Balozi Ankal Muhidin, 
Salamu zenu wana jukwaa kutoka jijini Kampala Uganda. Baada ya salamu waungwana, napenda niungane nanyi kuchangia mada ya juzi ya ndugu yetu bw. John Mashaka kuhusiana na sarafu moja ya Afrika mashariki ambayo mjadala wake umeshika kasi kubwa hapa jijini kampala. 


Magazeti, redio na hata vituo vya televisheni, vimekuwa vikijadili na kupinga wazi wazi hii mada kwa kina sana. Magazeti ya(The Monitor<http://www.monitor.co.ug/Business/Prosper/Uganda-not-ready-for-East-African-common-currency/-/688616/1635480/-/id0wduz/-/index.html na East African Herald<http://www.eastafricaherald.com/2012/12/East-Africa-Currency.html) ilipinga wazi wazi huu mungano

Baadhi ya raia nao wamekuwa wakitoa maoni yao; wamekuwa wakishirikishwa katika huu mjadala na vyombo vya habari na asilimia kubwa wanaoshirki hawakubaliani na serikali yao kuingia katika umoja wa sarafu katika jumuiya ya Afrika mashariki. Waganda wengi hawaoni maana yoyote ya hii sarafu zaidi ya sifa za kisiasa zinazotafutwa na viongoziNamaanisha kwamba, waganda wengi hawaafikiani na serikali yao kutumia sarafu tofauti na shillingi wanayotumia sasa hivi. Wengi wanatabiri mtafaruku mkubwa sana hapo mbeleni ikiwa serikali yao itakubali matumizi ya sarafu ya jumuiya. Baadhi ya nchi jirani inaonekana kuwa na ajenda ya siri kwenye huu muungano, na waganda wakiingia kichwa kichwa, itakula kwao.Nadhani hata sisi watanzania tusipokuwa makini katika hii swala la sarafu moja, tutakumbwa na matatizo makubwa sana hapo mbeleni. Jirani zetu ni wajanja, waliza na ardhi, wakaja ajira, na sasa ni sarafu. Watanzania inabidi tuwe makiniNdugu yetu Mashaka John aliandika makala nzuri sana hapa kwenye blog yetu iliyobeba ujumbe mzito wa kitaaluma ambayo kwa wengi wenye uelewa ilitufungua macho. Nchi yetu haipo tayari. Matayarisho yetu ya awali hayatoshelezi ushirika wetu kwenye sarafu moja.Matatizo barani ulaya yanatosha. Wagiriki wanaokota vyakula kwenye dampo za takataka kutokana na mataziyo yaliyoletwa na EuroNina uhakika Rais wetu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na umakini wake, tayari ameshaona janja ya nyani ya jirani zetu na kamwe hatoruhusu nchi yetu kutumiwa na hawa watu wenye ajenda zao za siri kwenye muungano huu wenye hofu.Bandugu, mnaoneleaje hisi swala, je tupo tayari kujiunga kwenye hii sarafuMdau,Gilbert Ruheza Rutabanzwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. MUUNGANO WA SARAFU EAC HAUBEBEKI:

    Mahitaji yake ni magumu kutekelezeka yaliyokuwa magumu sana ni haya hapa,

    1.Kunahitajika kuchangia mapato ya Rasilimali ina maana mapato (Resource revenue sharing among nations)

    Mali za TANZANIA, Gas na Mafuta, Uranium, Diamonds, Steel, na Madini na rasilimali zingine, Mali za UGANDA Mafuta na Kahawa mapato yao kwa kuwa ktk Muungano wa Sarafu ni mujibu yatumike kwa nchi zote za Umoja zikiwemo zisizokuwa na mali hizo kama KENYA, BURUNDI na RWANDA.

    Hivyo Maumini wakubwa wa sera hii unakuta ni zile nchi zisizokuwa na mali (Kenya,Rwanda na Burundi)ili ziweze kunufaika na Rasilimali za wengine.

    UGUMU: UGANDA NA TANZANIA KAMWE HAZIWEZI KUKUBALI KUCHANGIA MAPATO KTK RASILIMALI ZAO HUKU WENGINE WAKIWA HAWANA MALI

    MFANO JUZI TU ,ILIPOTOKA TAARIFA YA KUTOKUFIKIA MALENGO YA KUELEKEA UMOJA WA SARAFU ILIYOPANGWA IWE DESEMBA-2012 TAYARI KENYA NA RWANDA WANAHARAKATI WAKUU WA SERA HII YA UMOJA WA FEDHA WAMEPANGA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA IDHAMINI MFUMO WA MALIPO NA MABADILISHANO (PAYMENTS AND CLEARING SYSTEM FOR EAST AFRICAN BANKS) KWENYE MIRADI YA MIUNDOMBINU NA MASUALA YA KIFEDHA KTK AFRIKA YA MASHARIKI.
    -----------------------------------

    2.Benki kuu moja kwa nchi zote (a single central Bank)
    Ili kufikia majukumu ya kudhibiti mfumuko wa bei, kudhibiti ukosefu wa ajira na kudhibiti mzugnuko wa kifedha lazima pawepo na Benki kuu moja ktk nchi za Umoja itakayokuwa na mamlaka na nguvu zaidi kuliko Benki kuu za kila nchi mwanachama.

    UGUMU: HAKUNA NCHI MIONGONI MWA WANACHAMA ITAMWANIMI MWENZA KUWEKA BENKI KUU IWE KWAKE, MFANO KENYA HAIAMINIKI MWENENDO WAKE KTK MASUALA YA KIFEDHA, PIA KWA VILE YENYEWE HAINA UHAKIKA WA AMANI NA UTULIVU ,PIA INA DOSARI KUTOKA KUMBUKUMBU YA AFRIKA MASHARIKI ILIYOVUNJIKA MWAKA 1977
    -----------------------------------

    3.Kuwa na Wizara moja ya Fedha iliyokuwa Mhimili na yenye nguvu na Mamlaka kwa nchi wanachama kuliko Wizara za Fedha za kila nchi. (Single Central Finance Ministry and Treasury administration)

    UGUMU: KILA NCHI MWANACHAMA HAIMWAMINI MWENZIE KUWA NA WIZARA MHIMILI Y FEDHA
    -----------------------------------

    4.A strong Common Secretariat (Mamlaka yenye nguvu ili kuzipangia nchi wanachama Sera na Mielekeo)

    UGUMU: HIYO MAMLAKA YA AFRIKA YA MASHARIKI BADO HAIJAIMARIKA KIUWEZO NA NGUVU ZA UTAWALA, MFANO KENYA IMETOA DIRA YA KUFUNGUA MILANGO YA AJIRA HUKU IKIBANA KISANII MZUNGUKO WA WAFANYAKAZI KWA KURUHUSU WAWE NA UMRI WA KUANZIA MIAKA 35 NA KIPATA CHA US$ 24,000 KWA MWAKA, EAC IMESHINDWA KUDHIBITI NCHI NA SERA ZAO KAMA KUONDOA VIKWAZO VYA USHURU (NTB-Non Tariff Barriers)
    -----------------------------------

    5.A single Political Federation (Shirikisho moja la Kisiasa)

    UGUMU: SHIRIKISHO LA FEDHA LINAHITAJI SHIRIKISHO LA KISIASA LILILOIMARIKA , WAKATI TUKITAKA SHIRIKISHO LA KIFEDHA SHIRIKISHO LA KISIASA HALIJAIMARIKA HADI SASA.
    -----------------------------------

    Mapungufu ni mengi kufikia Shirikisho la Kifedha huku uaminifu na maslahi bianfsi baina ya nchi ikiwa ndio mihimili mikuu inayojenga harakati za KENYA na RWANDA nyuma ya pazia.

    ReplyDelete
  2. Sarafu moja imewashinda umoja wa nchi za Ulaya sasa wanayumba kiuchumi.

    ReplyDelete
  3. John Mashaka:Kumbe hizi mada muhimu zinaweza kuandikwa kwa kiswahili rahisi tu na zikaeleweka(na kizungu kwa mbali pale penye ulazima).Angalia huyo mtoa comment wa Kwanza alivyoshusha NONDO za nguvu na zinaeleweka hata kwa sisi ambao haya masuala si fani yetu lakini tukisoma tunaelewa.Asante wewe mtoa cooment wa kwanza.

    David V

    ReplyDelete
  4. Jamhuri ya Kenya (REPUBLIC OF KENYA)

    Ndiyo nchi pekee inayokosa usingizi juu ya mwendo kasi wa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA baada ya mafanikio makubwa ya kuzipata rasilimali, Gas,Oil,Uranium,Steel na Madini mengine kibao.

    Muelewe ktk maisha yetu inapotokea yule mtu anaye mdharau mwingine ikiwa mdharauliwa akifanikiwa kimaisha ni lazima mwenye kumdharau moyo utamuuma!

    Kila uchao Jirani zetu wanatudharau ktk vyombo vya habari vya kidunia, wanatufanyia kampeni chafu sana na hujuma nyingi sana lakini wapi HUWEZI KULIZIBA JUA KWA UNGO hii imedhihirika.

    SASA PAMOJA NA DHARAU ZAO IMEKTOKEA WANAKUJA KUONA RASILIMALI ZETU ZITAWANUFAISHA ENDAPO TUTAINGIA KTK USHIRIAKIANO KAMILI AMBAO MIHIMILI YAKE MIKUU NI VITU HIVI:

    1.KUTUMIA SARAFU MOJA
    2.KUWA NA SHIRIKISHO MOJA LA SIASA
    3.KUWA NA BENKI KUU MOJA

    ReplyDelete
  5. %he so called educated TZ people are treating kenyans as junior partners in the East African union. A few educated Tanzanians like the so called Mashaka john, are spreading rumors and unfounded lies about Kenya, that Kenya will grab Tanzania land, Kenya will take their jobs, Kenya this, Kenya that. This is what we call cheap propaganda and Kenyaphobia in Tanzanians heads. If you have self confidence on yourselves, why fear Kenyans?

    A few educated Tanzanians instead of educating their citizens on how to create jobs, they are turning on propaganda like the so called Mashaka John whose main job is to demonize Kenyans. Kenyaphobia is everywhere in TZ because of misguided people like Mashaka. Of course Kenyans are more educated and competent on their job in the entire EA. That is why Kenya is the most developed of all countries in East Africa

    Tanzania and Burundi are the least developed, and being in the same union with Kenya, TZ has a chance of being a regional number two. Once we have one currency or our countries are united, most likely, Kenya will export its educated labor force to help Tanzania develop its own talents and resources. The first EAC died because Nyerere and Iddi Amin did not want to listen to Kenyatta good advice and these people living in exile with Iddi Amin mentality should not dictate your future

    TZ are good neighbors and should avoid Mashaka john’s cheap propaganda. This cult-like leader who has built huge blind following is not a hero as some see him. He is a propagandist like any other politician. He is not a Tanzanian after all; he is a Hutu and former refugee who once lived in a refugee camp in Kenya during his early (90’s) teenage years. He is trying to exploit his political ambitions by making Kenyans look evil. He has been Tanzania attack dog against Kenya which is not good in our relations.

    Mashaka was pointless in his arguments. His victory was mastery of English, which Kenyans taught him and that is the only praise he can get. John and his followers know that it will be better for Tanzania to allow Kenya farmers help develop its land than let the Chinese and Arabs grow food and fuel for their countries.
    What is happening in Europe is because they borrowed too much. In East we don’t borrow especially in Kenya we don’t depend on foreign aid. Single currency is good for our economies because it will make our countries compete with the USA and EU in trade. We will have negotiations power in trade and militarily we will. Our TZ friends should join Kenya so they can also learn from Kenya’s 2030 vision which will make the EA like Switzerland. Tanzania is on the losing end if it can follow people like these with their own political agenda

    Nairobian

    ReplyDelete
  6. Mdau wa kwanza, hapo ktk pointi zako NO.1 umepiga kwenye Kambi kuu ya Jeshi Penmtagon,

    Katika suala la (Resource revenue sharing among nation) Republic of Kenya kwa kutumia Usanii wao wameenda mbali!

    Kwa kuwa wamejitambua ya kuwa panahitajika kuchangia Mapato ya rasilimali wakati wao wakitaka kunufaika na rasilimali za wenzao huku wao wakiwa hawana vyanzo hivyo, wamelazimisha vitu hivi:

    1.Wameiagiza Kampuni ya TULLOW OIL PLC. iliyokuwa inafanya utafiti wa Mafuta nchini Uganda mwaka 2006 na ikayapata ifanye utafiti wa Kisanii na kutoa ripoti ya kuwa kwa kuwa Bonde la Ufa la Kenya linashabihiana na Bonde la Albertine la Uganda ambako mafuta yamepatikana ya kwamba na Kenya Kampuni hiyo imeyapata mwezi March 2012, kitu ambacho hakuna uhakika kama yatakuwa na thamani ya kibiashara (commercial viability) kitu ambacho hadi sasa Serikali ya kenya imeshindwa kutoa tamko kuhusu uhakika wa Kibiashara na kiuchumi wa matokeo ya utafiti huo wa patikanaji wa mafuta.

    2.Wameialika pia Kampuni iliyopata Gas pwani za Tanzania Msumbiji, Kampuni ya Uingereza ya BG PLC. kwa kigezo cha kuwa miamba ya bahari zetu inashabihiana hivyo inaweza kupata, Kampuni ilifanya mpango huo huo wa utafiti wa kisanii vivyo hivyo mbivu na mbichi bado kutolewa na Serikali ya Kenya huku ikijulikana wazi kuwa sio rahisi kupata gas na mafuta ktk mwamba wa bahari wa Kenya na hata yakipatikana uwezekano wa mafuta yao kuwa na manufaa ya kibiashara na kiuchumi (Commercial viability) bado ni mgumu, wangemshirikisha Bingwa wa Miamba Prof. Muhongo Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania angewapa mbivu na mbichi pia hawawezi kumshirikisha kwa kuwa wanajua wazi Usanii wao hauwezi kutimia kwake.

    Kilichobakia wao wanatengeneza Propaganda za upatikanaji wa mali ili nao waonekane wana mali ya kushirikiana na nchi zingine Afrika ya Mashariki.

    UPATIKANAJI WA MALI ZA RASILIMALI KAMA GAS, OIL ,URANIUM NA VINGINEVYO UNAGOMBEWA KAMA MPIRA WA KONA NA WAWEKEZAJI WA DUNIA, HIVYO MALI IKITHIBITIKA KUWEPO MUHUSIKA HUNA KAZI YA ZIADA KUTAFUTA WAWEKEZAJI NI VILE MALI INAJINADI YENYEWE NA WAKATI MWINGINE MITAJI INAUZWA NA KUNUNULIWA MIONGONI WA WAWEKEZAJI.

    MFANO WALIOPATA MAFUTA UGANDA TULLOW OIL PLC.(Kampuni ya Canada) WALIPEWA DAU LA KWANZA NA KAMPUNI MOJA YA Uingereza kwa bei ya US$ 1.9 BILLION WAKATI WAKISUBIRI WAMEJITOKEZA KAMPUNI KUU YA MAFUTA NA GAS YA UWEKEZAJI YA SERIKALI CHINA ''China National Oil and Gas Exploration and Development Corporation'' (CNODC) IMETANGAZA DAU KUBWA ZAIDI LA US$ 3.1 BILLION !

    Hivyo Kenya ielewe ya kuwa rasilimali ikipatikana kamwe hainadiwi kwa uratibu bali hugombewa kama mpira wa kona na wawekezaji!

    ReplyDelete
  7. Monetary Union:

    Hili Shirikisho la Sarafu moja ni Meli ya sumu ama yule samaki mwenye sumu Kasa aliyewahi kuua mamia ya watu Visiwani Pemba.

    1.kenya yenyewe inamezea mate kuutaka huo Muumngano wa Sarafu moja, wakati hapo hapo ikihofia kushushwa kwa thamani ya Fedha zake kwa kuwa ili kuipata Sarafu moja pana mahitaji magumu haya hapa:

    -Inflation rate/ Mfumuko wa bei uwe karibu sawa kwa nchi zote.
    (Zipo nchi zinatumia ukusanyaji wa Kodi kupitia ukata wa Kiuchumi. inflation-'TAXATION WITHOUGHT REPRESENTATION' ili kuuweka sawa Uchumi wake na mzunguko wa kifedha)

    -Common Key Rate of Exchange kwa zile Fedha muhimu za Kigeni USD,GBP, EURO na YEN ziwe ktk kiwango kimoja kwa hela za nchi zote Wanachama yaani 1 KEN Shs=1TZN Shs=1 UGA Shs, huku Rwanda na Burundi zikiwa hazitumii kabisa Shillings zikitumia FRANCS, kitu ambacho Kenya yenyewe ni vigumu kukubali azimio hili ingawa inataka Muungano wa Sarafu Moja EAC!.

    -Fiscal Deficit/ Mbonyeo wa Ukosefu na upatikanaji wa Ajira uwe sawa kwa nchi zote huku Kila Benki kuu ya nchi zetu ikitumia kuchezesha Infation na Unempoyment ili kuuweka sawa uchumu wake na kwa kudhibiti thamani ya sarafu.

    -Bond Market, panahitajika Uaminifu na Uadilifu sana ktk masuala ya Dhamana za Madeni na ufanyaji wake wa Biashara hasa kwa ngazi ya Kitaifa Primary Market than Secondary Market.

    Pana aina kadhaa za Dhamana za Madeni 'Bonds' ambazo Benki kuu na Mabenki ya Kibiashara huweka hisa hizo za Dhamana za Madeni ktk Vikapu au mafungu makuu matatu (3) HTM-Held to Maturity(Dhamana zinazowekwa hadi zifikie muda wa kuuzwa), HFT-Held for Trading (Dhamana zilizopo kwa kuuzwa kwa tija zitakapohitajika) and AFS-Available for sale(Dhamana zilizopo Sokoni tayari kwa kuuzwa). hivyo huwezi hamisha Dhamana kutoka fungu moja hapo kwenda fungu lingine kwa Sheria za Kimataifa za MASOKO YA DHAMANA NA BIASHARA YA DHAMANA ZA MADENI (Bonds Trading) HAIKUBALIKI, LAKINI mabenki kadhaa ya nchini KENYA yalifanya hivyo mwaka huu mwanzoni ili kuficha hasara za Biashara za Hisa kwenye Taarifa za Kifedha za Mabenki yaliyouza Hisa.

    ReplyDelete

  8. Nairobian *hapo juu* anahitaji kujiheshimu mwenyewe kwanza vinginevyo ajue kwamba katengeneza ufa zaidi. Kwanza sote tunajua kwamba utajiri wa Kenya ni wa wazungu wanaoishi Kenya, huku waswahili wa Kenya wakiwa hoi bin taabani. Hao wachache wenye mali Kenya, na nyang'ao kadhaa wala siyo wawakilishi wa wakenya.
    Pole sana Nairobian kwa your ignorance.

    ReplyDelete
  9. You Nairobian, you are pathetic and an idiot. Hivi una beef na watanzania au na mashaka? unazani hicho kiingereza chako kinatutisha au kinaweza kulinganishwa na cha mashaka? muungano hatuingii, nyie watu hovyo sana. nyang'au

    ReplyDelete

  10. "Nairobian", it is not fear we TZ's have towards Kenyans. It is CAUTION.
    Which is justifiable from Data provided from posts, these people are providing FACTS.

    Keep dreaming, "a vision which will make the EA like Switzerland"

    Please leave us with our tortoise pace, we can take care of ourselves si ndio.

    BY THE WAY, WILL THE 2030 VISION REMOVE THE MATHARE VALLEY SLUMS?

    ReplyDelete
  11. Nairobian:

    Anonymous Fri Dec 07, 03:46:00 PM 2012

    Your views are mostly 'productive' but even Kenya itself fears parts of the process towards EAC integration.

    -It is recently it has been trumpeting much on Monetary Union but last week it has slowed down on fearing if it join it's currency will be subject to devaluation.

    Not only Tanzanians are fearing,even Kenya is fearing also building Limbo thinking in their mind about the EAC integration.

    -Let us look on Labor issue, Kenya imposed that they are open doors for EA workers from other member countiries but they should be from 35 yrs old and having an annual income from US$ 24,000.00(No or few people at this age of 35 will be interested to work in Diaspora anymore, also few Tanzanian especially the target group youths abd Higher education Graduates will not qualify at this), while Tanzania has made rising Foreign Worker's permitts Fees.

    -No country in the world will agree to intimidate it's people on their status of employement despite it is an economic phenomena that happens a country to admit Foreign labor but on strict conditions or un avoidable situations may be nationals are not fulfilling the labor demand of the concerned field or specialization of work.

    Recently the Former EAC General Secretary Ambassador Juma Mwapachu has just released his well authored book about all EAC countries individual allegations in BLACK and WHITE (fears and wishes among the EAC countries) in the same topic that we are discussing here at this Blogspot panel.

    ReplyDelete
  12. Niko na wakenya huku ughaibuni, wanaiba hadi vijiko. Ukidondosha hata dola moja akaiona anakaa kimya kisha anaiokota na kuifanya yake. Watu wa ajabu sana hawa. They are so greed.

    ReplyDelete
  13. Lisetn Nairobian anononymous Fri Dec 07, 03:46:00 PM 2012


    1.Knowing a little English like the one you have doesn't mean you are well educated, there are some of the world countries like Germany,France,Japan,China and others are highly developed but not English Countries!

    2.Nothing like that you say Kenyaphobia from Tanzanians, and even John Mashaka tells the truth that even Ugandans have said in their medias ''NOT READY AND DOES NOT WANT MONETARY UNION'' as presented by the Columnist Gilbert Ruheza Rutaganzwa a Tanzanian based in Kampala-Uganda.

    3.Tanzania land is already for Tanzanians as it's Land Ordinance says.

    4.Every country in the world MUST protect it's labor market for its citizens first, but allow foreign workers under un avoidable circumstances, even Kenya is doing this , there fore Nairobian you, your brothers and sisters will have look employment at Kericho Tea Farms there in Kenya first before expecting foreign work in other EAC member counrties, it will depend whether to get work or not but not 100% because JUST you are a citizen of EAC!.

    5.Please, do not convict John Mashaka with Hutu sentiments in ethnicity, he is 100% genuine Tanzanian, it is you who is a NUBIAN originated in South Sudan and you are not Kenyan, you were left by your fellow who returned to their country after South Sudan Independence lasy July-2011.

    6.Even Tanzania has got piles of piles of educated people, it is not true to say most Tanzanians are un educated!

    7.We have enough Diaspora Community across the world higly educated in all fields of education and professions
    -Doctors,
    -Scientists,
    -Researchers,
    -Engineers,
    -Nuclear Engineers and Scientist like our Vice President Hon.Dr.Gharib Bilal
    -Insurers
    -''many Bankers'' like John Mashaka
    -Eminent and Senior Diplomats like Hon. Dr.President Jakaya Kikwete,

    Those to give axcess labor force in case necessary and not Kenyans, to do this our Government of Tanzania has close Diplomatic ties and different Programs structured to connect them back home, there fore we don not expect Kenyan labor force.

    8.We have abundant resources
    -Gas
    -Oil
    -Uranium
    -Steel
    -Manganese
    -Coltan
    -Copper
    -Gold
    -Nickel
    -Gemstones

    There fore this resource base will atract our foreign investors to bring with their experts to work with educated Tanzanians named at No.7 above and not Kenyans.

    9.Tanzania with such basement No.7 and No.8 with other factors it is ''MUST BE'' NO.1 in EAC and not No.2 as you said it is Kenya may be will be No.2 or Rwanda.

    10.With having URANIUM we Tanzania ''MUST BE'' Military power Economic,Political,Financial and Economic power in the region and the world at large.

    GOT THE POINT NAIROBIAN???

    ReplyDelete
  14. Mdau wa 13 hapo juu ANONYMOUS WA Sat Dec 08, 12:46:00 PM 2012

    Kamasi zitamshuka Nairobian!

    Si mchezo point hizo 10 hapo juu amepiga Mkenya wa Nairobian Mabao 10-0

    Bao la Matokeo Uwanjani Namboole ktk CECAFA Jijini Kampala Uganda sasa linasoma hivi:

    Tanzania(Mdau wa kumi na tatu) -10
    Kenya(Mdau wa Jijini Nairobian)-0

    Wakenya kwa hoja tunawafunga hivi je kivitendo mtatuweza Watanzania?

    Kwa pointi 10 zenye akili za Mdau wa 13 hapo juu!!!

    ReplyDelete
  15. IN SWAHILI:

    Wakenya,

    Piga ua kama itakubalika suala la Umoja wa Sarafu BENKI YA AAFRIKA YA MASHARIKI ni LAZIMA iwe ktk JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kwa kuwa MZIGO MKUBWA ANABEBESHWA MNYAMWEZI!, kwa wingi wa mali tulizonazo Tanzania Gesi,Mafuta na Madini, Rasilimali ya Utulivu, huku tukizingatia Uwezo wenu KENYA ktk WIZI NA UFISADI.

    AMA SIVYO HAITAWEZEKANA KAMWE!

    -----------------------------------

    IN ENGLISH:

    kenyans,

    Incase it becomes the issue of Monetary Union subject to be approved,THE EAST AFRICAN CENTRAL BANK it is MUST BE in THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, for our Nyamwezi Tribesmen (most mascular energetic bodied people) saying that the big load must be carried on the back or shoulders of such NYAMWEZI Tribesman!, for our abundant resources that we have got in Tanzania like Gas, Oil and Minerals, Resource of Peace and stability,while considering KENYA'S ability in FELONY AND GRAFT.

    IF NOT, WE SAY IT CAN'T WORK!

    ReplyDelete
  16. Ndugu Gilbert Ruheza Rutabanzwa,

    Ahsante kwa Makala hii pamoja na mwendelezo wa ile ya kwanza ya Ndugu John Mashaka,

    Kama mnavyoona wewe na wengi wa Wadau waliochangia suala hili ni tete kwa maana ni Mtego wa Panya, gusa unase.

    Kama unavyoona ktk Ushirikiano huu, baadhi ya nchi hasa Kenya na Rwanda zinaegemea zaidi ktk Miswaada na Maazimio yanayokuwa na manufaa kwao zaidi kama(Muungano wa Sarafu, Masuala ya Ajira,Ardhi,Mitaji n.k.)

    Kitu ambacho wengine hatuwezi kukubali!!!

    ReplyDelete
  17. Nairobia anonymous of Fri Dec 07, 03:46:00 PM 2012

    You can see with the Resources base named by Commentor No.13 above anonymous of Sat Dec 08, 12:46:00 PM 2012

    WITH HIS 10 COUNTS OF POINTS ESPECIALLY No.7 and No.8 KENYA DOES NOT HAVE,

    1.SUCH TECHNOLOGY FOR OIL AND GAS INCLUDING THE REST OF SENSITIVE MATTERS LIKE URANIUM AND OTHERS.

    2.ENOUGH CAPITAL FOR DEALING WITH THESE VENTURES.

    What small knowledge Kenya has is the ability for it's labor force with their Nursery education to work at Tea Plantations and Tea Factories there in Thika and Kericho within Kenya and not in Gas, Oil and Nuclear Plants of future Tanzania!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...