Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akifungua rasmi Siku ya Kimataifa ya Kujitolea bila malipo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Disemba ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Volunteer Action Counts’.(Picha na www.dewjiblog.com)
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Bi. Venerose Mtenga akihutubia na kuwaasa vijana kufanya kazi kwa kujitolea bila kusubiri malipo.
Mgeni rasmi amewaasa vijana kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea kwa sababu Serikali kupitia Wizara yake imetenga Bilioni 1.5 kwenye mfuko Maalaum wa Vijana ili kuwakopesha vijana kwenye vikundi vidogo vidogo ili wajiunge na ujasiriamali na kujitoa katika umaskini.
Mshehereshaji wa Siku ya Kimataifa ya kujitolea Austin Makani akijadiliana na washiriki kuhusiana na umuhimu wa vijana kujitolea.
baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali, wanachama wa UN Clubs na wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kujitolea.
Baadhi ya washiriki wakijadiliana umuhimu wa kujitolea katika makundi.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Bi. Venerose Mtenga, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot na Afisa Program wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitole (UNV) Bi. Stella Karegyesa katika picha ya pamoja na washiriki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kutenga mamilioni ya pesa ni jambo moja kwamba pesa hizo ziwafikie walengwa ni habari tofauti kwa walafi wachache ktk kundi la walasimu. Ifike wakati maneno/ahadi viende sambamba na vitendo vya dhati ili kuwakwamua walengwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...