Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),David Mgwassa akisungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kinywaji kipya kinachoitwa ZANZI (kinachoonekana pichani) iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam leo.
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),Joseph Chibehe akitoa ufafanuzi wa Kinywaji hicho kipya aina ya ZANZI ambacho kinapatikana katika ujazo wa 750ml na katika Pakiti zenye ujazo wa 100ml ambacho kitakuwa kikipatikana nchi nzima.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya TDL,David Mgwassa na kulia ni Meneja Usafirishaji wa TDL,Bavon Ndumbati.
 "...hiki ndicho kinywaji kipya tulichokizindua leo..." 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),David Mgwassa (katikati),Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),Joseph Chibehe na Meneja Usafirishaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL),Bavon Ndumbati wote kwa pamoja wakigonganisha glass kuashiria uzinduzi rasmi wa kinywaji hicho uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam.a

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

 1. At Zanzibari twanywa tembo na sie?,,,au huu ndo ule Muungano?

  ReplyDelete
 2. Zanzi,,,,

  Hiki ni kinywaji maalum kwa Polisi Zenji kunywa ili wapate nguvu ya kuchapa mikanda na marungu kukabiliana na Kundi la Uamsho na wapinga Muungano!

  ReplyDelete
 3. Mbona hamjesema kinywaji cha moto au baridi? alcoholic or non-alcoholic?

  ReplyDelete
 4. TDL.

  Kwa nini mfikie kutupatia toleo la KONYAGI-C (Zanzi), baada ya KONYAGI-A(original mikono juu), huku mkijua kuna wale akina mama kule Kigogo Mbuyuni,Keko Magurumbasi na Musoma na Tarime Mkoani Mara wanazalisha kiwango kizuri ch KONYAGI-B mngewafikiria kwanza hawa kuwaingiza ktk uzalishaji wa Taifa kupitia KONYAGI-A kabla hamjafikia KONYAGI-C (zanzi)!!!

  ReplyDelete
 5. You guys, no mention on alcohol content at all?

  ReplyDelete
 6. Hongera TDL kweli mlistahili tuzo ya Mzalishaji bora aw mwaka

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...