Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo mchana ametunuku nishani kwa watu kutoka makundi mbalimbali yajamii waliotumikia taifa kwa uadilifu na kutoa mchango wa pekee.Miongoni wa waliotunukiwa nishani leo ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue,Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Eusebia Munuo pamoja na Msanii Mkongwe Bi.Fatma Baraka Khamis(Bi.Kidude).Wengine waliotunikiwa nishani ni pamoja na Watumishi wa umma na askari jeshi na polisi.

Pichani ni Rais Kikwete,akimtunuku Nishani ya Sanaa na Michezo,Bi. Fatma Baraka Khamis (maarufu kwa jina la Kidude) kupitia Baraza katika sherehe za kutunuku nishani mbali mbali katika viwanja vya Ikulu,Jijini Dar es Salaam,ikiwa ni katika kusherehekea maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Bi.Fatma Baraka Khamis(Bi.Kidude) mara baada ya kumtunuku nishani ya Sanaa na Michezo,katika hafla ikiyofanyika mchana wa leo katika Viwanja vya Ikulu,Jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Nishani Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue mara baada ya kumtunuku nishani.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Nishani Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Eusebia Munuo.Picha na Freddy Maro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Inasikitisha sana tena sana na pia ni majonzi yalowaje kuona Jamaa zetu wa serekali ya zanzibar kushindwa kumtunukia Bikidude kwa mchango wake katika kila pembe ya dunia lakini pia nimefurahishwa na Rais kikwete kwa kumkubuka hasa ukiangalia Bikidude ni mpenzi wa Rais kikwete na mama salma

    Mungwana vitendo

    ReplyDelete
  2. Tunakupongeza raisi wetu kwa kutambua michango ya wananchi...na viongozi wengine wa ngazi za chini waige mfano huu, kwa kuwa rais anatambua michango ya kitaifa lakini kuna wengine wanatoa michango mikubwa sana kwa ngazi za mikoa, wilaya n.k. Hata kwenye makampuni yetu ya serikari kuna watu wanajitoa kweli kweli. Ila kwa bahati mbaya nyakati hizi watu wanaojituma kazi kwa ngazi za ki-mashirika ya serikali hawatakiwi, wezi ndio wanatakiwa zaidi. Tuombe Mungu kwa hilo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...