Tamthilia mpya kabisa ya Televisheni kutoka kwa Watu wa Marekani! Onyesho la Kwanza la SIRI YA MTUNGI litakuwa ITV saa 3.30 usiku tarehe 9 Desemba. Na EATV saa 3.30 usiku tarehe 12 Desemba.

Mchanganyiko mzuri wa wahusika wa Siri ya Mtungi, waliohusiana kwa damu au ndoa, au kwa mapenzi tu, unaunda jamii inayohamasishwa na penzi, lililoletwa na woga, ushirikina na usaliti, ikinyanyuliwa na ucheshi na furaha, na kupewa nguvu ya mshikamano wa ndani wa familia na urafiki.

Tamthilia hii ya Televisheni ni Programu ya awali ya TCCP (Tanzania Communications Capacity Project) iliyotekelezwa na JHU-­‐CCP (Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communications Programs) kwa msaada wa USAID (United States Agency for International Development) na kama sehemu ya PEPFAR (US President’s Emergency Fund for AIDS Relief).

Ikiwa imetayarishwa na MFDI (Media For Development International), Siri ya Mtungi inawaleta pamoja Wasanii bora wa Tanzania, waandishi, wana mitindo ya nguo, wakurugenzi wa sanaa, waigizaji na watendaji wa filamu kwenye mafanikio makubwa ya ukuaji wa tasnia ya filamu na televisheni Tanzania.

Kati ya mitaa yenye harakati nyingi ya Dar es Salaam na ile iliyo kimya ya Bagamoyo, tunapenya nyuma ya milango iliyofungwa mpaka kwenye maisha ya Cheche na mkewe Cheusi, binti wa kiongozi maarufu katika jamii, mwenye wake wengi, Mzee Kizito, pamoja na wahusika wengine kama Duma, mwana DJ; Lulu-­‐ shangingi lililokubuhu; Farida-­‐ roho ya nyoka; Masharubu-­‐ mzee kikwekwe na wengine wengi.

RATIBA YA ITV: Jumapili 3.30 usiku -­‐ Jumatano 3.30 usiku
 RATIBA YA EATV: Jumatano 10.30 Alasiri -­‐ Alhamisi 7.00 Mchana -­‐ Jumamosi 10.30 Alasiri

Mtengenezaji wa Tamthilia hiyo ya Siri ya Mtungi,John Riber akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi Tamthilia hiyo itakayokuwa ikirushwa na kipindi cha Televisheni cha ITV.
Baadhi ya washiriki wa Tamthilia hiyo wakiwa kwenye picha ya Pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. tunaisubiri kwa hamu,bila shaka itakuwa tamthilia nzuri,itakayo fungua ukurasa mpya wa tamthilia zenye ubora wa kimataifa!hongera sana washiriki wote kwa hilo!karibuni!

    ReplyDelete
  2. Hongera!Tusonge mbele tuwache viogonzi wano tumia ukabila na uchawi kula vidole vya ALBINO, wa endlea kutawala nchi. Mimi sina husiano na Iran.Kama ni dini yangu basi makosa ni Mungu. Rais Kikwete ndiyo ana husiano na Iran. Asitumie dini na ukabila na chuki. Atashindwa kushindana na Mungu.Hiyo ni ushindi wa temporary tu. Mungu nidyo ana ushindi wa melele.Wana fikiri uchawi ndiyo kila kitu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...