THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika - NECTA


Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limesema  matokeo ya kidato cha nne bado hayajakamilika na kuwa habari zilizozagaa wiki hii kuwa yapo tayari si za kweli.


Hata hivyo Baraza hilo limebainisha kuwa licha ya kutokamilika, matokeo hayo yanakaribia kutoka kwa mujibu wa  ratiba za baraza hilo ambapo hutakiwa kutoa matokeo hayo mwezi Februari. Ofisa Habari na Mawasiliano wa NECTA, John Nchimbi amesema uvumi wa kwamba matokeo hayo yako tayari ulitokana na kuzushwa kupitia mtandao wa kijamii (Facebook).Alifafanua kwamba habari kuwa matokeo hayo yameanza kutoka kisirisiri kabla hayajatangazwa rasmi na kwamba hatua hiyo inalenga kuyachakachua, siyo taarifa sahihi.Aliwataka wananchi kuwa makini na uvumi huo kwa vile endapo matokeo hayo yatakuwa tayari yatatangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo na pia kuwekwa kwenye tovuti ya Baraza pamoja na wananchi kuweza kuyapata kupitia simu zao za mkononi.
Kuna Maoni 6 mpaka sasa.

 1. Mkweli Anasema:

  Hongereni sana kwa kufafanua jambo hili. Kuchakachua si jambo geni.

  Ingefaa NECTA iweke tarehe maalumu ya February ambayo itakuwa ndiyo tarehe na siku maalumu ya kutoa matokeo ya Kidato cha Nne. Tarehe maalumu kwa kutoa matokeo ya Kidato cha Sita n.k. Kusema tu yanatoka February. Mwezi ni mrefu kwa hamasa inavyokuwa!

 2. KYAKU KUMYENSA Anasema:

  NAWAPONGEZA JOPO LA MICHUZI BLOG, NA HII IWE FUNDISHO KWA BLOG UCHWARA ZINAZOJIFANYA NI MANAIBU MAKATIBU WA NECTA/ WIZARA NA KUSAMBAZA HABARI ZA UONGO IKIWEMO KUWEKA TOP TEN YA WALIOFAULU. AIBU KWAO KWANI WANARUDISHA MAENDELEO NYUMA

 3. amani tesha Anasema:

  mi naishauri necta ituweke wanafunzi katika hali itayotufanya tujijue tulipotoka na tunapokwenda tena kwa wakati yaani iwe inatoa tarehe maalum ya kutoa matokeo

 4. Vizuri wamesema wenyewe maana kila mtu alikuwa na tetesi zake

 5. Unknown Anasema:

  matokeoo yanatoka lini tena brotherr


 6. kikubwa wekeni tarehe maalumu ya kutangaza