Amiri Jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Uhuri akiwa kwenye gari maalum la Kijeshi na Sambamba na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange walipokuwa wakitoa salamu kwa wananchi na wageni mbali mbali waliofika Uwanjani hapo kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara.Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika maadhimisho Miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara,leo katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Brass Band cha majeshi ya Ulinzi na usalama kikitumbuiza katika maadhimisho hayo.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakipokea salamu za heshima kutoka kwa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi la Usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika maadhimisha hayo,kutoka kulia ni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Mh. Joseph Kabila,Mama Maria Nyerere, Rais wa Msumbiji,Mh. Armando Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada ya kuwasili uwanjani hapo.katikati ni Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda.
Vijana wa chipukizi wakionyesha michezo na ujumbe mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
Kikosi cha wanaanga cha Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikitoa salamu za heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikosi cha ardhini Jeshi la wananchi la Tanzania (JWTZ) kikitoa salamu za heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride la utii na heshima mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.Picha na Full Shangwe Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera Hongera Tanzania!Hongera wananchi kwa maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania."Tumethubutu Tumeweza na Tutaendele Kusonga Mbele". Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  2. mi hata sifahamu si tulisikia Tanganyika imekufa kwani uhuru wa Tanzania bara ni lini tunavojua kulikuwa na uhuru wa Tanganyika maana Tanzania haijazaliwa kipindi hicho.
    Hii inachekesha kitu hakipo bado kinasherehekewa? na Majeshi ya Muungano tena?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...