Ofisi ya Bunge inapenda kuwataarifu Wanahabari wote kuwa Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vitaanza kukutana hapa jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu 14 Januari 2013, kabla ya Mkutano wa 10 wa Bunge unaotarajiwa kuanza Mjini Dodoma siku ya Jumanne Januari 29, 2013. 

Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, Kamati hizi hukutana angalau majuma mawili kabla ya Vikao vya Bunge, ili kupitia Taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Shughuli za Serikali na Taasisi na Idara zake, ikiwa ni pamoja na kupitia miswada inayotarajiwa kuletwa Bungeni. 

Aidha baadhi ya Kamati zitajihusisha na kufanya Ziara za Ukaguzi katika Sehemu mbalimbali nchini kwa mujibu wa Kanuni ya 114 (1- 5) kama Ratiba inavyojionesha katika kiambatanisho BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...