Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa Tiketi ya CHADEMA (aliekuwa amesimamishwa Ubunge),Mh. Godbress Lema akiwasalimia wanachamana na wafuasi wa Chama hicho waliokuwepo ndani ya Mahakama ya Rufaa,jijini Dar es Salaam leo.wakati alipofika kusikiliza Rufaa yake dhidi ya kesi ya Kupinga matokeo ya Uchaguzi dhidi yake iliyofunguliwa na Wanachana wa CCM jijini Arusha.Mh. Lema ameshinda Rufaa hiyo na kufanikiwa kurudishiwa nafasi yake ya Ubunge wa Jimbo la Arusha mjini.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe (katikati) akiwa sambamba na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Godbress Lema (pili kulia) na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari wakiwa ndani ya Mahakama ya Rufaa,jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusikiliza Rufaani ya kupinga matokeo ya Uchaguzi iliyokuwa ikimkabili Mbunge,Godbress leo ambaye ashinda Rufaa hiyo leo.
Wanachama na Wafuasi wa Chadema wakimshangilia Mbunge wao mara baada ya kushira Rufani ya kesi yake ya kupinga matokeo ya Uchaguzi jimbo la Arusha mjili iliyokuwa ikisikilizwa leo kwenye Mahakama ya Rufaa,jijini Dar es salaam.
 Wanachadema wakitembea kwa maandamano kuelekea kwenye ofisi za Chama chao zilizopo Kinondoni jijini Dar.
 Mwanamama huyu ambaye ni Mama ntilie na hakutaka kuwa nyuma kishangilia ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Arusha,Mh. Godbress Lema.
 Pongezi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama,Mh. Wilbrod Slaa.
Katibu Mkuu wa CHADEMA,Mh. Wilbrod Slaa akizungumza na vyombo vya Habari baada ya Ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mh. Godbress Lema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kitu na boksi....Hongera Lema, Hongera Chadema. sasa turudi kazini

    ReplyDelete
  2. Huo ndio ukomo wenu wa juu kabisa Kisiasa!

    Ushindi huo wa Kesi ya Rufaa ya LEMA ndio kama vile mmeshinda Uraisi Uchaguzi Mkuu wa 2015 na ndio uwezo wenu wa mwisho wa pumzi zenu Kisiasa.

    Hapo Mahakamani ni vile Polisi na Mamlaka zimejipanga kisawa sawa hata inzi hawezi kuruka kukatiza, mnaweza KUSHEREHEKEA USHINDI WENU HUO kwa kuanza kukata watu kwa Mapanga!

    ReplyDelete
  3. George MwinamiDecember 21, 2012

    Hongera Mpiganaji Godbless Lema kwa kupambana mpaka kimeeleweka.
    Hongereni pia mawakili wa Godbless Lema;wakili Tundu Lissu, wakili Method Kimomogolo na wakili Mbogolo!Hongereni sana kwa ushindi mkuu dhidi ya hujuma na mahakama zisizohuru za Tanzania!

    ReplyDelete
  4. oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  5. Kumbe haki ipo Tanzania?mbona kila siku nasikia hawa chadomo wanasema haki hakuna na je inakuwaje mtu wa chadomo anashinda kesi hivi hivi?nadhani Jaji na watu wa mahakama hii wafukuzwe kazi,haya tukija upane wa pili nadhani sasa kule mjengoni kwenye Eazy Comedy yule Masanja aliyeondoka anarudi sasa kwa vishindo,Bange oyeee.

    ReplyDelete
  6. Alonifurahisha ni huyo Mama Ntile aloona aache shuhuli zake aoneshe ishara ya vidoel kama alama ya CHADEMA. Watanzania wengi tuna imani na ninyi CHADEMA, tafadhali migogoro yenu inayosababishwa na baadhi ya wanaotaka madaraka malizeni haraka ili tuunganishe nguvu tuikombee hii nchi toka kwa majambazi.

    ReplyDelete
  7. Pamoja na aibu ya mahakama na waamuzi na yote kwa yote yaliyotkea. CHADEMA Mtumie fursa hii ya ushindi huu kwa mara nyingine tena kwa hekima na busara, Ifike mahali muonyeshe tofauti na hao watesi wenu.... kwa kauli na matendo na hasa mara baada ya tukio hili. Bw Lema Arusha waone tofauti ya wakati hukuwepo na wakati huu Unaporejea Vinginevyo itakuwa hovyo tupu na Fedheha na Aibu. Tafadhali msituangushe.

    ReplyDelete
  8. Katika Mikutano na Matukio Mengi Ya Chadema
    Kabwe Zitto Huwa Haonekani sijui ni Kwa nini??

    Naomba Majibu Kidogo

    ReplyDelete
  9. Pongezi zenu lakini mjipange kwa upinzani chanya wenye lengo la kujenga nchi yetu kudumisha amani na umoja.

    ReplyDelete
  10. Mama ntilie muuza chapati,

    Unataka kutuambia CDM imekunufaisha na nini tokea uwe mwanachama?

    Mbona ungali unaendelea na kuungua vidole kwa kuchoma chapati?

    ReplyDelete
  11. Ama kweli Siasa wengi ndio waliwao!

    Wewe mama muuza chapati mama ntilie badala ya kwenda kujiunga na Saccos ili ukope kupanua Biashara yako unajiunga na siasa za Chadema!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...