THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MCHUNGAJI AACHANA NA MKEWE KWA KUMTUHUMU NI MCHAWI MBEYA

Mchungaji wa kanisa linalojulikana kwa jina la Calnel Centre Mchungaji Elia Ambakisye Jongo alijikuta katika mzozo mkali na aliyedai kuwa ni mke wake baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi.
Sabina Lameck mke wa mchungaji anaedaiwa kuachwa sababu ya uchawi 
Katikati mama mzazi wa mchungaji Elia Jongo wakiwa katika kikao hicho
Baadhi ya wazee wa kanisa wakiwa makini kusikiliza kisa hicho
“ Ninachotaka ni huyu mwanamke kurudisha nguo zangu kwa sababu alizichukua ili apeleke kwa mganga kwa nia ya kunisaidia mimi nirudiane na mchungaji lakini badala yake naona dawa hizo zimemsaidia mwenyewe hadi anataka kuolewa yeye,” alisema Mwanamke huyo. ambaye alikuwa mke wa mchungaji Elia
Huyu ndiye muumini wa kanisa hilo anayedaiwa kutaka kuolewa na mchungaji Elia pia muumini huyu ni mzee wa kanisa hilo
Mchungaji Elia na dada yake wakiwa makini kumsikiliza mchawi wake
“ Huyu mwanamke ni mshirikina maana tangu tutengane alianza kunivurugia huduma ambapo waumini walianza kupungua kanisani na yeye kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kunivurugia huduma” alisema mchungaji huyo kwa hasira.
Askofu wa kanisha hilo Pasta Lugito 
 Hili ndilo kanisa la Calnel Centre mbeya lipo katibu na kiwanja cha ndege Mwanjelwa  Mchungaji wa kanisa linalojulikana kwa jina la Calnel Centre Mchungaji Elia Ambakisye Jongo alijikuta katika mzozo mkali na aliyedai kuwa ni mke wake baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi.
Tukio hilo la aina yake lilitokea  katika kanisa hilo lililopo Airport Jijijini Mbeya baada ya Mchungaji huyo kupokea ujumbe mfupi katika simu yake ya mkononi kutoka kwa Mwanamke anayedai alikutwa mke wake ambaye waliachana miaka mine iliyopita.
Mchungaji huyo akiwa mbele ya wazee wa kanisa, Familia yake, waumini pamoja na wanahabari alisema sababu ya kuwakusanya watu hao kumetokana na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Sabina Lameck akitaka kutubu kwa mabaya aliyomtendea mumewe.
Hata hivyo baada ya mwanamke huyo kupewa nafasi ya kuanza kujieleza alianza kumtuhumu muumini wa kanisa hilo kuwa anauhusiano na mchungaji ambaye ni mumewe wa ndoa ambapo pia alidai kuwa mwanamke huyo alichukua nguo za mchungaji na mkewe kwa madai ya kupeleka kwa mganga ili kusudi awasaidie warudiane.
“ Ninachotaka ni huyu mwanamke kurudisha nguo zangu kwa sababu alizichukua ili apeleke kwa mganga kwa nia ya kunisaidia mimi nirudiane na mchungaji lakini badala yake naona dawa hizo zimemsaidia mwenyewe hadi anataka kuolewa yeye,” alisema Mwanamke huyo.
Kwa upande wake mchungaji Jongo alimtuhumu mwanamke huyo kuwa ni mshirikina na kwamba sababu ya kutengana naye ni kutokana na mwanamke huyo kuzaa na mwanaume mwingine nje ya ndoa hali aliyosema alidhalilishwa kama mchungaji.
“ Huyu mwanamke ni mshirikina maana tangu tutengane alianza kunivurugia huduma ambapo waumini walianza kupungua kanisani na yeye kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kunivurugia huduma” alisema mchungaji huyo na kuongeza.
“ amekuja leo hapa baada ya kusikia mimi nataka kuoa muumini wangu ambapo yeye ameanza kumzushia kuwa ni mshirikiana kitu ambacho si cha kweli lakini kama kuna ukweli wowote utajulikana kwa sababu Mungu yupo,” alisisitiza Mchungaji huyo.
Hata hivyo usuluhishi huo haukufika mwafaka baada ya kuibuka kwa malumbano hali iliyomlazimu msimamizi wa usuluhisho huo Askofu wa kanisha hilo laiyejulikana kwa jina moja la Pasta Lugito kuahirsha mazungumzo hayo huku wakimpiga marufuku mwanamke huyo kukanyaga katika makazi ya mchungaji.


Kuna Maoni 22 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Heheh, "huduma ya ibada inavurugwa kwa uganga"

  Huu uchuro sasa.

 2. Anonymous Anasema:

  very so sad.

 3. Anonymous Anasema:

  Hivi matukio haya ya ajabu ajabu kwanini yanatokea sana Mbeya???

  Kuchuna ngozi, baba kulala na mtoto wake, wachungaji kuchawi..

  Mbeya kuna ushirikina mwingi au ni habari zao zinajulikana zaidi?

 4. Anonymous Anasema:

  HII INAWEZEKANA MBEYA TU,

  MBONA BIBI HARUSI MTARAJIWA "MZEE" WA KANISA ANAONEKANA KIJANA SANA?

 5. Anonymous Anasema:

  Nani mwenye nguvu Mungu au Mganga. Wewe mchungaji sisi waumini wa kanisa lako tuamini nini?
  Ulitakiwa umshinde shetani kwa nguvu za bwana. Sasa unamuogopa mganga.
  SHAME na wewe ni shirikina tu!!!!!!!!

 6. Anonymous Anasema:

  huyu mchungaji commitment ZERO

 7. Anonymous Anasema:

  Sasa inakuwaje mchungaji anashiriki katika imani za kishirikina? Hii sijaipenda kabisa kwa kweli

 8. Anonymous Anasema:

  Kama Biblia inasema ndoa ya kikristu ni mke mmoja mume mmoja, hakuna talaka.............. hapo mchungaji ametumia kifungu gani.
  WAKATI MWINGINE NAKUBALI WAKATOLIKI WALIONA MBALI, HAWA WACHUNGAJI HAWATUPI MIFANO BORA YA NDOA... NA WAANDISHI ALIWAITA ILI DUNIA IJUE KUWA MKEWE NI MCHAWI... JE SI ANGEMPIGA MAOMBI YA UPAKO UCHAWI UTOKE?

 9. Anonymous Anasema:

  Dunia inakoelekea siko jamani, kwa ufahamu wangu mdogo wa mambo ya Mungu kama mtu ni mshirikina wewe mwenye nguvu ya Mungu utaonyeshwa na kuomba ili huyo mtu ashindwe kukufanyia ubaya na sio kusemana hadi vikaoni. Mchungaji kwa hekima angeliombea kwa kuwashirikisha watumishi wachache na hatimaye lingeisha na sio vikao hadi watanzania wote tunajua. Nina mashaka na uchungaji wake cause hata jengo la kanisa linatia mashaka, wote watubu na kuanza upya.

 10. Anonymous Anasema:

  Mungu wangu weee.. haya makanisa yalivyokuwa siku hizi....Utotoni nilifundishwa kuwa Yesu ni kiboko ya wachawi wote na Mchungaji anayetumiwa na Mungu hawezi kutetemeshwa na nguvu za giza(wachawi na waganga) lakini siku hizi hawa wachungaji ndo wao tunawasikia ktk kuendekeza ndumba. Bwana asifiwe sana.. Bring back the good old evangelical churches.

 11. Anonymous Anasema:

  hizo ndio athari za nyumba ndogo,badilisheni sheria mruhusiwe kuoa mke zaidi ya mmoja...haisaidii kusingizia uchawi...kinachonekana ni mchungaji kamtelekeza mke wa kwanza sababu ya kitu kimpya wanachokutana ktk uzee wa kanisa.

 12. Anonymous Anasema:

  Mbombo ngafu...

 13. Anonymous Anasema:

  Hizi ni dalili za siku za mwisho. Na hapa tunaona kwamba maandiko yanatimia. Jamani tutubu. Mungu na aturehemu. "Mchungaji" umetia aibu kweli kweli. Jamani haya mambo yanaonyesha ni vipi huyu Mchg hamjui yule anayemtumikia, yeye ni Mungu mkuu na wala hashindwi na uchawi, sasa wewe Kiongozi wa kanisa kama unamwogopa mchawi, utawasaidia vipi waumini wako? Bwana Yesu tusaidie!!!

 14. Anonymous Anasema:

  Jamani kweli nami naungana na wachangiaji wa hapo juu kwamba tunaishi siku za mwisho na karbu YESU anakuja kuhuku watu maana ni aibu kubwa eti mchungaji anavunja ndoa yake kwa sababu ya mke mshirikina?
  Mchungaji kumbuka kiapo kwamba ulisema hutaachana na mama huyo kwa namna yeyote ile mpaka mauti itakapowatenganisha.
  Sasa je umekufa? Unataka kuacha mke kwa kisingizio cha ushirikina?
  Uliomba na kufunga kwasababu ya tatizo la mkeo?
  We mchungaji gani unayeogopa ushirikina unahubiri nini sasa?
  Wwe sema una agenda ya siri unataka kabinti hako eti kamzee wa kanisa?
  Naungana na wenzangu kwamba WOTE MMENGAUKA NA MKATUBU NA MREJEE KWA YESU
  MCHUNGAJI UKABATIZWE UPYA NA MAMA MCHAWI NA HUYOANAYETAKA KUOLEWA
  AHENI VIKAO VYA KIPUMBAVU

 15. Anonymous Anasema:

  Da. tatizo la hawa jamaa, wakristo,madhehebu yamezidi sas, kila mtu ananzisha kanisa lake, na kujita mchungaji, hata, shule ya uchungaji hana, akiweka matulubai basi, kanisa hilo. hata mimi ni mkristo lakini naion, hii haijakaa sawa, makanisa kila kukicha, serkali idhibit haya makanisa holela,, angalia sasa hapo, jamii inajifunza nini?

 16. Anonymous Anasema:

  Eheee Mchungaji,

  Hapo penye nguvu za kiza si ndio pa kuonyesha uwezo wako Kiimani sasa?

 17. Anonymous Anasema:

  Mchungaji acha Usanii!

  Mwogope Mwenyezi,

  Kwa nini usiseme ya kuwa mwanamke anayeitwa Mzee wa Kanisa unayetaka kumuoa analipa?

  Ni wazi umemuona Mwanamke Mzee wa Kanisa ni mzuri zaidi ya mkeo,

  Na ni kuwa umemtafutia sababu mkeo kumwacha ili uwe huru Kumuoa yeye!

 18. Anonymous Anasema:

  Wewe, wewe, wewe Mchungaji Jongo sema tu ya kuwa umetaka kubadilisha ladha na umetaka 'kuosha jando' tu na ndio nia yako haswa!!!

 19. Anonymous Anasema:

  Jamani mmeona Wachungaji Vibwetere walivyokuwa wengi kwa sasa?

 20. Anonymous Anasema:

  Lohhh Mchungaji unamsaliti Mkeo halali kwa Mipango namna hiyo?

  Ya nini tabu yote hiyo?

  Kweli umeshuka kiimani 'UKATEMA BIG-G KWA KARANGA ZA KUONJESHWA'?

  Si ungehamia kwenye Imani zingine zinazoruhusu Mke zaidi ya mmoja?

 21. Anonymous Anasema:

  Mchungaji umewakatisha tamaa Waumini wengi sana!

  Si ungetumia mwamko wa Kiimani ili kukabiliana na Uchawi huo?

 22. Anonymous Anasema:

  Habari hii inafaa iende kwenye 'magazeti-pendwa'