THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

viwanja vinauzwa.

Viwanja vinauzwa,vimepimwa na vina hati,vipo eneo la Viwanda Mwanambaya Mkuranga barabarani na vimezingatia hifadhi ya barabara,vimepakana na kiwanda cha Cement,kiwanda cha Gypsum na Yad ya Scania used,Heka 4 bei yake ni sh mil.700,zipo heka 28 nyuma ya hicho mil 700,zipo heka 4 zinapakana na ukuta wa kiwanda cha Cement Mil.600.

Zipo heka 6 hazijapimwa zipo barabarani  eneo hilo hilo mil 500. Mwandenga  zipo heka 67 Mil. 700,Zipo nyumba eneo la Gerezani  kariakoo Mil. 700 kwa Mil.900,Round about ya Kariakoo bilioni 1 na 200 milioni.Kariakoo stendi ya Kawe ni bilioni 1 na 200 mil. Ipo beach gezaulole Kigamboni Mil.600,pia vipo viwannja vya Mil.10 na vilivyopimwa kwa mil 25 Gezaulole-Kigamboni.

Kwa mawasiliano piga namba 0652020343


Kuna Maoni 12 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Hivi zile bei elekezi za viwanja bado hazijaanza kutoka?

 2. Anonymous Anasema:

  duh.. !! hata newyork vipo vya rahisi zaidi ya hapo.

 3. Mkweli Anasema:

  Kwa muondoko huu, Nani mzalendo asiye fisadi atamudu kumiliki ardhi??? Ya Zimbabwe ya ardhi yatakuja Tanzania.

 4. Anonymous Anasema:

  Mbona Watanzania vichwa vigumu sana kuelewa mambo?Hivi Mwalimu Nyerere tumemtupa wapi?Angekuwa hivyo wakati wa Uongozi wake,nchi hii ingekalika kweli?Masikini wangekuwa na sauti yoyote katika maamuzi ya nchi yao?Ardhi ni "Godgiven natural resource",ni zawadi kutoka kwa mwenyezi Mungu,muumba wa vyote kwa viumbe wake wote!Kila binadamu ana haki ya asili,ya kuzaliwa,kumiliki eneo kwa ajili ya maisha yake.Kama vile vile ambavyo huwezi kuuza "Hewa(Oxygen)",au "Maji(watersource)","Mwanga/Jua(light)",na rasilimali adimu na adhimu za aina hiyo,ambazo ni Mungu pekee aliye na uwezo wa kuzifanya ziwepo na zisiwepo,na kuhatarisha uhai wa viumbe wengine!Hivi karibuni tu,lilitoka Tamko la Serikali kupitia kwa Waziri wake,kwamba,Serikali muda si mrefu itatoa "Bei Elekezi"kwa ardhi yote nchini,ili kuziba mianya ya aina hiyo yenye kila dalili ya "Ushetani" wa kuabudu Pesa na Utajiri wa haraka haraka bila kuutolea jasho,isipokuwa kuwahi tu eneo la tukio!Kupitia Blog hii iliyotukuka,napeleka Ujumbe kwa Waziri Mhusika na Ardhi nchini,kwa maana hiyo,napeleka kilio changu serikalini,na kutarajia kwamba Rais wetu atausoma ujumbe huu,kwamba,"Asitishe mara moja"zoezi lolote hapa nchini,popote pale,la "Kuuza Ardhi" kwa mtindo huu wa "kidalali",hadi hapo Serikali itakapo toa Tamko Rasmi kuhusu biashara hiyo.Huu ni "Wizi na si Vinginevyo"!Mwenye Uwezo wa kununua Kiwanja kwa bei hiyo ys shs.milioni 700 na zaidi,Takukuru wafanye kazi yao,ili kubaini fedha hizo zimetokana na vyanzo gani,lakini,zisiwe Kodi za Walalahoi!Jamani,muda unakwenda kasi,mambo haya yasiachiwe yaote mizizi hapa nchini!waiting to see govt'ments' response! du!hapana,sasa nchi imefika pabaya!Mwisho wake,tutaanza kuuziwa hata Makaburi ya kuzika ndugu zetu!Serikali iko wapi,mmelala fofofo!....(to....y)

 5. Anonymous Anasema:

  ...viwanja karibu na kiwanda cha cement na gypsum hilo ni eneo la makazi au la viwanda...?

 6. Anonymous Anasema:

  Duhhhhh!!!!! Hivi hawa watu wanayajua maisha ya watanzania wa kawaida kweli? au hizi bei ni kwa ajili ya mafisadi tu??

 7. Anonymous Anasema:

  Yeye anaeuza katumia vigezo gani kufikia hizo bei za bilion moja, na kodi yake vipi nani analipa!?

 8. Anonymous Anasema:

  Hivi kweli tutamiliki mali kweli kwa bei kama hizi? Hii si kutaka wasionacho/masikini watumie mtaji wao kuweza na wao kumiliki vitu vya bei kama hizi??

 9. Anonymous Anasema:

  wandegereko waende wapi? moshi? au Mtwara, kama gesi inakataliwa wananchi vilevile wangekataa nchi kuuzwa kama hivi. Huu ni wizi. Mtanzania gani mwenye uwezo wa kununua kiwanja bei kama. Anaeuza viwanja hivyo, ni serikali au Knightsupport. Tumekwisha watanzania.

 10. Anonymous Anasema:

  Nichagueni kuwa rais....nina ahidi kuondoa ufisadi tanganyika na zanzibar


  Nagombea 2015...kauli mbiu ni. ..bongo si new york...ukisikia hiyo pigA kura kwangu

 11. Anonymous Anasema:

  Kwa bei hizo nanunua nyumba Mayfair London na wala siyo kiwanja. Hii inaonyesha ni jinsi gani tunaishi ktk nchi ambayo hakuna regulation ya kitu chochote, kuanzia hospitals, shule hadi sasa ardhi. Kwanini watu wauze ardhi kwa bei hizo. ktk nchi masikini kama hii wanamuulizia nani kama hawataki kujenga system ya capitalism ktk nchi masikini. I think wee need to discuss about moral issues here!

 12. Anonymous Anasema:

  Poleni ndugu mnaozisikia leo bei za hivi viwanja.
  Hii ndiyo Tanzania.
  Hapo bado hujampa huyo dalali 10% yake. Uzalendo bado Tanzania hicho ndicho kinatuuua hata wakipanga bei haitasaidia nataka utachukua hutaki nenda kwa mpanga bei akakupe chakwake.