, kama mzazi naelewa ni wakati mgumu kiasi gani mnaopitia, Mungu pekee ndiye mfariji wenu,kama msemaji aliyetangulia hapo juu ni siku chache tumesikia juu ya malaika mwingine Daniella,na leo malaika mwingine tena, tunaumia ila hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo.

 6. Anonymous Anasema:

  Sifahamiani na hii familia wala ya Daniella lakini misiba hii imeniumiza sana, imeniuma mno, Poleni sana wazazi, kama mzazi naelewa ni wakati mgumu kiasi gani mnaopitia, Mungu pekee ndiye mfariji wenu,kama msemaji aliyetangulia hapo juu ni siku chache tumesikia juu ya malaika mwingine Daniella,na leo malaika mwingine tena, tunaumia ila hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo.

 7. Anonymous Anasema:

  Poleni sana wafiwa, kwakweli kwa wazazi hakuna kitu kinasikitisha kama kuondokewa na mtoto... The angles.
  Masikini, alikuwa anaumwa nini, mbona ghafla hivi???

  Pole saana, may you find comfort in God's hand

 8. Anonymous Anasema:

  Pole sana kwa famila.