THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Ngoma azipendazo Ankal

Leo Ankal anaamka na 'Treat her like a Lady' ya The Temptations. Ankal anashukuru kwa kuungwa mkono kwa safu hii kwa wapenzi wa muziki wa zamani na wa sasa kwa kuwa kila upande unaburudika na kujifunza mengi. Ieleweke enzi hizo ngoma zilikuwa zinapigwa 'kavukavu' na hamna kutegemea kompyuta na ala zinazojipiga zenyewe.

Kama itakumbukwa kwa jiji la Dar es salaam kulikuwa na viota vingi vya disko, ikiwemo YMCA iliyokuwa inatamba kwa Disko Toto kila Jumapili jioni chini ya DJ Kalikali na DJ Neagre Jay, RSVB ya Mbowe hotel na DJ Jerry Kotto na Seydou, Valentino Discotheque iliyokuwa Continental hotel Mtaa wa Nkrumah, Space 1900 iliyokuwa chini ya DJ Paul MacGhee pale Vision hotel (zamani Maggot), Rungwe Oceanic ya Kunduchi chini ya DJ Young Kim, Motel Agip chini ya DJ Bonny Luv, Keys hotel mtaa wa Uhuru alikuwapo DJ Eddy Sally  na kadhalika. Wenye data ya madisko ya mikoani kama vile Arusha 'Cave', Iringa, Mbeya na Mwanza kazi kwenu...


Kuna Maoni 12 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Asante Ankal.
  Arusha nakumbuka Mawingu Disko kule njiro we bwana wee

 2. Anonymous Anasema:

  Ankal nae anakumbukwa enzi zile anapiga picha YMCA, picha yako unachukua weekend inayofwata hahahahahaha

 3. Umewasahau DJ Ebonite Woo Jack, DJ Richie Dillon, DJ Luke Joe, DJ John Peter Pantalakis, DJ Joe Johnson Holela n.k

 4. Anonymous Anasema:

  Umewasahau kina DJ Ebonite Woo Jack (Richard Mazula), DJ Richie Dillon, DJ John Peter Pantalakis, DJ Joe Johnson Holela, DJ Deo Composer, DJ Danny Star (Mzambia), DJ Luke Joe

 5. Anonymous Anasema:

  Mwanza ilikuwa mambo ya Alshers chini ya DJ Richie Dillon, palikuwa hapatoshi

 6. Anonymous Anasema:

  Moshi town kulikuwa na Dj Issa kibaya kwenye kiota cha Liberty Hotel.

 7. Anonymous Anasema:

  nyie acheni tu kifo kibaya jamani. inanikumbusha marehemu mmoja baada ya mwingine. tumshuru mola kwa kuendelea kutupa uhai. hii ardhi kweli inameza watu!!!!!

  Lakinu tusisahau ujumbe ya huu mwimbo hasa kwenye kudhamini wake zetu. Kwa mfano:

  "....When I was young, my mama used to say,
  Boy, A woman's like a flower, with love on her you shower...Ever since that day, her words never went away...I always will remember to treat my baby tender..."

 8. Anonymous Anasema:

  Pia usisahau mwananyamala B Villa Motel kulikua mashindano ya disco kila weekend.

 9. Anonymous Anasema:

  Duuuu nakumbuka mbali sana!

  Dj.Ebonite Woo Jack, pana Dj. mmoja amefariki Marekani miaka ya karibuni alikuwa ni mzaliwa wa Iringa ila alianza kazi zake Dar na baadaye kuhamia Philadelphia Marekani,,,naomba nikumbushwe ni nani yule?

 10. Anonymous Anasema:

  Duuuu nakumbuka mbali sana!

  Dj.Ebonite Woo Jack, pana Dj. mmoja amefariki Marekani miaka ya karibuni alikuwa ni mzaliwa wa Iringa ila alianza kazi zake Dar na baadaye kuhamia Philadelphia Marekani,,,naomba nikumbushwe ni nani yule?

 11. Anonymous Anasema:

  Msimsahau Dj. Young Millionaire alikufa kwa ajali ya Gari maeneo iliyopo makutano ya Holiday Inn Hotel na njia ya Haidery Plaza.

 12. Anonymous Anasema:

  Choggy Sly


  Msimsahau Dj. Nguli huyo !