Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (katikati) akipitia kumbukumbu wakati akiongoza kikao cha Wadau cha maandalizi ya Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Oman unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 24 na 25 Februari, 2013. Wengine katika picha ni Balozi Bertha Semu-Somi (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bw. Elibariki Maleko, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Mashariki ya Kati.
Baadhi ya wadau waliohudhuria kikao hicho wakimsikiliza mwenyekiti (hayupo pichani)
Wadau wengine wakati wa kikao hicho.
Picha na Rosemary Malale

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ni hatua ya muhimu sana kukaa Kikao na Oman ili kudumisha Muungano na kuijenga 'Jamhuri ya Muungano wa Tanzania'!

    ReplyDelete
  2. Wewe mdau wa mwanzo hapo juu, kikao cha TZ na Oman kina uhusiano gani na muungano wa Tanzania?. Kwani Oman imekuwa Zanzibar?.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Pili Zanzibar iliwahi kutawaliwa na Oman, pia inasemekana hao Mabwenyenye wanaochochea Muungano kuvunjika wana Uraia wa Oman lakini sio Maafisa wa Serikali ya Oman!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...