Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Roma, unapenda kuwakumbusha Watanzania wote muishio Roma na Italy kwa Ujumla kuwa, Jumamosi ya tarehe 24 Novemba 2012, kutakuwa na Mkutano wa Kufunga Mwaka wa Jumuiya ya Watanzania Rome kuanzima saa kumi jioni kwenye Ukumbi wa Wakenya Uliopo Via Giovanni Lanza 122 Mjini Roma.

Karibuni tupeane mawazo mapya, tudumishe Jumuiya yetu na turekebishe kwa pamoja pale palipo na upungufu!
Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania na Mungu ibariki Jumuiya ya Watanzania Roma.

KARIBUNI TUPEANE MAWAZO MAPYA, TUDUMISHE JUMUIYA YETU NA TUREKEBISHE KWA PAMOJA PALE PALIPO NA 

Kwa maelezo zaidi Mnakaribishwa kutembelea
 Na Ndg. Andrew Chole Mhella
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Tuko pamoja wana wa Tanzania!

    Wandugu Roma Italia tuwe sote pia tushirikiane na kupena taarifa za ukweli na uwazi kuhusu mustakabali mbali mbali kwa faida zetu sote huko nje na sisi huku nyumbani Tanzania.

    Msiwe kama wanajumuiya Ugiriki ambao walikuwa wanatoa taarifa za upotoshaji na wakawa wabishi sana kuhusu hali halisi ilivyo kuwa inawakabili huko walipo, kitu ambacho sio kizuri.

    Tukumbuke ya kuwa 'mficha maradhi Umauti humuumbua'!

    ReplyDelete
  2. Sawa sote ni ndugu moja sisi na Kenya isipokuwa na ninyi mjitahidi mara ingine mje mfanyie shughuli yenu kwenye 'PUB YA WATANZANIA' badala ya 'PUB YA WAKENYA'!

    ReplyDelete
  3. Angalau safari hii mmejitahidi kwa kuandaa Kikao chenye viburudisho na Mziki,

    Ni vile safari ya mwanzo Kikao cha mwezi Mei-2012 meza zilionekana nyeupeee chupa moja kubwa ya 'MAJI YA UHAI YA HUKO ITALIA' tena ikiwa meza ya mbele, High Table !

    Tulijiuliza huku tulipoona meza nyeupa tofauti na vikao vya Canada na Marekani wakiturushia picha zao meza zimenona , tulifikiri au wandugu Italia nao wamelaliwa na Mitikisiko wa Kifedha na Kiuchumi kama Ugiriki?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...