Tanzania ni moja kati ya nchi kumi zilizochaguliwa ili kuwa mwenyeji wa mkutano wa aina hii ya kipekee wa kwanza kutokea unaohusisha wataalamu wa afya na usafi wa mazingira na wataalamu wa teknohama utakaofanyika tarehe 1/12/2012 unaolenga moja kwa moja katika utafutaji na uundaji wa mifumo au njia mbali mbali zitakazosaidia kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya afya na usafi wa mazingiraWakati asilimia 90 ya watanzania wana huduma ya choo ni asilimia 12 tu ambao wana huduma hiyo katika hali ya usalama inayolinda afya bora. Jumuiya mbali mbali za wanateknohama ndani ya nchi na duniani kote zimeonekana kuwa na nafasi na uwezo mkubwa wa uundaji wa ufumbuzi utakaosaidia kuongeza  idadi na kufuatilia maboresho ya vyoo na usafi wa mazingira.  

Sanitation Hackathon* itafanyika katika majiji mbali mbali makubwa kwa muda mmoja tarehe 1/12/2012 – 2/12/2012. Majiji hayo ni pamoja na Dar es Salaam(Tanzania), Cape Town (Afrika kusini), Dakar (Senegal), Dhaka (Bangladesh), Helsinki (Finland), Jakarta (Indonesia), Lahore (Pakistan), Lima (Peru), London (Uingereza), Pune (India) and San Francisco, New York na Chicago (Marekani).

Ili kuandaa shughuli hii, wataalamu wa masuala ya afya na usafi wa mazingira wanafanya kazi bega kwa bega na wadau mbali mbali katika ngazi ya jamii ili kuandaa na kuchanganua changamoto kuntu ambazo zinaweza kutatuliwa kwa kupitia matumizi ya teknolojia za mawasiliano. Waandishi wa program na wataalamu wa data wataungana katika marathoni hii ili kuunda mifumo mbali mbali itakayotumika kutatua changamoto zinazoikabili sekta hii ya afya na usafi wa mazingira.

Shughuli hii ambayo nchini imepewa jina la  ‘Bongo Safi’ itawezeshwa na Benki ya Dunia kupitia kitengo chake cha teknolojia za mawasiliano pamoja na washirika wengine  ambao ni KINU (jumuia ya teknolojia za mawasiliano iliyo wazi kwa wote), (Kamisheni ya sayansi na teknolojia ya Tanzania (COSTECH),Jumuiya za wataalamu kutoka  programu ya  teknolojia za mawasiliano inayoendeshwa Tanzania, Wizara ya Afya na maendeleo ya jamii, WaterAid, UNICEF,Taasisi ya utafiti wa tiba (NIMR) pamoja na washirika wengine wengi. Tarehe 24 hadi 25 Novemba wataalamu wa teknohama, wataalamu wa takwimu za jiografia na waandishi wa habari walisafiri kwenda Rufiji na Tandale kupata uelewa wa changamoto za afya na usafi wa mazingira katika kiwango cha chini. Mpaka sasa wataalamu 130 wamekwisha jiandikisha kwenye Sanitation Hackathon.

The Sanitation Hackathon inakuja ikiwa ni mfuatano na maboresho ya “Water Hackathon” ambayo pia iliandaliwa na kuwezeshwa na benki ya Dunia mwaka wa 2011 ambayo wataalamu wa teknolojia za mawasiliano wapatao elfu moja walijiandikisha katika sehemu zipatazo kumi duniani. Wataalamu hao waliunda mifumo mbali mbali katika utatuaji wa changamoto zinazoikabili sekta ya maji. Baadhi ya Mifumo iliyoundwa imeboreshwa na inawekwa tayari kwa ajili ya matumizi makubwa zaidi. 



Tarehe muhimu za Sanitation Hackathon:
• Tarehe ya mwisho ya usajili wa wataalamu wa teknolojia za mawasiliano: Novemba 28, 2012
• Uchangiaji mawazo kati ya wataalamu wa teknolojia za mawasiliano na wataalamu wa afya na   usafi wa mazingira: Novemba 28, 2012
• Sanitation Hackathon: December 1-2, 2012
Zawadi 
Washindi watatangazwa siku ya mwisho ya Hackathon ambayo ni tarehe 2 Desemba 2012 na zawadi kwa washindi hao zitakua ni  upatikanaji wa malezi-taalamu kwa washindi kutoka kwa wahisani mbali mbali.

*‘Hackathon’ ni mashindano ya  uchangiaji mawazo ya kitaalamu yahusishayo wataalamu wa masuala ya uundaji programu za kompyuta kwa ufanisi ili kuunda mifumo itatuayo  changamoto na matatizo mbali mbali .

Anwani Muhimu:
Washington: Edward Anderson,  +1 202 473-8563 eanderson1@worldbank.org
Global Sanitation Hackathon: Vivek Raman, +1 9111 4147-9471vraman1@worldbank.org
Nairobi: Toni Sittoni:  +1 202 123-4567tsittoni@worldbank.org
Dar es Salaam: Jason Cardosi,  +255 22216-3286jcardosi@worlbank.org
Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea tovuti yetu: www.sanitationhackathon.org/dar-es-salaam
Kwa usajili tafadhali tembelea tovuti hii: www.bongosafi.eventbrite.com
Jiunge nasi Facebook: http://www.facebook.com/bongosafi
Tufuate kwa kupitia Twitter: #bongosafi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...