Uongozi wa Skylight Entertainment na Skylight Band, unatoa tamko la kulaani kitendo cha watu wachache waovu wenye tabia ya kuvuruga Amani kwenye sehemu za burudani. Tunapenda kuwahikikishia wapenda burudani wa jiji la Dar es Salaam kuwa tutaendelea kutoa burudani mpya na inayokidhi kiu cha muda mrefu cha wapenda burudani katika fani ya muziki wa live.
Aidha tunakemea vitendo vyovyote vya ubabe wa kizamani usio na tija kwa jamii. Tunaamini maeneo ya burudani ni kwaajili ya kukutana, kuburudika, kufahamiana, kuondokana msongo wa mawazo unaotokana na maisha ya kila siku na kutengeneza network na watu mbalimbali kijamii, kikazi na kibinafsi.
Eneo la burudani sio kwaajili ya kuonesha wengine wewe ni nani na una uwezo gani. Tunawaomba wana burudani wote tushirikiane pamoja kuwakemea na kuwafichua, kulaani na kuwatenga wote wanaoashiria vitendo vya uvunjifu wa amani. Tunaendelea kuimarisha ulinzi na kuwahakikishia burudani kwa kwenda mbele.
KaribuThaiVillage kila Ijumaa ujumuike na marafiki na kupata burudani na ladha za kimataifa. Tunawashukuru wapenzi na washabiki wa Skylight kwa kutupokea vizuri ndani ya muda mfupi.
Mungu ibariki Skylight,Mungu IbarikiTanzania.
Imetolewa na
Mkurugenzi Mtendaji
Skylight Entertainment.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. wivu ndo unawasumbua si kingine big up L Ndege bendi yako babukubwa!! haina mpinzani kwa sasa ila jaribu kuweka mambo ya zamani pia ili tuburudike wote

    ReplyDelete
  2. mdumishe na huduma sasa sio mtu anakuja hapo wahudumu wenu wanamwangalia anatafuta kiti na meza ya kukaa mwenyewe na bado baada ya hapo umvizie waiter ndio upate huduma, embu boresheni customer care jamani, kitu kidogo kama hicho kinaweza kikafanya tusihudhurie hapo tena, msijisahau na msisahau kuwa mteja ni mfalme.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...