Maonyesho ya pili ya sekta ya makazi yaani Tanzania Homes Expo yamefikia tamati siku ya Uhuru na kufungwa rasmi na Naibu Waziri ofisi ya makamu wa Rais Charles Kitwanga. Maonyesho ya pili ya Tanzania Homes Expo yalishirikisha mabenki, mashirika yanayouza na kujenga nyumba, mapambo ya nyumba, nishati mbadala, magari, maji, upimaji, viwanja na ujenzi na mengine mengi.
Mkuu wa wilaya ya kinondoni Jordan Rugimbana akipata maelezo toka kwa ofisa wa Shrika la nyumba la Taifa juu ya nyumba zakuuzwa na miradi ya NHC.
Naibu Waziri ofisi ya makamu wa Rais Mh Charles Kitwanga akipata maelezo toka kwa Ng: Nzava na Sizya Fimbo wa African Life.
Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais akimkabithi tuzo Mkurugenzi mtendaji wa Azania Bank Ndugu Charles Singili ambao walidhamini maonyesho ya Tanzania Homes Expo.
Naibu Waziri ofisi ya makamu wa rais Mh Charle Kitwanga akipata maelezo toka kwa muuzaji wa nyumba za sea breeze Ndg: Adamjee. Kushoto ni mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo Zenno Ngowi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...