THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.


Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Roma, unapenda kuwakumbusha Watanzania wote muishio Roma na Italy kwa Ujumla kuwa, Jumamosi ya tarehe 24 Novemba 2012, kutakuwa na Mkutano wa Kufunga Mwaka wa Jumuiya ya Watanzania Rome kuanzima saa kumi jioni kwenye Ukumbi wa Wakenya Uliopo Via Giovanni Lanza 122 Mjini Roma.

Karibuni tupeane mawazo mapya, tudumishe Jumuiya yetu na turekebishe kwa pamoja pale palipo na upungufu!
Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania na Mungu ibariki Jumuiya ya Watanzania Roma.

KARIBUNI TUPEANE MAWAZO MAPYA, TUDUMISHE JUMUIYA YETU NA TUREKEBISHE KWA PAMOJA PALE PALIPO NA 

Kwa maelezo zaidi Mnakaribishwa kutembelea
 Na Ndg. Andrew Chole Mhella
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma.


Kuna Maoni 3 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Tuko pamoja wana wa Tanzania!

  Wandugu Roma Italia tuwe sote pia tushirikiane na kupena taarifa za ukweli na uwazi kuhusu mustakabali mbali mbali kwa faida zetu sote huko nje na sisi huku nyumbani Tanzania.

  Msiwe kama wanajumuiya Ugiriki ambao walikuwa wanatoa taarifa za upotoshaji na wakawa wabishi sana kuhusu hali halisi ilivyo kuwa inawakabili huko walipo, kitu ambacho sio kizuri.

  Tukumbuke ya kuwa 'mficha maradhi Umauti humuumbua'!

 2. Anonymous Anasema:

  Sawa sote ni ndugu moja sisi na Kenya isipokuwa na ninyi mjitahidi mara ingine mje mfanyie shughuli yenu kwenye 'PUB YA WATANZANIA' badala ya 'PUB YA WAKENYA'!

 3. Anonymous Anasema:

  Angalau safari hii mmejitahidi kwa kuandaa Kikao chenye viburudisho na Mziki,

  Ni vile safari ya mwanzo Kikao cha mwezi Mei-2012 meza zilionekana nyeupeee chupa moja kubwa ya 'MAJI YA UHAI YA HUKO ITALIA' tena ikiwa meza ya mbele, High Table !

  Tulijiuliza huku tulipoona meza nyeupa tofauti na vikao vya Canada na Marekani wakiturushia picha zao meza zimenona , tulifikiri au wandugu Italia nao wamelaliwa na Mitikisiko wa Kifedha na Kiuchumi kama Ugiriki?