Mgeni rasmi Dk. Hassan Mshinda, akitoa hotuba ya ufunguzi wa  Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha waandishi wa habari za Sayansi nchini (Kulia) ni Meneja Mkuu wa Biashara na uwakala wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kilala Sendama.
 Mgeni rasmi Dk. Mshinda, mwenye shati la kiafrika, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TASJA.
 Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake David Ramadhan (tatu shoto) akimkabidhi Katibu Mkuu mpya wa TASJA, Benard Lugongo, wanashuhudia ni baadhi ya viongozi waliochaguliwa.
Viongozi wapya wa TASJA wakiwa katika picha ya pamoja waliokaa kulia ni Mwenyekiti mpya Greyson Mutembei na Katibu Mkuu wake Benard Lugongo wakiwa na baadhi ya wajumbe wapya wa kamati ya utendaji.


CHAMA cha Waandishi wa habari za Sayansi nchini (TASJA), kimepata viongozi wapya watakiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
 Waliochaguliwa ni Pamoja na Greyson Mutembei, ambaye ni Mwenyekiti mpya, Bakari Kimwanga Makamu Mwenyekiti, Benard Lugongo Katibu Mkuu na Nasra Abdallah Mweka hazina.

Mbali mkutano huo umewachagua wajumbe wa kamati ya uttendaji ambao ni David Ramadhan, Asia Rweymamu, Gabriel Mushi, Restusta James, Jackob Nduye na Hamis Shimye.
 Awali akifungua mkutano Mkuu  huo wa mwaka, mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Hassan Mshinda, alisema ili nchi iweze kuendelea inahitaji wanasansi na wabuni wengi ambao wataleta maendeleo nchini. 
“Tunajua TASJA kwa namna mlivyo mnaweza mkawa chachu ya maendeleo katika sekta ya Sayansi nchini, nasi kama wadau wakuu tunaamini waandishi wa habari mna mchango mkubwa katika wakuelimisha wananchi. 
“Ahadi yangu kwenu TASJA kupitia COSTECH mnafika mbali sambamba na kuwaunganisha na taasisi zingine kimataifa,” alisema Dk. Mshinda 
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Biashara na uwakala wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kilala Sendama, alisema kuwa hivi Maendeleo ya teknolojia za mawasiliano yamejkuwa yakichukua nafasi kubwa katika maendeleo ya Taifa.
 “Kwetu TPC tumejiandaa katika kutoa huduma zatu ikiwemo EMS, Post Cargo na Inateranet ambayo imekuwa ikitumiwa na watanzania wetu nanyi TASJA ni moja ya wadau wetu,”alisema


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...