Watanzania wote Mnaoishi Uingereza, Wales, Scotland na Irelandmnakaribishwa ktk sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania. Sherehe hii itafanyika ukumbi wa The Royal Regency, High street North, Manor Park, London, E12 6TH

Kingilio ni £10 only kabla ya saa 6 usiku, baada ya hapo ni £15.Chakula safi na nyama choma vitakuwepo, pamoja na burudani nzito Live kutoka Jambo Band pamoja na mwimbaji mashuhuri UK 'Francia'.Woote mnakaribishwa kufurahi na kujumuika na watanzania wenzenu kutoka sehemu mbali mbali.Tujivunie nchi yetu, Mungu ibariki TanzaniaAsanteni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ahsanteni sana Watanzania wenzetuu kwa kujali nchi yetu bila uoga. Endeleeni kuitangaza nchi yetu kwa mema na uzuri wake. Hiyo siku basi mpate muda wa kutangaza maeneo yote muhimu ya TZ ya utalii kwa wageni wenu ili wapate muda wa kuja na kujionea na ndio pato letu. Mbarikiwe ila Miaka 51 ya uhuru na siyo 52 kama ilivyoandikwa na mwandishi.

    ReplyDelete
  2. Michuzi ukipewa habari uwe unaangalia vizuri kabla haujarusha, mbona hapo mmeandika miaka 52 wakati ni 51 ya Uhuru. Hayo ndo maoni yangu.
    Ni mimi from Zenj

    ReplyDelete
  3. haya maneno narejea tena kama nilivyoandika katika habari iliyopita "Mimi katika kusoma kote, japo kichwa changu kilikuwa kibovu kwenye historia, lakini sijawahi kusikia Tanzania kama iliwahi kutawaliwa, huu ni upotoshaji wa historia yetu, kwasababu Tanzania imezaliwa mwaka 1964 wakati uhuru ulikuwa 1961...sasa ukisema Uhuru wa Tanzania munamaanisha nini? ninavyojua mie Tanganyika na Zanzibar ndio zilizotawaliwa na kupata uhuru lakini si Tanzania hivi vitu viwili kwa vitatu tofauti.....TUACHENI KUPOTOSHA HISTORIA YETU, tufanyeni kama wanavyofanya wazanzibari, ikifika siku ya mapinduzi wanasherehekea SHEREHE ZA MAPINDUZI YA ZANZIBAR sio MAPINDUZI YA TANZANIA".

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...