Mdau Alex Kajumulo ametuletea hii akitana wadau muipitie na kuona kama inafaa kuwa UZI wa  timu yetu ya Taifa (Taifa Stars).Wadau mnasemaje juu ya hili??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. SIO MBAYA Ila chata yake sio muhimu kwa kweli

    ReplyDelete
  2. ina too much makorokocho!

    ReplyDelete
  3. Inafaa 100%. Ni best kiliko zote nilizoona

    ReplyDelete
  4. ipo fresh sio mbaya akapewa dili la kutegeneza....tuache unafiki na majungu

    ReplyDelete
  5. Mbaya mnoooooo!

    Hivi ni lazima kuweka rangi zote za bendera kwenye jezi zetu za timu ya Taifa??!!!

    ReplyDelete
  6. mimi naona rangi nyeusisi aweke itapendeza.hiyo inaonekana kama imefanana na jezi ya zanzibar.mimi sijaipenda.

    ReplyDelete
  7. Upangaji wa rangi bado ni tatizo sugu. Jezi zinawekwa rangi zoote mpaka inachukiza.Hata kama unataka kutumia rangi zote mpangilio uwe simple. kuweni wabunifu kidogo.
    Mzozaji.

    ReplyDelete
  8. rangi nyeusi ambayo ni rangi muhimu haimo hivyo HAIFAI !

    asante !

    ReplyDelete
  9. Hii haifai kuwa jezi ya Taifa kwa kuwa jezi haina rangi nyeusi ambayo iko kwenye bendera yetu

    ReplyDelete
  10. Hiyo nembo yake(KAJUMULO)inatia shombo hapo vinginevyo poa tu!

    ReplyDelete
  11. kajumulo ni mbuga gani ya wanyama TANZANIA? au unauza sura

    ReplyDelete
  12. Tunaweza kutengeneza jezi ya taifa kwa kombinashen 24. Kumbuka hesabu za form four the combination and permutation. Bendera yetu ina rangi 4 kwa hiyo ni 4X3X2X1.

    ReplyDelete
  13. vilaka vingi bana hiyo ssiyo afadhali hata zingine,kwani hiyo nayo kama zile zingine tu

    ReplyDelete
  14. Lete, lete, lete, lete, lete!!!

    Alex Kajumulo bwana kaka,

    Fanya mambo uzi unafaa kabisa huo lete lete lete!

    Kama unavyoona brother Kajumulo Kikosi chetu cha Taifa kiko hoi bin taabani kwa upande wa nyuzi!!!

    ReplyDelete
  15. BABU KAJU NAMKUBALI SANA SANA KTK VIFAA VYA MICHEZO.. HII SIO MBAYA LAKINI NAONA HIZO RANGI MBILI (NJANO) ZA KARIBIA NA SHINGONI UNGEZITOA..
    SHUKRAN

    ReplyDelete
  16. Yaelekea alitaka kuinclude rangi za bendera ya taifa. Lakini nadhani amesahau rangi yetu ya asili, nyeusi.
    Hata hivyo nampa big up kwa kujaribu..

    ReplyDelete
  17. Maoni yangu.Si mbaya lakini yafuatayo yangerekebishwa.
    1.Nembo zake(kajumulo) zimekuwa nyingi mno kama vile siyo ya taifa bali ni ya kajumulo stars.Apunguze hata kama ni mdau mkubwa.
    2.Rangi za bendera ya taifa hazijakamilika.Zingine hazipo.
    Ni hayo tu

    ReplyDelete
  18. tunaomba kajumlo, angalie wapi pa kuweka rangi yetu nyeusi.

    ReplyDelete
  19. nimeshasema mara kadhaa. Nembo ya TFF inabidi ipitiwe na wataalamu. Hii nembo haina hadhi kabisaa...imekaa kichovu sana. Kwana kuna ubaya gani ku-adopt nembo mpya? Wapeni vijana kazi wawaletee nembo nzuri ya TFF hii nembo ni vurugu tupu haina hadhi ya kitaifa. Kuna wadau wengi wanaweza kuanzia hapo. Kwa ujumla hii Jezz bado inatakiwa kazi kiasi...!!bado haijavutia sana....!!

    ReplyDelete
  20. kwani uzi wa sasa una shida gani? MBONA uzi huu una nembo ya Kajumulo badala ta Taifa stars? Halafu mbona uzi huu hauna rangi nyeusi? Mi nilidhani Mr. Kajumulo si raia tena wa tz!

    ReplyDelete
  21. Hapana,haifai.

    David V

    ReplyDelete
  22. Ni Nzuri lakini naona rangi nyeusi inakosekana, kwa hiyo nadhani ingwekwa katikati ya rangi ya njano ya pembeni. Yaani punguza size ya strip ya njano ili ziwe mbili halafu katikati ndio hiyo nyeusi

    ReplyDelete

  23. infaa sana ila tungeomba tuonee na huko mgongoni kuna rangi na alama gani?? je mtu binafsi ukitaka kupata nakala yako utapataje?? thanks babu kajo for your contribution to our country.

    ReplyDelete
  24. Its a good thing to see a Tanzanian doing great thing.Keep it up bro!uzi uko poa sana na ninaunga mkono hoja.Mungu ibariki nchi yetu

    ReplyDelete
  25. Hiyo KAJUMULO ndio imechukua nafasi ya Nike, Adidas, Puma...siyo?

    Mimi naona siyo sawa, iwekwe TANZANIA, maana kutokana na uwezo wetu waTZ, kesho atatokea MURJI, CHUDASAMA, MUSHI, MWASAKAFYUSI, RAMIA, CHOLO...

    JE, SI ITAKUWA VURUGU MECHI?

    ReplyDelete
  26. Wabongo 2napenda Kukosoana Saana ...Majungu Meengi..Uzi Uko Poa..Bob Kaju Mwaga Nyuki...

    ReplyDelete
  27. Mpangilio wa rangi mbovu.!!!...sio lazima kuwa na rangi zote za bendera ya Tanzania kwenye jezi. Uzi huo haufai..!!

    ReplyDelete
  28. Si lazima kila rangi iliyopo kwenye bendera iwepo kwenye jezi thts y inaonekana too complicated!

    ReplyDelete
  29. Mimi niulize timi ya taifa jee taifa gani ninavyofahamu mimi TANZANIA ni muungano wa nchi mbili yaani ZANZIBAR na TANGANYIKA na ZANZIBAR tuna timu yetu bendera yetu na wimbo wetu wa Taifa sasa hili laplap la hapo juu sielewi la taifa gani au ndio Tanganyika any way ikiwa ni hivyo why dont you made it clear and call it Tanganyika star. Acheni ujinga huo mtu hakatai asili yake.

    ReplyDelete
  30. Pengine mimi macho yangu hayaoni rangi vizuri lakini ninaiona rangi nyeusi chini ya rangi ya manjano au macho yangu? S.C. Toronto, Canada

    ReplyDelete
  31. Siyo kwamba wabogo wanapenda kukosoa na majungu mengi kama mchangiaji mmoja alivyosema, aliyeiweka jezi hiyo kwenye mtandao alihitaji watu watoe maoni yao ili kama kuna marekebisho yafanyike. Tafadhari heshimu mawazo ya wengine hata kama yanapingana na yako. Ndg Kajumulo, nembo yako haihitajiki kwenye jezi ya timu ya taifa iondoe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...