Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Mkadam Khamis akimpa Taarifa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ya kukamilika rasmi kwa matengenezo ya choo maalum cha kuchunguzia wasafiri wa anga wanaotiliwa mashaka kwa kujihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya kilichopo uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar Nd. Said Iddi Ndembwagani mara baada ya kuwasili uwanjani hapo kukaguwa choo maalum kwa ajili ya kuchunguzwa wasafiri wanaotuhumiwa kuingiza dawa za kulevya nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Bongo bwana sasa choo cha nini wekeni camera za (in consumption) kila kitu mtakiona na si kuweka choo mpate gharama za kununua dawa za kuwapa waharishe tena ili zoezi liende sawa vinginevyo ni wastage of time.

    ReplyDelete

  2. Sasa wakishaziona watazitolea wapi

    ReplyDelete
  3. Mdau wa pili anony Thu Dec 06, 10:47:00 AM 2012

    ...Sasa wakishaziona watazitolea wapi.
    -----------------------------------
    JIBU:
    -----------------------------------
    Ili kukwepa Bajeti ya juu na gharama za dawa za kuwafanya kuharisha wameza Madawa ya Kulevya anatakiwa aajiriwe Mpishi wa UGALI WA DONA LA MABUNZI NA MAHARAGE, na BAJETI YA CHAKULA HICHO MAGUNIA KADHAA IWEPO HAPO JIKONI UWANJANI, Mpishi atakuwa na jukumu la kusonga ugali mgumu ukiiva analishwa mmezaji wa Madawa kwa kila mmoja anapewa Kipimo cha DONA LA KILO MOJA NA BAKULI LA MAHARAGE YA MBEYA ni lazima akimaliza 'Mlima' huo ataomba apelekwe chooni na hapo mzigo utashuka tu!

    DONA MCHEZO?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...