Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akimvisha mkanda wa ubingwa wa WBF,bondia Francis Miyeyusho baada ya kumtwanga Nassibu Ramadhani kwa T.K.O raundi ya kumi.kushoto ni promota wa mpambano huo,Mohamed Bawazir.
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akimpongeza Bingwa wa WBF,bondia Francis Miyeyusho baada ya kumtwanga Nassibu Ramadhani  kwa T.K.O raundi ya kumi.kushoto ni promota wa mpambano huo Mohamed Bawazir.
Bondia Francis Miyeyusho (kulia) akionesha ufundi wake kwa kumtupia masumbwi Bondia mwenzie,Nassibu Ramadhani wakati wa Mpambano wao wa kuwania ubingwa wa WBF uliofanyika jana jioni kwenye Ukumbi wa PTA,Sabasaba jijini Dar es Salaam.Miyeyusho alishinda mchezo huo kwa T.K.O raundi ya kumi.
Bondia Francis Miyeyusho (kushoto) akimpatia dozi za kutosha mpinzani wake,Nassibu Ramadhani wakati wa Mpambano wao wa kuwania ubingwa wa WBF uliofanyika jana jioni kwenye Ukumbi wa PTA,Sabasaba,Jijini Dar es Salaam.Miyeyusho alishinda kwa T.K.O raundi ya kumi.
bondia Francis Miyeyusho akiwa amebebwa juu juu na mashabiki wake huku akiwa na mikanda yake miwili aliyoshinda baada ya kumtwanga Nassibu Ramadhani.

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila kushoto akiwa na wadau waliojitokeza kuangalia mpambano huo.Picha na Super D Boxing 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Sasa kaka francis kwanza nakupongeza kwa ushindi pia najua utakua umepata fedha japo kidogo ila si kitu nachotaka kukushauri ni kutengeneza mwili wa kimichezo hasa masumbwi simaanishi mwili jumba hata ila ongeza kidogo nyama kwa kwenda gym ili mwili uwe kama wa mwanamasumbwi wa kweli ili hata sisi tulio mbali na huko tuweze kuvutiwa na hatimae kuweza kufanya biashara za kweli maana kwa miili hiyo tunaogopa hata kukualika kwa mpambano kwa kuhofia kupotezana na kupata lawama bure zisizo na msingi.

    ReplyDelete
  2. Ebwana michuzi bondia wetu anayekwenda german kutuwakilisha atapigana lini vile? nazungumzia cheka wa morogoro?

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza unaandika pumba, do you know Joe Calzaghe?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...