Mahmoud Ahmad Arusha

Baadhi ya Abiria wanaosafiri na mabasi kwenda mikoani wameitaka mamlaka ya usafirishaji majini na nchi kavu Sumatra kuangalia wezekano wa kuwa na ukaguzi wa mara kwa mara kwenye mabasi yatokayo mikoani kwani kumekuwa na ukiukwaji wa sheria za usafirishaji mara kwa mara na Abiria kuendelea kupata matatizo wawapo safarini.

Hayo yamezungumzwa wakati abiria hao wakisafiri kutoka singida kuelekea Wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro kwenye basi la Mtei Coach na kumtaka kondakta kuelezea Tiketi ya Arusha mwisho wake wapi?kwani abiria anayetoka singida hadi usa river je anatakiwa kulipa nauli hadi usa au la.

Tukio hilo limetokea wakati mwandishi aliposafiri na basi hilo kutoka Stand kuu kuelekea Usa River kwani ndani ya basi alikuwepo abiria na familia yake waliokuwa wanasafiri kutoka Singida hadi usa River na kutakiwa kusimama ili kuwapisha Abiria wengine kwani tiketi yake iliangikwa singida Arusha.

Taarifa zinadai kumekuwapo na changamoto mbali mbali kwenye usafiri wa Mabasi ya mikoani kwa abiria kukosa masaada pindi yanapojitokeza matukio ya ukiukwaji wa sheria za usafirishaji huku mamlaka husika ikijitokeza kwenye wakati wa siku za mwisho wa mwaka hadi pale wanapopelekewa taarifa ndipo hustuka na kuja njiani na kutakiwa kuacha ofisi zao kuja kushughulikia kero mbali mbali za Abiria.

Abiria hao wakamtaka waziri wa uchukuzi kuliangalia suala hilo kwa ukaribu kwani matatizo wayapatayo ni makubwa zaidi ya ukaguzi wa nauli pekee huku wengine wakiwa hawajapewa tiketi za kuonyesha wanasafiri hadi wapi haya yamekuwa ni matatizo ya kawaida kwa abiria wengi wasafirio kwenye baadhi ya mikoa hiyo ya kanda ya kaskazini.

“Utakuta wakati mwingine unasafiri kutoka sehemu Fulani kwenda sehemu nyingine unapitishwa kituo na unapohoji unaambiwa umelala hivyo unashushwa sehemu nyingine kama huna fedha nyingine unafanyaje”alihoji Fadhill Kibwana makazi wa jiji la Arusha.

Fadhili alienda mbali kwa kuzitaka mamlaka husika ikiwemo jeshi la polisi kuwa makini na madereva na makondakta wa mabasi ya Abiria hapa jijini kwani wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya kinyama kwa kuwapandishia nauili wakati wa jioni wanaporudi majumbani kwao wakati wanapotoka kwenye mihangaiko tyao ya kujipatia ridhiki zao za kila siku.

“Nauli ya Usa River ambayo kihalali ni sh.500 inageuka sh,1000 huku wahusika wakiyafumbia macho bila ya kuchukuliwa hatua sehemu mbali mbali huko vijijini wananchi wamekuwa wakipata taabu bila ya msaada utakuta mahali pa nauli ya 500 inatozwa hadi 2500 huu sasa ni wizi wa mchana kweupe”alisema Hadija Kichwa mkazi wa Magugu mkoani manyara.

Matatizo ya usafiri kwenye mikoa mbali mbali hapa nchini yamekuwa kero kwa wananchi hasa wa vijijini kwani imeonekana kuwa wananchi hao wamesahauliwa huku wakizitaka mamlaka husika kwenda huko kila mara ili waweze kupata haki zao za msingi ikiwemo hiyo ya usafiri.

Uchunguzi uliofanywa na Gazeti hili unaonyesha matatizo yamekuwa mengi kwa wasafirisha abiria humu nchini na zaidi kwenye vijiji huku wamiliki hao wakikiuka nauli halali za abiria kwa kuwatoza nauli hadi 65% ya nauli halali kwa kilometa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. UKITAKA KUJIONEA MENGI KULIKO HAYA ULIYOANDIKA AU KUHOJI WATU WA SINGIDA PANDA MABASI YA TABORA-DAR ES SALAAM, HASA MABASI YA NBS.
    Katika mabasi abiria anaruhusiwa kubeba kilo 20 za mizigo lakini tafsiri ya kwao kwa mzigo ni BEGI la Nguo tu. ukiweka mzigo wa aina nyingine lazima ulipie mzigo huo kwa kilo ambayo kwa bei waliyojipangia wao ni shilingi 1000 hadi 1500. hata kama utakuwa umechukua LITA 5 za Asali wao kwao ni lazima ulipie.
    Pia katika mabasi haya suala la abiria kusimama njiani ili kunywa chai ni mwiko wao chakula wanacho kijua ni WALI wa kwa MWARABU mwenzao DODOMA iwe unatoka TBR au DSM chakula ni DOM tu, ukizingatia kuwa MABASI yao huondoka saa 12 Asubuhi katika vituo vyote vya mwanzo. huu kama si unyanyasaji nini?
    Hata hivyo, SUALA LA KUJAZA ABIRIA kwa mabasi haya kwao ni kitu cha kawaida hasa basi likitoka DAR likifika DOM utaanza kuona mabadiliko toka Basi la MKOA kwa MKOA kuwa DALADALA,Wenyewe husema wanajazia .
    Lugha za wafanyakazi nazo ni kama vile mtu na Mtumwa wake na mengineyo mengi tu yasiyo pendeza kwa abiria

    ReplyDelete
  2. Hemed -Star consultJanuary 30, 2013

    NInavyojua mie nauli kama imeandikwa shs 20,000/= hadi Arusha basi ni sehemu yoyote ya Mkoa wa Arusha ambayo abiria atashuka. na Mzigo wa kilo 20 haulipiwi hadi uzidi hapo na kila kilo inayozidi ina kiwango cha ke cha kulipiwa.

    naomba mr Mzirai au Shiro mtujuze.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...