THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATANGAZWA LEO

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa na QT.

Jumla ya watahiniwa waliofaulu kwa Mujibu wa Matokeo hayo ni 23520 kuanzia daraja la I hadi la IV huku katika mchakato huo wasichana waliofaulu katika mchakato huo ni 7178 na wavulana ni 16342.Aidha Waziri Kawambwa amesema kuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza ni 1641, daraja la pili ni 6495 na daraja la tatu ni 15426 na waliofeli ni 24903.

Shule bora ni pamoja na St. Francis Girl ya Mbeya, Marian Boys ya Bagamoyo, Feza Boys Dar es Salaam, Marian Girls Bagamoyo na Simini,hizo ndizo zilizopo kwenye tano bora huku shule nyingine ni Kanosa, Jude, St. Mary.


Kuna Maoni 12 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Asnte Mh.Kawambwa.

  KWENU BARAZA LA MITIHANI(NECTA).Matokeo kwenye website yenu ni kitu kizuri sana.Nawapongeza sana kwa hilo lakini kwanini msipange majina ya shule kwa ALPHABETI??.Yaani mtu unatafuta shule hadi macho yanauma.Wape kazi vijana wa IT wako wengi mtaani hawana ajira mtaani.

  David V

 2. Anonymous Anasema:

  Bofya kwanza wewe , ukishayaona ndio nasi tubofye

 3. Anonymous Anasema:

  sasa walio feli mbona namba yao ni kubwa zaidi hata walio fanya mtihani..je hii ni typo error au ndiyo report kamili

 4. Anonymous Anasema:

  Asante kutupa taarifa, ila hizo link za baraza mbona zote hazifanyi kazi??

  Naelewa wanaopenda kuangalia matokeo tuko wengi ila hata kufungua page ya kwanza ni shida??? jamani

 5. Anonymous Anasema:

  mbona matokeo yenyewe hatuyaon???????????????????? tunaona ya miaka iliyopita tu

 6. Anonymous Anasema:

  Wakiofaulu Div I mpaka Div IV ni 23,520 na waliofeli ni 24,903.

  Hivyo asilimia ya watahiniwa waliofaulu ni 48.5% na waliofeli ni 51.43%.

  Taarifa hii inasemazaidi ya nusu ya watahimiwa wamefeli.

  Tunaomba takwimu za ufaulu wa watahiniwa wa kidatu cha nne miaka ya 1980, 1990 ili tuone kama kuna maendeleo ya kielimu kwa kutumia asilimia ya ufaulu wa wanafunzi na kama hali inaporomoka tujiulize ni kwa nini?

 7. Anonymous Anasema:

  Mm jamani hiyo Website ya matokea kanyaboya maana imewekwa lakini kufunguka kwake sijui hadi YESU atakaporudi.

 8. Anonymous Anasema:

  Labda sijui mahesabu jamani au ni macho yangu. Ukijumlisha waliofaulu
  Daraja la kwanza 1641
  Daraja la pili 6495
  Daraja la tatu 15426
  Jumla ya waliofaulu ni 23562. Tunaambiwa waliofaulu ni 23520 sasa hao 42 wanetokea wapi?

 9. Anonymous Anasema:

  Matokeo ndivo yalivyo au usahishaji mbaya? Kuna shida gani? wanafunzi wabovu? au waalimu wabovu au hawakuandaliwa vizuri, au vitendea kazi? au ni vituko gani hivi? mbona sijaamini macho yangu?

 10. Mkweli Anasema:

  Someni vizuri tangazo. Kweli mchambuzi wa hapo juu, waliofeli ni 51.34%. Halafu Bunge likiambiwa mfumo wa elimu Mbovu wanachachamaa. Ilhali takwimu ziko wazi. Matokeo ya miaka iliyopita, ndenda ktk website ya NBS. Kila mwaka unaposonga kufeli kunazidi.Hawa watoto watakuwa wageni wa nani katika hii karne ya Info Tech??? Uongozi kazi kweli kweli

 11. Anonymous Anasema:

  Mdau wa Sita hapo juu anony wa Mon Feb 18, 09:00:00 pm 2013

  ..Tunaomba Matokeo ya Miaka ya 1980 na 1990 ili tulinganishe!

  Mdau kwa kweli Kiwango cha Ubora wa Elimu nchini kinazidi kuzama Kaburini!

  Tukumbuke usemi usemao ya kuwa Kuelimika sio kuvuka Vidato au Kufaulu sio uwezo wa kujibu maswali mengi ya Mitihani kwa Ufasaha bali KUELIMIKA NI KUPOKEA MTAALA ULIO KIDHI MAHITAJI NA KUHITIMISHA MLOLONGO WA MASOMO (SYLABUS COVERAGE)

  Tukilinganisha Matokeo ya Ufaulu wa Miaka ile 1980 na 1990 tutaona waliokuwa Wanafaulu ni Wachache isipokuwa wanakuwa wana Kiwango cha juu ktk Kuelimika kuliko Kufaulu kwa idadi kubwa ya Utitiri kwa Wanafunzi wa Miaka hii huku wakiwa na Kuelimika kuliko chini ya Kiwango.

 12. Anonymous Anasema:

  Elimu nchini ipo Kaburini kitambo tu, ilikwisha fariki tokea mwaka 1997 ilipobadilishwa Mitaala kwa mara ya kwanza.

  Ndio maana hivi sasa tunashuhudia % asilimia kubwa za Ufaulu wa Mitihani huku Viwango vya Taaluma Kielimu hakuna kabisa!

  -Tumeshuhudia Mwanafunzi anafaulu hajui kusoma na kuandika!

  -Mwanafunzi anaandika akichanganya herufi kubwa na ndogo!

  -Mwanafunzi anaandika jina (tena kwa hati mbaya kabisa) ktk sehumu ya Namba ya Mtihani!

  Hivi kwa mazingira hayo hapo juu tuna cha kujisifu kuhusu Kiwango cha Elimu nchini???