Katika kuizunguka dunia nashukuru nimetembelea nchi nyingi duniani ikiwa barani Afrika na kwengineko ambako nimejaaliwa kutembelea.Nimekuwa najifunza kila kukicha jinsi watu wanavyoishi na mazingira kwa ujumla.

Kati ya nchi saba za Afrika nilizobahatika kutembelea moja ya nchi ambazo naweza kusema watoto wadogo walio na chini ya miaka 16 wamekuwa wakijihusishaa na masuala ya vilevi kama Pombe,Bangi na madawa ya kisasa ya kilevi `Drugs` ni nchi ya South Africa.South Afrika ni moja ya nchi ambazo zimepiga hatua kimaendeleo kati ya nchi nyingine za Afrika.Tatizo linakuja pale wenzetu wanavyoutumia uhuru wa malezi vibaya. 

Nikizungumzia malezi nazungumzia makuzi ya watoto na wazazi wao.Ndugu zetu wa South Afrika wametoa uhuru kwa watoto wao vibaya sana tofauti na mila na tamaduni za makabila au nchi nyinginezo barani Afrika.Nchini South Africa kumuona mtoto wa kike anavuta bangi ni jambo la kawaida,kuwaona wanafunzi wakiwa na pombe ni kitu cha kawaida tofauti na kwengineko barani Afrika.

 Suala zima la uhuru kwa watoto lisipotiliwa mkazo na kipaumbele tutakosa wataalamu wazuri duniani,totakosa taifa bora lenye upeo mzuri kimaendeleo,na hii sio tu kwa South Afrika bali na kwengineko duniani.Malezi bora kwa watoto ni jukumu la mzazi na mtu yoyote mwenye kuelewa umuhimu wa ulezi.Nasema hivi nikiwa na maana nyingi ila mojawapo ni kwamba anapoathirika mtoto wa mwenzio kumbuka hata wewe athari hizo zitakuathiri na wewe kwa njia nyinginezo.


Picha ya juu ukiangalia vyema utaona jinsi gani wanafunzi walivyoshiriki katika suala la ulevi na kinachofuata hapo ni ngono zembe,kubakwa pasipo kutarajia,maambukizi ya ukimwi na magonjwa mengineyo ya zinaa.

 Mwanafunzi mlevi kwa asilimia kubwa hana muelekeo mzuri katika masomo yake.Wazazi chonde chonde tuwaangalie watoto wetu ili kulinusuru Taifa letu.

Nawatakia jumapili njema na hii ni zawadi yenu kwa siku ya leo kwenye sherehe za miaka 51 ya uhuru wa Tanganyika.
mzingatie ujumbe wetu wa leo.

Mdau
Maganga One.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mdau asante kuonesha huruma yako kwa waafrika. Tatizo la SA ni maisha waliyopitia. Jamaa zetu hao wametawaliwa na wakoloni kwa muda mrefu. Kama mnavyojua wakoloni hawakutaka kuondoka South Afrika. Na kutokana na ubaguzi wao, hawakutaka kuona mwafrika anakuwa sehemu ya maisha yao. Hivyo katika mikakati yao ya kuhakikisha muafrika hawi sehemu yao, waliazimia kuwaangamiza kwa namna nyingi kadiri ilivyowezekana. Hata hivyo kwa kuwa kuna sheria za kimataifa, na pia waliogopa historia isiwashitaki, waliamua kuwapa uhuru waafrika kushiriki katika mambo yasiyowaletea maendeleo ili mwisho nature ichukue mkondo wake. Tatizo letu waafrika ni kuupokea huo uhuru bila kutumia akili. Ukiangalia hata hapa Tz utakuta sasa hivi kuna mkakati mkubwa sana wa kuwahamasisha vijana kujielekeza zaidi kwenye mambo ya starehe kama vile fiesta, n.k. Lego ni kuwafanya vijana wetu wasiwe na akili ya kuhoji mambo na mwisho watawala wafanye wanavyotaka. Hivyo ndivyo walivyofanyiwa wazaire (DRC) ambapo karibia wote walijihusisha na muziki huku madini yao yakiibiwa.

    ReplyDelete
  2. MASOMO ,ELIMU NA ULEVI ni USIKU NA MCHANA!

    Haiwezekani mtu bora akajengeka kutokea katika mazingira ya ulevi, iwe nyumbani au Shuleni.

    Wanafunzi hasa wa Elimu ya Juu msilete ubishi kusema ya kuwa mpo umri wa zaidi ya Miaka 18 ambapo mnahesabika ya kuwa muwatu wazima hivyo mnaweza kuruhusiwa kuvuta sigara na kulewa, ndio inawezekana lakini isizidi ikapitiliza hadi kuangusha magari network kuzima na kadhalika.

    Au msije mkasema mnajipoza kwa ugumu wa masomo.

    Ni muhimu kujibana na matumizi ya ziada wakati mkiwa mngalipo masomoni ili muweze kuwa zao bora baadae.

    ReplyDelete
  3. Hasara kwa Taifa!

    Kwa mzazi hana hasara kwa kuwa mzazi akisha zaa mtoto akiharibika anabakia kutoa laana tu na kutafuta njia ingine ya kukabiliana na maisha.

    Isipokuwa hasara inakuwa zaidi kwa Taifa kutokana na gharama kubwa ya huduma za kijamii na kiraia mtu anaiingizia Serikali na Taifa kiujumla huku akiwa ni mzigo na hata tija.

    Hatuwezi kujenga zao bora la Wahitimu wa Masomo ili kujenga Taifa ilhali wanafunzi wakiwa Masomoni wanakata maji!

    ReplyDelete
  4. aCHA UJINGA WEWE, INAANZA KUWA HASARA KWAKO KABLA YA TAIFA. TAIFA LINAKU-DELETE.

    ReplyDelete
  5. Wewe Mdau wa nne juu (4) Anonymous wa Mon Dec 10, 12:31:00 PM 2012

    ..aCHA UJINGA WEWE, INAANZA KUWA HASARA KWAKO KABLA YA TAIFA.

    -----------------------------------
    Akili yako ni ndogo sana!
    -----------------------------------

    WEWE MWENYEWE HUNA HASARA KWA KUWA UNAKUWA KAMA MNYAMA KWA KUWA HUNA FAIDA YEYOTE UNAYOIRUDISHA KWA WAZAZI WAKO NA WEWE MWENYEWE, ISIPOKUWA TAIFA KWA VIGEZO HIVI:

    1.Unafikiri kazi unaoifanya (KUZALISHA MALI, NA KUTOA HUDUMA) na kupata uwezo wa kula ananufaika nani?

    JIBU: Inanufaika nchi kwa PATO LA TAIFA, usipofanya kazi nani anapata hasara? ...NI NCHI.

    2.Ukifanya makosa kama kutaka kujiua au kuvunja Sheria za Nchi kwa nini unachukuliwa hatua?

    JIBU: unachukuliwa hatua kwa kuwa umeikosea nchi !

    HIVYO ELEWA UJINGA WAKO KWA KUTOKUWAJIBIKA NCHI IKANUFAIKA NI KUWA UNAIGHARIMU NCHI KWA KUWA WEWE MWENYEWE HUNA HASARA NI VILE UNAKUWA NI MZIGO KWA NCHI!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...