Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imekuwa ikiwapangia vituo vya kazi wahitimu wa Kada
za Afya tangu mwaka 2005/2006. Katika siku za hivi
karibuni kumekuwepo na Matapeli wanaowarubuni na kuwaibia fedha baadhi
ya waombaji wa kazi kwa lengo la kuwapangia vituo vya kazi vya Uuguzi
na Wahudumu wa Afya.
Wizara inapenda kuwaarifu wananchi hususan wahitimu wa Kada mbalimbli
za Afya kuwa:-
1. Kwa mwaka 2012/2013 Wizara
bado haijapata Kibali cha kuwapangia Vituo vya kazi. Kibali hicho
kitakapotolewa wananchi watatangaziwa utaratibu wa jinsi ya kuomba kupitia Runinga, Magazeti,
Radio na Tovuti ya Wizara (www.moh.go.tz).
2. Wizara itabadili mfumo wake wa utoaji wa barua
za kupangiwa vituo vya kazi ambapo kuanzia sasa waombaji hawatapewa
barua za kupangiwa vituo vya kazi bali majina ya waombaji na vituo walivyopangiwa
yatatolewa kupitia Tovuti ya Wizara (www.moh.go.tz) na wahusika watatakiwa kwenda kuripoti katika vituo
walivyopangiwa baada ya kuona majina yao kupitia mtandao.
3. Upangaji wa vituo vya kazi hauwagharimu fedha yoyote. Hivyo, waombaji wote msitoe
fedha yoyote kwa ajili ya ahadi kuwa utapata ajira na mnatakiwa kuwa
makini na matapeli hao.
Regina L. Kikuli
KAIMU KATIBU MKUU
03 DESEMBA, 2012
Du kama ni hivi basi tulipofikia sasa si pazuri tena na nadhani huko tunakokwenda kwa spidi hii mambo ndio yatakua mabaya zaidi.
ReplyDelete