Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kokonko Bwa.Peter Toima (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibondo/Kokonko Bwa.Juma  Magango (shoto) na baadhi ya Wanachi wakielekea kukagua  Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.




Wakielekea kukagua ujenzi wa mradi wa darja la pamoja.
Pichani ni  Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.

Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.

Mradi huo unaotarajiwa kukamilika februari 20,2013 utagharimu kiasi cha shilingi 260,000,000/=,aidha imeelezwa kuwa mradi huo utatekelezwa kwa awamu nne,awamu ya kwanza imeshaanza ambayo unahusisha ujenzi wa daraja,barabara KM1 inayotoka kwenye soko hadi darajani na hifadhi ya Mazingira,utekelezaji wa awamu ya kwanza umefikia 70% mpaka sasa.
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na  Msimamizi wa Mradi kanda ya Umwagiliaji kutoka Mkoani Tabora,Alfred Swai alipokwenda kukagua mradi  wa ujenzi wa  daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi.
Msimamizi wa Mradi kanda ya Umwagiliaji kutoka Mkoani Tabora,Alfred Swai akitoa ufafanuzi mbele ya Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana kuhusiana na ujenzi wa Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.


Jengo la Soko la Pamoja lililokaguliwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mapema leo jioni,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi.Picha na habari zaidi bofya JIACHIE BLOG.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tunaposema chama kinaunda serikali maana yake shughuli zote za kiutendaji zitaongozwa kwa ilani ya chama kilichoshinda kwa kuunda serikali ambayo kinaamini kwamba ilani itatekelezwA na report ya utekelezaji itatolewa kupoitia vikao vya chama na ndio maana kuna wakuu wa mikoa na wilaya ambao wote ni mawakala wa CCM kuhakikisha ilani ya chama inatekelezwa. NINA MASHAKA NA HUU UTARATIBU MPYA WA CCM WA KWENDA KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA KUTOA MATAMKO MAKALI WAKATI TAYARI WALISHAUNDA SERIKALI NA WALITAKIWA WAHOJI SERIKALI KUPITIA VIKAO VYAO. (hapo wanasumbua watendaji wa serikali na nahisi wengi wao wanawapokea na kutoa maelezo huku hawapendezwi pia sidhani kama ni sahihi)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...